Jifunze kilimo cha nyanya

Ekari moja umetumia gharama kiasi gani na mavuno umepata tani ngapi

Tunauza kwa box sio kwa kilo, unapata box nyingi kama utalima kwenye shamba zuri na utahudumia vzr

Heka moja inaweza kugharimu mil 2-3 itategemea na changamoto za magonjwa na madawa kadri inavyojitokeza

faida itategemea na bei Ila ikianzia 10000 tu unapata faida, sababu inatoa box nyingi na unavuna sn. ukianza kuchuma unachuma kila wiki sasa hizi nyanya zina michumi mingi inafika hadi michumo 9.
 
ni 560,000/= zina gharama sn Ila zinazaa sn ni kubwa na ngumu wafanyabiashara wanazipenda sn zinafanya vzr sokoni hata bei take tofauti na za nyanya za kawaida
Mkuu hizo 50g zinakuwa na miche/Mashina mangapi? Na gharama za kuandaa/kulima /operational cost za shamba la mbegu 50g in kiasi gani na mavuno take in kiasi gani
 
Mkuu hizo 50g zinakuwa na miche/Mashina mangapi? Na gharama za kuandaa/kulima /operational cost za shamba la mbegu 50g in kiasi gani na mavuno take in kiasi gani
miche ni mingi huwezi kuhesabu Ila inatosha heka 1 na kubaki inaweza kupanda heka 1 na nusu kama hazita kufa sana maana kuna zoezi la kurudishia miche kwenye mashimo yaliyokufa.

Hiyo gharama niliyokwambia nimejumlisha kila kitu kuanzia kukodi shamba, kulima kwa trekta, kupiga shimo, kupanda, kurudishia, palizi, madawa yani kila kitu hadi kuvuna.
 
Shukran kwa elimu
miche ni mingi huwezi kuhesabu Ila inatosha heka 1 na kubaki inaweza kupanda heka 1 na nusu kama hazita kufa sn maana kuna zoezi la kurudishia miche kwenye mashimo yaliyokufa

hiyo gharama niliyokwambia nimejumlisha kila kitu kuanzia kukodi shamba, kulima kwa trekta, kupiga shimo, kupanda, kurudishia, palizi, madawa yani kila kitu hadi kuvuna
 
Mkuu hizo 50g zinakuwa na miche/Mashina mangapi? Na gharama za kuandaa/kulima /operational cost za shamba la mbegu 50g in kiasi gani na mavuno take in kiasi gani
Mkuu mavuno ya nyanya yapo hivi, sisi tunauza kwa box, na tunavuna kila wiki.

Sasa ule mchumo wa kwanza tunaita fundisha, sasa mfano mchumo wa kwanza ukichuma box 20 utaangalia na bei itakavyokuwa sokoni mfano ikiwa 10000 utapata 200,000/=

Utakuja mchumo wa pili box zinaongeza unaweza kupata box 60 pia utazidisha kwa bei iliyopo sokoni au tufanye ile ile 10000 utapata 600,000/=

Mchumo wa tatu unaweza kupata box 120 pia utazidisha kwa bei

Mchumo wa 4 utaweza kupata box 180 pia utazidisha kwa bei

Mchumo wa 5 unaweza kupata box 240 utazidisha kwa bei,

Baada ya hapo nyanya nitaanza kupungua mchumo unaofata zitarudi 180 alafu 120 alafu 60 mwisho 20 biashara imeisha

Utajumlisha kila mchumo umepata bei gani utatoa na gharama ulizotumia

Hizo bei ni mfano zinaweza kuzidi au kupungua
 
kwa mbegu za kiwaida riogrand inafanya vzr Ila sio kama sawa na mbegu za kisasa

kuhusu bei ikianzia 10000 ni bei nzuri inalipa gharama na faida unapata kubwa tu
Sasa mkuu kwamimi nisieweza kununua hiyo mbegu gharama kubwa je kwambegu hizi zakawaida unanishauri ninunue mbegu gani?
 
Mkuu shina moja linaweza litatoa kilo ngapi kuanzia mchumo wa kwanza mpaka wa mwisho?
Mkuu hatuuzi kwa kilo tunauza kwa box kama hivi.

3f88b295694d4f25b33c0e3d3733e078.jpg
 
mbegu zipo kwenye makundi mawili, kuna mbegu za kawaida na mbegu za kisasa
kwenye mbegu za kisasa assila inafanya vzr sn japo bei yake kubwa Ila zipo mbegu zengine za kisasa zenye bei nafuu mf kilele, Monica f1, kipato nk
Tatizo sisi wageni wa mbegu ni vigumu kuzijua maana kila kampuni ya kuuza pembejeo inaipa mbegu jina lake kulingana na brand ya kampuni yake hivyo unakuta mbegu ya aina moja inakuwa na majina mengi kutokana na kampuni inayoizalisha
 
Sasa mkuu kwamimi nisieweza kununua hiyo mbegu gharama kubwa je kwambegu hizi zakawaida unanishauri ninunue mbegu gani?
Mkuu riogrand nibora kuliko mkulima? Au Tanya kwa uzoefu wako inaweza kunilipa ikiwa ntaihudumia vizuri ?navip naweza kuotesha kitalu kwasasa vip soko lake litakua zuri.

Nipo Bagamoyo
 
Tatizo sisi wageni wa mbegu ni vigumu kuzijua maana kila kampuni ya kuuza pembejeo inaipa mbegu jina lake kulingana na brand ya kampuni yake hivyo unakuta mbegu ya aina moja inakuwa na majina mengi kutokana na kampuni inayoizalisha
Kama mgeni tafuta msaada wakati wa kununua mbegu kwa wakulima wazoefu, mbegu zipo aina nyingi zinatofautiana ubora pia uwa wanachakachua.
 
kama mgeni tafuta msaada wakati wa kununua mbegu kwa wakulima wazoefu, mbegu zipo aina nyingi zinatofautiana ubora pia uwa wanachakachua
Hii unayoitumia inasambazwa na kampuni gani? hapo ndio pa kuanzia maana nikienda kibo seeds unakuta ina jina jingine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom