Jihadhari na simu za mitandao ya Kikorea, China na Marekani

Jihadhari na simu za mitandao ya Kikorea, China na Marekani

Wiki kadhaa zilizopita nilikuwa na ndugu yangu mmoja mitaa ya Aggrey tukitafuta simu aina ya galaxy Note 4 mpya, huwezi kuamini tulizunguka maduka yanaweza kufika hata 100 lakini hatukupata hata note 4 moja ambayo ni ya kimataifa (Africa pia) zote zilikuwa ni simu ambazo wamezitoa kwenye mitandao ya simu ya Kimarekani, Korea na China pamoja na nchi nyengine kubwa kubwa. Simu hizi nyingi zilikuwa zimelokiwa na jamaa wamezi unlock na pia ni mbaya kwa matumizi yetu ya kitanzania, leo hii nimeona niandike thread hii kuelezea madhara ya hizi simu na pia tuelezane njia za kupunguza hayo madhara kwa wenye nazo.

Hupati updates, warranty wala support yoyote
Unaponunua simu hizi usitegemee kupata updates badala yake ukitaka update inabidi udownload manual, vile vile hata kama simu ni mpya ikiharibika inabidi urudishe ilipotoka. mfano una galaxy s7 ya kikorea ukiwapelekea samsung Tanzania hawatakutengenezea sababu haiwahusu. Hata mwenye duka akikwambia anakupa warranty ni muongo tu labda airudishe alipoitoa kama atakua tayari.

Zinasumbua ussd
Umeshanunua simu ukaona ukiuliza salio *102# inakubali lakini mpesa, tigopesa na vyengine vinakataa? ukiona hivyo ujue tayari upo mkumbo huu umeuziwa simu za kikorea na wenzie
connection-problem-invalid-mmi-code.png


Muda wote zinaandika 4g au kutoshika kabisa 3g
Watu wengi hufikiri simu zao zina 4g kumbe hazina, mitandao mingi ya kimarekani na baadhi ya nchi wanaitwa hspa+ kama 4g kitu ambacho sio sahihi, hivyo simu hizo zikija hapa kwetu huandika 4g hata kama mtandao ni wa 3g, ukiona simu yako ipo hivi ujue umeshauziwa hizi simu, pia kuna mitandao kama T-mobile band yao ni 1700mhz hivyo simu zao zinaweza zisishike kabisa 3g huku kwetu

Simu za CDMA na band tofauti
Pia simu hizi zipo za CDMA zinaweza kuja Tanzania zisishike kabisa network ukapata pengine 4g tu, na hio 4g inaweza iwe ni band ambazo hazikubali kwetu, mtandao pekee wa Tanzania wenye band za kichina china ni smart band 2300mhz hivyo ukiwa na simu ya namna hii angalia mtandao wa smart.

Zinakuja bila google play store
Nchi kama China playstore kwao sio maarufu, hivyo simu zao zikija huku kwetu zinasumbua unakuta haina playstore wala app yoyote ya google hivyo kuanza kukuhangaisha kuweka hizo app sometime inabidi hadi uflash simu

SMA charachter sio 160
Kikawaida sms moja huwa na herufi 160 (pamoja na space na namba) lakini simu hizi huwa na herufi chini ya 160 hivyo utakatwa hela nyingi zaidi pamoja na kuharibu mfumo mzima wa kutumiwa mfano mtu akituma msg ya 160 kwako itakuwa kama msg 2. kwa wale wanaotuma msg ni muhimu hii.
jw-ucEQB3dwV42Bl8OMBJR51HbdW-0rLyJoJvOsrr2IP_b2-LlhJd0Cx-qaW0JqM_54=h900

mfano hii ina charachter 70 tu hivyo msg ya 160 itahesabika kama sms 3

Dialer ya kikorea au kichina
Pia inaweza tokea dialer (ya kupigia simu) ikawa mfumo wa kikorea
main-qimg-6a4e834ec4324839357802e8b65ec023


Support ndogo ya developers
Pia simu hizi huwa na custom rom chache au usipate kabisa, njia za kuroot wakati mwengine zinakuwa ngumu, nyengine zinalokiwa bootloader etc kama wewe ni power user simu hizi zinakuwa pasua kichwa.

