Jifunze namna ya kujikinga dhidi ya radi

Nilidhan nikikua hofu itaisha ila wapi hata niwe usingizi nikishaona ule mwanga nashtuka ...radi ikipiga mapigo ya moyo yanaongezeka sana nakuwa na hofu na kutetemeka kabisa sijui nn hunipata ila nateseka sana
Tafuta kale kama ka miwani flani keusi unafunika uso na kuziba masikio huwa kuna vidude vya kuzibia masikio utasikia sauti kwa mbali hivyo usingizi pole pole utakuja
 
Hapa umenivunja mbavu sana mkuu. At first nilidhani wanamfukuza kwa kujali usalama wa huyo mtu kumbe ni kuhofia kulala giza ha ha ha ha
Hahahahaa wewe jamaa umetisha hapo .
Jamaa alifanya kitu cha ajabu sana,yaani tulipokuwa tumejikinga sisi kwenye kibaraza haikuwa ikifika hata mitre 20 kutoka ilipokuwa transformer ila yeye akaona pale ni mbali bora asimame chini yake.

Yaani jinsi raia walivyopandwa na hasira alipokuwa amesharushiwa mawe ya kutosha aligeuza akaenda tena ng'ambo ya barabara huku akizidi kuloa daladala nazo zikamrushia maji machafu basi ikawa tafrani.kwa mda mfupi wote tulikuwa tunacheka jinsi ile sinema ilivyokuwa inaendelea.
 
Tafuta kale kama ka miwani flani keusi unafunika uso na kuziba masikio huwa kuna vidude vya kuzibia masikio utasikia sauti kwa mbali hivyo usingizi pole pole utakuja
Aisee umenikumbusha ,,inakuwa ni kitambaa cha kuziba macho kina mpira vingine vimeandikwa do not disturb ...
Nitavitafuta mana ndio tunaelekea kwenye heka heka
 
Nilidhan nikikua hofu itaisha ila wapi hata niwe usingizi nikishaona ule mwanga nashtuka ...radi ikipiga mapigo ya moyo yanaongezeka sana nakuwa na hofu na kutetemeka kabisa sijui nn hunipata ila nateseka sana
upo kama mm mkuu
 
Radi hutokana na kuachiliwa kwa umeme tuli, tukio ambalo hutokea kutokana na tofauti ya nguvu za umeme kati ya mawingu na ardhi.
Hapa kwenye definition ya radi nimetoka kapa
 
Mtoa Mada shukrani kwa darasa tamu.

Ila urudi kujibu maswali ya wachangiaji ili tujifunze kutokana na maswali yaliyoulizwa
 
Wakati wa mvua, huwa ni kawaida kwa radi kutokea na kila
mwaka watu huuawa katika maeneo mbalimbali duniani baada ya
kupigwa na radi.
Jumamosi, watu 16 waliuawa radi ilipopiga kanisa moja la
kidventista kusini mwa Rwanda.
Meya wa eneo hilo alsiema waumini 140 walijeruhiwa wakati wa
kisa hicho katika kanisa la SDA.
Meya huyo alisema wanafunzi 18 walijeruhiwa baada ya kupigwa na
radi eneo hilo Ijumaa. Mmoja wao alifariki.
Msimu wa mvua za masika unawadia na tayari idara za utabiri wa
hali ya hewa zimeanza kutoa tahadhari.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) tayari imetabiri kwamba
kutatokea mvua kubwa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na
Mtwara wiki hii.
"Wakazi wa maeneo yaliyotajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari
stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari
zinazotolewa," TMA imesema kupitia taarifa.
Kando na uharibifu unaotokana na mafuriko, kupigwa na radi
kunaweza kusababisha maafisa.
Utawezaje kujikinga?



