SoC01 Jifunze haya mtandaoni uweze kujiajiri na kuajiri

Stories of Change - 2021 Competition

Tyler Durden

Member
Aug 5, 2021
73
114
Ni jambo lisilofichika sasa kuwa mfumo wetu wa elimu uko dhoofu li hali, kama sio hoi bin taabani. Haumuandai mhitimu kujiajiri au kuweza kutengeneza ajira, hali ni mbaya sana, wahitimu wengi wa elimu ya juu na kati wapo mitaani wakiwa hawajui nini hatima yao.

Viongozi walioshika mpini katika suala hili nao ni kama vile bado wamesinzia kwa kuwa sio wahanga hasa wa tatizo hili, wengi wao ni wanufaika wakubwa wa mfumo wa elimu uliopo sasa.

Maendeleo ya teknolojia yametuletea elimu mpya, elimu ya mtandao. Unachohitaji ni kifaa chako kilichounganishwa na mtandao wa intaneti tu. Hakuna malipo ya ada. Ni wewe na kifurushi chako cha intaneti unabadilisha Maisha yako. haijalishi una elimu au la ukitumia elimu hii ya mtandao vizuri unaweza kujiajiri na kuwapa ajira wengine.

basic-concepts-of-e-learning.jpg

picha na Medical Student Blogs
Haya ni Baadhi tu ya maarifa unayoweza kujifunza bure mtandaoni kwa muda mfupi na kuweza kukusaidia kujiajiri kuingiza kipato na kuweza hata kuwaajiri wengine.