Hayo ni baadhi ya madhara ya simu za kikorea, kama kuna mengine nimeyasahau mutaniambia.

Namna ya kujua kama simu ni ya kikorea au international
Kusema simu inaitwa lg g2 au galaxy s5 haitoshi kila simu inakuwa na model zake, simu moja kama galaxy s5 inaweza kuwa na model tofauti tofauti hata 10, hivyo kujua simu yako fanya hivi

-Nenda setting halafu about utaona model number ya simu
Tap-on-device-name-under-settings.jpg

Ukiipata hio model number angalia online ni ya wapi, site kama gsmarena kwenye specs za simu hueka model na maeneo zinapotoka unatakiwa uwe na model international, au just google simu yako na neno international version kwa mbele, mfano galaxy s5 international version utapata model ya international kama huna hio ujue kuna uwezekano kupata madhara ya hapo juu

-Njia nyengine ni kuregister na warranty ya samsung sema njia hii ni kwa simu mpya zilizotoka chini ya miaka miwili iliopita.. utaandika neno REG*imei# halafu tuma kwenda 15685 utajibiwa, badili neno imei na imei halisi ya simu

jinsi ya kupunguza madhara ya simu za kichina

1.Badili app husika
Mfano dialer ina maneno ya kikorea nenda playstore install dialer nyengine tumia

2. Badili rom
Unaweza ukaeka custom rom kama cyanogen hii itasolve matatizo mengi tu

3. Mods mbali mbali
Kuna simu zinakubali kubadili bands zake na kueka bands za nchi yako, kuna mods za bootloader kwa wale ambao rom za international zinakataa etc

Una tatizo la simu za Kikorea? Usisite kulitaja hapo chini.
ukiona kitu kimevuka miaka miwili kurudi nyuma ndo unazo ambulia hizo
 
Habari!na samsung g906k ya kikorea haikubali ussd na wala iwez change network type imean 3g ,4g but automatic ina jicontrol kama eneo la 4g na nimepata hilo tatizo nilipopata update ya android 6 unaweza nisaidia kusolve@chief-mkwawa
nikupe tu njia ya kupunguza tatizo.
1. downloads apps za miamala ya pesa kama app ya tigopesa na mpesa.
2. kwa voda wana app ya kujiunga vifurushi.
3. jiunge vifurushi vya muda mrefu.

kwa hio 3g na 4g angalia hii code kama inafanya kazi *#*#4636#*#* ili manual uweze kuforce ikae 4g.
 
unalipiaje kitu playstore kwa tigopesa?
Hakikisha una salio lako kwa njia ya tigo pesa .. bonyeza *148*321# kujiunga na huduma hii uweze kununua application kutoka playstore .. then fuata mwongozo huu hapa chini .. chagua kitu unachohitaji kununua then bonyeza neno BUY baada ya hapo zitatokea option za kufanya malipo nawe utaweka malipo yako katika njia ya TIGO PESA utaombwa kufanya usajili wa namba yako basi utafanya usajili na ukimaliza kabisa weka PIN sita ..ukimaliza kuweka njia ya malipo basi bonyeza BUY . kazi kwisha
Screenshot_20180517-155506.jpg
Screenshot_20180517-155506.jpg
 
Hakikisha una salio lako kwa njia ya tigo pesa .. bonyeza *148*321# kujiunga na huduma hii uweze kununua application kutoka playstore .. then fuata mwongozo huu hapa chini .. chagua kitu unachohitaji kununua then bonyeza neno BUY baada ya hapo zitatokea option za kufanya malipo nawe utaweka malipo yako katika njia ya TIGO PESA utaombwa kufanya usajili wa namba yako basi utafanya usajili na ukimaliza kabisa weka PIN sita ..ukimaliza kuweka njia ya malipo basi bonyeza BUY . kazi kwisha View attachment 780011View attachment 780017
ngoja niijaribu.
 