Radi ni nini?
Radi hutokana na kuachiliwa kwa umeme tuli, tukio ambalo hutokea
kutokana na tofauti ya nguvu za umeme kati ya mawingu na ardhi.
Huwa ni cheche kubwa ya umeme kutoka angani, ambayo huwa na
nguvu sana. Inaweza kusababisha moyo wa binadamu kuzima na
kuacha kupiga na pia kuunguza viungo muhimu mwilini.
Zaidi ya robo tatu ya wanaonusurika baada ya kupigwa na radi
hupata ulemavu wa aina fulani ambao hudumu maishani.
Radi hutoka wapi?
Mara nyingi radi hutokea kwenye sehemu ya chini ya anga, ambayo
kwa Kiingereza hufahamika kama 'troposphere'.
Huwa inaenea kutoka kwa wingu moja hadi jingine au kutoka kwa
wingu hadi ardhini.
Radi inaweza pia kupatikana katika mawingu ya majivu kutoka kwa
volkano.
Wanaume hupigwa zaidi ya wanawake
Kwa mujibu wa Taasisi ya Serikali ya Kuzuia Ajali UIngereza
(Rospa), wanaume wana uwezekano mara nne zaidi ya wanawake
wa kupiwa na radi.
Hili inadhaniwa hutokana zaidi na aina ya shughuli ambazo
wanaume hujihusisha nazo, ambapo uwezekano wao wa kuwa nje
wakati wa mvua huwa juu mno.
Wachezaji gofu mara nyingi huwa kwenye hatari zaidi kwani ndio
walio na uwezekano mkubwa wa kuwa maeneo ya wazi mbali na
nyumba au eneo la kujikinga mvua.
Aina tatu za kupigwa na radi
Huwa kuna aina tatu za radi ambazo zinaweza kumpiga mtu.
Moja ni kupigwa moja kwa moja, ambapo radi hukupiga na nguvu
za umeme kupitia ndani ya mwili wako hadi ardhini.
Pili ni kupigwa pembeni, ambapo huwa kitu kilichokaribu nawe
kimepigwa na radi, nguvu zikaruka na kukufikia.
Tatu ni radi inapopiga ardhini na kisha kukufikia.
Utawezaje kujikinga?
Tafuta hifadhi pahali ambapo kuna jumbwa kubwa au ndani ya
gari. Kukiwa na jumba ambalo lina kifaa cha kukinga dhidi ya
radi, utakuwa salama zaidi.
Usiwe katika maeneo ya wazi, au kwenye mlima ulio wazi.
Iwapo utakosa pahala pa kujikinga mvua, punguza uwezekano
wako wa kupigwa kwa kujikunyata na kujifanya mdogo zaidi.
Unaweza kuchutama, kuweka mikono yako kwenye magoti na
kufichwa kichwa chako ndani.
Usijikinge mvua chini ya miti.
Iwapo upo pahala ambapo kuna maji, ondoka na kukwepa
maeneo ya ufukweni yaliyo wazi.
Utafiti umeonesha kwamba kuwa karibu na maji huongeza
hatari ya mtu kupigwa na radi.
Kwa kuwa radi huwa nguvu za umeme, unafaa kujiepusha na
vitu vya chuma vyenye ncha kali ukiwa kwenye mvua.
Kumbuka, hatari ya kupigwa na radi inaweza kuwepo kwa muda
hata baada ya mvua kubwa kuacha kunyesha.


Source Unaweza kujikinga vipi dhidi ya radi?
 
Wakati wa utoto wetu, tulikuwa tunafurahia sana mvua na ule mwanga, tukiamini kuwa ule mwanga MUNGU alikuwa akitupiga picha, ila zile ngurumo tulijua shetani anaburuza mapipa sasa yanagongana (sikumbuki tuliwaza nini hadi kuamini hivyo).
Nakumbuka radi ikimulika tulipenda kusema, MUNGU tupige picha, tutazikuta Mbinguni.
 
Elimu nzuri sana hii,ila nadhan ni kudra za Mungu tu maana kipindi nakua mvua ilikuwa ikinyesha mie na watoto wenzangu tulikuwa tunakimbizana huku tukijificha kwenye miti mirefu ila haikuwahi kutokea ajali mbaya.

Pia hata sasa hakuna anayezingatia haya hata kukiwa na radi za namna gani,just imagine mji kama wa Dar unakuta watu wanajikinga mvua chini ya miti siku hiyo ndezi mmoja pale Ilala Boma ameenda kujikinga mvua chini ya transformer.

Watu walimfurusha na mawe huku wakimlaum kwamba anataka awalaze gizani kama radi ingemchapa.elimu kama hii inafaa itolewe pia kwenye radio na tv stations ili kuwafikia wengi zaidi.
Ha ha ha ha ha ha ha ha
 
Back
Top Bottom