Alexander The Great
JF-Expert Member
- Aug 28, 2018
- 4,514
- 23,701
Habari wana JF,
Bila kupoteza muda, acha nijikite kwenye mada husika.
Palikua na MFALME na MWENDAWAZIMU ambao walikutana makaburini.
MFALME: "Imekuaje wewe unaishi makaburini siku zote??? Na hutaki kuondoka mahala hapa??? Je huna hata chembe ya akili hata ya kukuonesha matatizo ya hapo unapoishi???".
Ni swali alilouliza mfalme baada ya kumuona yule mwendawazimu amejenga kibanda makaburini.
MWENDAWAZIMU: "Nadhani itakuwa wewe ndie hujielewi!!! Au pengine huna hata chembe ya akili!!!"
MFALME: "Kwanini unasema hivyo???!!!"
MWENDAWAZIMU: "Mimi nimeona hakuna nyumba ya kubaki na kudumu ila hizi hapa, nikaamua kusogea karibu na hapa!!! Ila wewe umeona fakhari kujenga kasri ilio kubwa na yenye ulinzi mkali sana, kisha ukapakimbia mahala hapa, unasahau kama nawe ipo siku utaliacha kasri lile, hao walinzi uliowapa kazi ya kukulinda usiku ma mchana hawataweza kuizuia roho yako ikitaka kutoka, na kisha utaletwa hapa" kisha akauliza;
**Kwanini usijiimarishe na usipaimarishe hapa???
**Kwani hawa hawakua RAIA zako???
**Kwani hawa hawataki tena kuishi vizuri???
**Kwani hawa hawataki kutembelewa tena???
**Pamoja na ufalme wako umeshindwa kuweka waangalizi mahala hapa ambapo kila mtu atarejea???
**Umejenga kwa gharama kubwa nyumba utakayoiacha baada ya MAUTI na kuitupa nyumba utakayoishi milele???
**Kwanini hauwausii raia wako na kuwakumbusha kuhusiana na mahala hapa (kifo)???
**Kwanini unajilimbikizia utajiri na kusahau shida za raia wako wenye hali za chini???
MFALME alibubujikwa na machozi huku akisema "SIO KILA MWENDAWAZIMU NI MWENDAWAZIMU, nimekosaje chembe ya akili mimi kufahamu haya????!!!
MFALME akamwambia MWENDAWAZIMU "omba chochote utakacho nami nitakupa".
MWENDAWAZIMU akasema naomba mambo matatu;
1) Naomba uniongezee umri wangu wa kuishi duniani.
2) Naomba unipe ulinzi mkali (kama ulioweka katika kasri lako) siku atakaponijia MALAIKA MTOA ROHO (kifo) ili asiweze kuitoa roho yangu.
3) Naomba unihakikishie kuingia peponi.
MFALME akapiga kelele sana!!!
MWENDAWAZIMU: "Nani kati yetu Mwendawazimu???"
MFALME: "Ni mimi, ni mimi, ni mimi.!!!"
MWENDAWAZIMU: "Kwanini???
MFALME: "Yote uliyoyaomba sina uwezo nayo, na nilikuwa natembea kwa fakhari sana kifua mbele, kwa dharau, kwa majigambo, kwa kebehi, nikimuadhibu raia yoyote asie niheshimu, na kusahau masikini, NIKIDHANIA nina uwezo kumbe mimi si lolote si chochote!!! Hata mimi mwenyewe hayo siwezi kujipatia!!!"
Basi Mwendawazimu akamwambia yupo anaeweza, nae ni MUNGU MWENYEZI ndie MFALME wa kila kitu, nami na akili zangu zote zimekwisha kumfikiria yeye!!! Kua mtawala mwenye kutenda HAKI & UADILIFU nae atakuongoza salama.
____________Mwisho___________
Jifunze kitu hapo rafiki yangu, sio kila wakati hadithi za mapenzi, hapana.
LIKE au TAG rafiki yako kipenzi kumkumbusha haya.
Ahsante,[emoji18]