Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,454
- 872,068
Ilipaswa mpaka muda huu tuwe tayari tuna watuhumiwa wetu lockup! Watuhumiwa wale familia 12 Tanzania kama wanafunzi wa Kristo aliyezaliwa jana. Jiulize ni kwanini mpaka sasa ziko huru na viongozi wakuu wameishia tu kutoa onyo kwamba waache maramoja shughuli zao za kilimo la sivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria! Yaani mamlaka zinafanya patano na watuhumiwa wenye kidhibiti mkononi
Hapa tumepigwa changa la macho kwakuwa nani amwajibishe nani.. WANAJUANA! Wamegaina mapande ya kupata minofu ya taifa, wewe mlalahoi utaishia kudanganywa tuu
Kuna familia 12 za bonde la Ihefu
Kuna familia 12 za miundombinu
Kuna familia 12 za mapato
Kuna familia 12 za maliasili
Kuna familia 12 za manunuzi
Kuna familia 12 za mafuta
Kuna familia 12 za uwekezaji
Kuna familia 12 za ardhi
Kuna familia 12 za kadhalika na kadhalika bila kusahau nishati na vitenge na mawasiliano
Hizi zote zinanyoosheana vidole kwa mbali tu lakini hawagusani.. Kila kundi wanakula kwa urefu wa kamba zao... Hawa ni the untouchables kwenye hili taifa.. Ukisikia chama kina wenyewe ndio hawa sasa!
Sakata la bonde la Ihefu lilikuwa ni sinema fupi kwa ajili ya uzinduzi wa bwawa la kufua umeme la Nyerere lenye figisu nyingi, matamko na fafanuzi zinazochanganya na kuchosha akili sana
Jukwaa lile la wahariri lenye taarifa kamili kuhusu wavamizi 12 wa Ihefu mpaka wa leo halijaweka wazi majina ya wahusika zaidi ya kuishia kusema watamkabidhi makamu wa rais! Lakini kuna cha kujiuliza hapa ni nani alifadhili safari yao ile na ni nani aliwapa 'nguvu' walau wa kuzitaja hizo familia 12?
Baada ya uzinduzi kwisha habari ya Ihefu nayo baibai, kilichofuatia ni ufafanuzi toka kwa mhariri mmoja kwamba zile familia 12 zipewe muda ama zigikiriwe vinginevyo kwakuwa zimewekeza sana pale kwenye lile bonde
Zimewekeza kwenye miundombinu
Zimewekeza kwenye vitendea kazi kama mashine nk
Zimekopa mikopo mikubwa kwenye taasisi za kifedha
Zimewekeza muda na pesa nyingi
Zimejenga mtandao wa ajira unaotegemewa na wengi ambao wataathirika kwenye huduma za msingi. karo za watoto nknk
Yaani watuhumiwa wanapata watetezi wa wazi na mchana kweupeee!
Sakata la bonde la Ihefu ni kina kirefu.. Masikio yetu yazoee tu kusikia mikwara hii ya wanasiasa tujifanye kukubali tunachoambiwa tuinue tanga maisha yasonge..
Tumeambiwa ni FAMILIA 12 ZENYE NGUVU TANZANIA! Hiyo pekeyake inatosha kukupa tahadhari kwamba USIJARIBU KUPAMBANA NAZO! Utaishia shimo la tewa la bongo
Wahariri wale waliingiza siku yao
Mzee mpango aliyekuwa mgeni rasmi hakualikwa kwenye uzinduzi pengine hata wale wahariri
Tusiandike sana haya mambo bali tuandike tu kujifariji.. Nchi wameigawana hii kwa mafungu ya familia 12 12..[emoji24]