Jifunze njia rahisi ya ku-root simu

Jifunze njia rahisi ya ku-root simu

Samahani wakuu, nikitaka kuroot Huawei y 330 hizi za tigo nitumie software gani ili niroot kwa urahisi?
 
Mkuu,kwanza ungeanza kwa kutupa shule,ku-root ni kitu gani na kina faida gani,wengine hatujui haya mambo,sio kila mwanaJF humu ni CHIEF MKWAWA
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,kwanza ungeanza kwa kutupa shule,ku-root ni kitu gani na kina faida fani,wengine hatujui haya mambo,sio kila mwanaJF humu ni CHIEF MKWAWA
 
Last edited by a moderator:
Naomba kuuliza.Nime install tayari na imekuja kama mnavyoona hapo kwenye picha.Je cm yangu itakuwa tayari imesha root...??? Tazama picha
 
kwanza naomba ku-declare interest kwenye huu ulimwengu wa technolojia.....pili naomba kuweka wazi kuwa mimi ni mbumbumbu mzungu wa reli juu ya hizi technolojia za simu na mengineyo.....tatu naomba maswali yangu nitayouliza yasionekane ya kipuuzi maana nahitaji kuelewa na kuwa mmoja kati ya wanajumuiya ya technolojia.
maswali ni haya:-
1- mie natumia simu samsung SGH-I927R with 4g je kuna haja ya ku-root cmu yangu?
2- je kwanini ni-root au nisi-root?
3-je kwa ku-root ninaweza kupata features za latest technology za simu say samsung s5?
4-wakati na-root inakuwaje kuhusu data na vitu vingine nilivyosave ndani ya simu?
5-kunauwezekano wa kuongeza size na ukubwa wa storage ya simu au hata memory simu iliyoundwa nayo na kuifanya iwe faster zaidi?

natanguliza shukrani za dhati...wenu mbumbumbu mzungu wa reli.
 
Njia hii inaweza kukubari kwenye vodafone smart 4-min?
 
Who Cares? since wewe ni mbumbumbu. nakushauri usiroot. kuroot maana yake ni kugain root access ya simu yako nna maanisha unapata uwezo kuongeza kubadili au kuondoa baadhi ya mafaili ikiwemo apps ambazo zinakuja na simu by default mfano simu za tigo utakuta zina app km tigopesa na app zingine tunazoziita bloatwares.

rooting ni kwa watu walioadvance kidogo na wanajua wanataka nini baada kuroot. so kama hujui ukiroot inasaidia nini ni heri uache.

ukiroot hupati teknolojia mpya ila ku update firmware version mfano ukiwa na kitkat uki update kwenda lollipop basi utapata features mpya

kuhusu kuongeza ukubwa wa ram au hard disk sijawai sikia labda inawezekana ila mie sijui ila kuongeza speed inawezekana kwa kutweak baadhi ya settings ila inabidi uwe advanced sana kwenye haya mambo

mwisho kufanya modifications kama ku unlock au kuroot kifaa chako kunakupotezea haki yako ya warrant. pia kufanya modifications kunawesa sababisha kuua simu soft brick au hard brick...

USHAURI WANGU: Kama hujui faida au hasara ya kitu unachotaka kukifanya ni heri usifanye mpk pale utakapokuwa na uhakika
 
Last edited by a moderator:
Kila nikijaribu ku-turn on hotspot kwenye simu yangu ya HTC ONE vx ili niweze kutumia Wireless kwenye pc inaniambia

"There is a temporary network problem that prevents the enablement of the mobile Hotspot function. Please retry later"

Je, tatizo ni nini? Au ndo inahitajika niifanyie root? Je root hii inakubalika kwenye simu yangu? Msaada please?
 
Kuroot ndio kufanya nini? Natumia iPhone sijaona kwenye list, je kuna lipi la nyongeza uki-root simu?
 
Back
Top Bottom