Hakikisha una salio lako kwa njia ya tigo pesa .. bonyeza *148*321# kujiunga na huduma hii uweze kununua application kutoka playstore .. then fuata mwongozo huu hapa chini .. chagua kitu unachohitaji kununua then bonyeza neno BUY baada ya hapo zitatokea option za kufanya malipo nawe utaweka malipo yako katika njia ya TIGO PESA utaombwa kufanya usajili wa namba yako basi utafanya usajili na ukimaliza kabisa weka PIN sita ..ukimaliza kuweka njia ya malipo basi bonyeza BUY . kazi kwisha View attachment 780011View attachment 780017
nimekamilisha usajili mpaka kuweka pini.

tatizo linakuja kwenye playstore sipati option ya tigopesa bali debit/credit card tu. ama ni lazima simu yenye playstore itumie tigo?
 
nimekamilisha usajili mpaka kuweka pini.

tatizo linakuja kwenye playstore sipati option ya tigopesa bali debit/credit card tu. ama ni lazima simu yenye playstore itumie tigo?
Mkuu ukibonyeza sehemu ya kulink credit card angalia payment methods zitajieleza kuna credit card na tigo pesa utabonyeza tigo pesa na kuweka PIN yako baada ya kuweka PIN utabonyeza submit na ombi litakubaliwa
Screenshot_20180517-190336.jpg
 
Samahani. Nipo nje ya mada.
Unaweza kunitajia duka linalouza vifaa vya simu na pc km memory card, harddisk, flash original?
harddisk nenda freedom wapo kkoo uhuru au jmall. wanazo western digital nzuri.

kwa memory card maduka ya camera utazipata ila pia ujue mwenyewe kuangalia nzuri ni ipi.

flash sifahamu na nyingi kibongo bongo si original. jaribu kucheki labda discountkubwa mkabala na kituo cha polisi msimbazi, kuna wakati walikuwa na vile vi sandisk vidogo vya 8gb kwa 10,000.
 
Nilikuwa na Galaxy S4 active ingawa ina 4G lkn ukiweka line yoyote yenyewe inaandika 4g nililetewa used toka US ila mambo mengine yanaenda vzr
 
Tafadhali fuata maelekezo niliyompa chief na hakikisha umeweka lain ya tigo
Mkuu nimefanikiwa kujiunga na hiyo huduma kwa msaada wa maelekezo uliyompa Chief-mkwawa, lakini nikijaribu kununua app playstore sipati opt ya tigopesa kwenye simu natumia laini mbili
Line no 1 ni Tigo
Line no 2 ni Vodacom

NB: Line no 1 (Tigo) ndio niliitumia kama internet connection
 
Hehehe ukakorogea hata mnazi
sio kosa atleast kwa sheria za wenzetu, sidhani kama kuna sheria hiyo hapa kwetu. ukinunua kitu ni chako jinsi ya kukitumia ni wewe mwenyewe, naweza nunua modem nikakorogea sukari.

sema wenzetu mtandao ndio una unlock, mfano umenunua kifaa cha tigo kimelokiwa, hao tigo unawalipa wanaki unlock
 
bado kwangu haiji. nahisi sababu line ya tigo haipo ndani ya simu, nitajiunga tigo nitumie kama primary line then nijaribu. nitakupa feedback baadae.
Mkuu msaada wa kitaalam,7edge proxy sensor ghafla tu aifanyi kazi,imeenda kwa fundi,anadai inabidi simu iflashiwe,msaada mkuu tutani mkuu kama kuna solution nyingine ya kusolve ili ttz
 
Mkuu msaada wa kitaalam,7edge proxy sensor ghafla tu aifanyi kazi,imeenda kwa fundi,anadai inabidi simu iflashiwe,msaada mkuu tutani mkuu kama kuna solution nyingine ya kusolve ili ttz
proxy sensor unamaanisha proximity? hio inaweza sababisha na protector ya simu ama hata uchafu tu juu ya simu,
 
Back
Top Bottom