Jihadhari utaishia Shimo la Tewa

Jihadhari utaishia Shimo la Tewa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,068
Kuna thread iliyotikisa usiku wa Jana mpaka muda huu ihusuyo wachumba wa JF. Mhanga wa hiyo habari ameamua kuvunja ukimya na kuweka kila kitu hadharani kwa masahibu aliyokutana nayo kwa wachumba aliowapata kupitia hapa jamvini.

Mengine mengi ni mambo binafsi nje ya jukwaa lakini baya zaidi ambalo linaweza kuathiri jukwaa ni hili la mtu moja kuwa na multiple IDs na kufanya mambo ya ajabu.

Dada muathirika amefungua njia kwa kuweka uozo wa wahusika jamvini sense mbali zaidi aripoti hili jambo kwa mods aweke ID zao zote na ikibidi wapigwe life ban.

Wakati Wengine tukichukulia jukwaa ni sehemu ya kukutana na kubadilishana mawazo uzoefu na kupeana maarifa na elimu kuna wapuuzi wachache wamegeuza jukwaa kama kijiwe cha ghiliba na mambo ya kishenzi.

Kama unajitambua una tabia hii acha la sivyo UTAISHIA SHIMO LA TEWA
 
Kuna thread iliyotikisa usiku wa Jana mpaka muda huu ihusuyo wachumba wa JF. Mhanga wa hiyo habari ameamua kuvunja ukimya na kuweka kila kitu hadharani kwa masahibu aliyokutana nayo kwa wachumba aliowapata kupitia hapa jamvini
Mengine mengi ni mambo binafsi nje ya jukwaa lakini baya zaidi ambalo linaweza kuathiri jukwaa ni hili la mtu moja kuwa na multiple IDs m

Ni kweli mkuu.... wenye mapenzi ya kweli tupo huku uswazi ..sio JF.
 
Yani nashindwa hata kushangaa, mtu Ana ID zaid ya moja , anaanzisha thread af anajijibu mwenyewe......pumbafuuu thana (kama kinyambe anavyosema)
 
Sioni sababu nyingine zaidi ya kificha uovu na madhambi tu. Lazima multiple IDs zinahusiana na ubazazi. Nikimtongoza Khantwe (samahani kwa kukutaja) kwa kitumia Eli79, siwrzi kumtongoza ICHANA (samahani tena) kwa ID hiyo coz huenda wanajuana na kuambiana mambo...so lazima mmoja nitatumia ID nyingine. Hata #LoveConnect mara chache utaona hizi common IDs, nyingi huwa ni mpya...something fishy is going on aisee
 
Last edited by a moderator:
Yani nashindwa hata kushangaa, mtu Ana ID zaid ya moja , anaanzisha thread af anajijibu mwenyewe......pumbafuuu thana (kama kinyambe anavyosema)

Ina maana mods hawajamstukia tu, dah wangemerge IDs zake pangekuwa patamu aisee....
 
kuwa na ID nyingi ili iweje!!! ni ulimbukeni na utoto tu
 
Ina maana mods hawajamstukia tu, dah wangemerge IDs zake pangekuwa patamu aisee....

watamerge vipi ?
wakati email unafungua kama unavyokula
kiufupi mimi nina email zaidi ya moja
ila nina id moja nikiamua email zote nafungulia id
hapo utamerge vipi ?
 
Sioni sababu nyingine zaidi ya kificha uovu na madhambi tu. Lazima multiple IDs zinahusiana na ubazazi. Nikimtongoza Khantwe (samahani kwa kukutaja) kwa kitumia Eli79, siwrzi kumtongoza ICHANA (samahani tena) kwa ID hiyo coz huenda wanajuana na kuambiana mambo...so lazima mmoja nitatumia ID nyingine. Hata #LoveConnect mara chache utaona hizi common IDs, nyingi huwa ni mpya...something fishy is going on aisee

Hahahah...hem na wewe niambie id zako zote pliiz
 
Last edited by a moderator:
Je mshana jr una uhakika na huyo pia kama ni habari ya kutunga au ni kweli, tatizo JF kutofautisha hadithi na matukio ya kweli ni ngumu sana, ila ulichoshauri kifanyike ni muhimu.
 
Story ya kutunga inajulikana na ya kweli inajulikana. Hii ni habari ya kweli na ameweka na mfano wa post nyingine ya jamaa inayosema natafuta shemale
 
Last edited by a moderator:
Story ya kutunga inajulikana na ya kweli inajulikana. Hii ni habari ya kweli na ameweka na mfano wa post nyingine ya jamaa inayosema natafuta shemale
mhhhh kama ni hivyo basi balaa, nimekuelewa sasa mkuu na yeye anatoka wapi na hiyo sampuli...pole yake sana
 
Hahahah...hem na wewe niambie id zako zote pliiz
Sina zaidi ya hii uionayo coz sina mission yoyote zaidi ya social interaction hapa...!
...wewe je, tena naifaham ile nyingine...!
 
Nimeogopa sanaaaaa
Ndukiiiiiiii

Usipokuwa makini humu unaweza kukuta unachat na popobawa lolz.

TRUST NO BODY
 
Sina zaidi ya hii uionayo coz sina mission yoyote zaidi ya social interaction hapa...!
...wewe je, tena naifaham ile nyingine...!

Well....kama unaifahamu bas siri yakoo
 
mhhhh kama ni hivyo basi balaa, nimekuelewa sasa mkuu na yeye anatoka wapi na hiyo sampuli...pole yake sana

Kuna watu machoni ni malaika lakini mioyoni mwao wamebeba siri kubwa ni zaidi ya vampires
 
nahisi adm ya jf haifuatilii registration ya members kwa ukaribu otherwise wangeshashtukia vitu kama hivyo,labda iwe ile form tunayojaza ni kufurahishana tu haina mantiki yoyote
 
Back
Top Bottom