kwasukwasu
Senior Member
- Jun 15, 2016
- 120
- 134
Swala mmoja alipatwa na kiu. Akaenda kwenye bwawa moja la maji. Bwawa hilo lilikuwa na maji safi yaliyotulia. Akainama na kuanza kunywkuanza kunywa maji
hayo.Swala akaiona sura yake kwenye maji yale yaliyotulia. Akaona pembe zake, akajisikia fahari sana. Akajiambia “Dah nna pembe nzuri sana”. Wakati anajiangalia miguu, akajisikia vibaya sana na kulaani alivyoumbwa na Mungu. Akiwa bado hajatimiza kiu yake, alimuona mwindaji akiwa na silaha zake. Akaona
hatari ya uhai wake na kuanza kukimbia kwa kasi kubwa kujiokoa. Akafanikiwa kutokomea mbali na upeo wa mwindaji yule na kufika katika msitu mnene lakini kwa bahati mbaya pembe zake zikakwama kwenye kichaka na akashindwa kutoka. Akajaribu kadri awezavyo kunasua
pembe zake bila mafanikio. Hapo hapo yule mwindaji akaja huku anakimbia na
kumkamata. Swala akagundua kwamba miguu aliyoisema vibaya muda mfupi uliyopita imemsaidia kuokoa maisha yake lakini pembe nzuri alizozisifia zimekuwa chanzo cha kifo chake.