  • Lugha na ukalimani- muingiliano wa watu katika biashara umeleta mahitaji ya wakalimani kuliko kipindi kingine chochote,mfano, Lugha ya kichina inazungumzwa na zaidi ya watu bilioni moja, China inaafanya biashara na mataifa mengi sana ya kiafrika, kufahamu lugha hii ni jambo linaloweza kukusaidia kuingiza kipato. Unaweza kujifunza kichina mtandaoni bure bila gharama yoyote katika mitandao ya , Nciku,BBC Chinese, livemochana Ting.
    d1131d41c2b5adcc56c48b0d8cd3d407f97615ed.png
    picha na Professional Translation Services | Mars Translation
  • Upishi wa vyakula vya mataifa mbalimbali- katika miji mingi mikubwa kuna migahawa inayouza vyakula vya nchi maarufu kwa vyakula vizuri kama China,India,Italy na Thailand. Hii inaonesha kuna soko kubwa la vyakula hivi. Mitandao imeturahisishia leo hii tunaweza kujifunza mapishi ya mataifa haya bure kabisa na kujiingizia kipato na hata kuweza kuajiri wengine. Mitandao kama BBC food techniques, Americas kitchen online,na tastemade ni maeneo unaweza kujifunza bure kabisa.
    culinary_terms-hero-1-@2x-1.jpg
    picha na https://www.gffoodservice.com.
  • Masoko ya mitandao ya kijamii- katika zama hizi za kidijitali kujitangaza katika Mitandao ya kijamii imekuwa ni lazima hasa kwa makampuni makubwa. Hii ni fursa ya kutengeneza pesa nyingi kupitia matangazo, makampuni mengi hayana wataalamu wengi wenye uelewa kuhusu masoko ya mitandao ya kijamii, ukiweza kuwekeza na kufahamu vizuri kuhusu masoko ya mitandao ya kijamii unaweza kutengeneza kipato. Unaweza kujifunza kupitia Google digital garage.
    social-media-marketing.jpg
  • Graphics design- hapa utajifunza program mbili za kompyuta ( Adobe photoshop na Adobe illustrator) hizi zitakuwezesha kutengeneza mabango, kusanifu picha, na kutengeneza nembo za makampuni mbalimbali, kazi hii ni rahisi sana kujiajiri hasa kwa wahitimu wa vyo ambao wengi wao wana kompyuta mpakato. Kuna kozi nyingi sana kuhusu taaluma hii katika mtandao wa youtube.
    images.jpg
    picha na Learn Hub | G2/
  • Sanaa za mikono- niliwahi kukutana na dada mmoja anatafuta chupa tupu za mvivyo,anazisafisha anazipulizia rangi nzuri za kupendeza kisha anazinakshi na maua na kuziuza kama mapambo ya ndani. Elimu hii alijifunza darasani? Hapana alijifunza katika mtandao wa youtube. Yapo mafunzo mengi sana mtandoni yatakayokuwezesha kuingiza kipato kwa kutengeneza vitu mbalimbali kwa mikono yako tu.
    close-up-person-twisting-chenille-stems-wooden-table_23-2147899029.jpg
    picha na freepik
  • Uandishi- uandishi sasa ni taaluma inayoweza kukuingizia kipato hasa katika zama hizi za kidijitali, unaweza kujifunza uandishi wa riwaya, Habari,Burudani, michezo, uchumi, Makala,n.k. baada ya kujifunza na kufahamu kahusu uandisha unaweza pia kujifunza blogu na kuanza kuchapa Habari na hadithi zako ili kuweza kujiingizia kipato kupitia matangazo.
    expert-tips-for-writing-job-posts.jpg
    picha na Learn English Fun Way - Fun and Easy Ways To Learn English
  • Ufundi wa fani zote- kuanzia ufundi wa vifaa vya kielektroniki kama kompyuta, na televisheni, mpaka ufundi wa mikono kama useremala, kuchomea, ushonaji, ufundi magari , umeme n.k unaweza kuchagua fani moja kati ya nyingi zilizomo hasa katika mtandao wa YouTube. Utahitajika kununua vifaa na mashine zinazohitajika katika ufundi husika. Ni muhimu kujipa muda na mazoezi ya kutosha ili kuwa mahiri kabisa kabla ya kuanza kupokea.
    artisan.jpg
    picha na Noyal Muzilak
  • Uchoraji- uchoraji unaweza kukuingizia hadi fedha za kigeni, ni taaluma unayoweza kujifunza mtandaoni kutoka kwa magwiji mbalimbali wa uchoraji, katika mtandao wa youtube kuna video za magwiji kama Bob ross , kevin hii na wengineo watakaokufundisha njia mbalimbali za kuzalisha michoro mizuri unayoweza kuuza na kujipatia kipato.
    the-5-best-free-drawing-and-painting-tools-for-teachers.jpg
    picha na elearning industry
  • Kupiga vyombo vya muziki- kabla ya ujio wa mitandao ili uweze kujifunza kifaa chochote cha mziki iwe gitaa, kinanda au ngoma ilibidi utafute mwalimu binafsi,ni gharama sana. Leo hii unaweza kuwa mahiri sana wa kupiga gitaa kwa kujifunza chumbani mwako tena bure kabisa. Tafuta kifaa chochote cha mziki unachopenda kisha anza kufuatilia mafunzo ya jinsi ya kukitumia. Ukifanikiwa kuwa mahiri unaweza kujiajiri kupiga mziki katika sehemu mbalimbali zenye mikusanyiko au unaweza kuajiriwa kupigia wasanii wakubwa au matukia mbalimbali.
    different-kinds-musical-instruments_1308-3320.jpg
    picha na freepik
  • Michezo mbalimbali- ipo michezo mingi tumeiona hata kwenye michuano ya olimpiki, ambayo haifundishwi popote hapa nchini kwetu, kuna nafasi ya kujifunza michezo hii mtandaoni. Michezo hii ina fursa kwenye Nyanja mbili, moja ni kuwa mahiri katika michezo husika na baadaye kupata nafasi ya kuwakilisha nchi, mbili kuwa mahiri na kuweza kuwa mkufunzi na kufundisha katika shule zinazohitaji kuendeleza wanafunzi wake katika michezo husika.
    Return_of_Sports.jpg
    picha na abssport
  • Kutengeneza na kuhariri video- tupo katika zama za kidijitali ambazo video ni nyenzo kuu ya mawasiliano, kila siku mtu mmoja huangalia wastani wa video kumi. Mitandao ya video kama youtube imetengeneza mabilionea. Ukiwa mahiri katika kutengeneza na kuhariri video zenye maudhui pendwa unaweza kutengeneza kipato kizuri na hata kuajiri, unatakiwa kujifunza program za kuhariri video kama vile Adobe premier na Adobe after effect ambazo mafunzo yake yanapatikana katika mtandao wa youtube.
    high-frame-rate-cover.jpg
    picha na Premiumbeat
  • Programu za Microsoft- programu za Microsoft hasa program ya kujaza takwimu ya Excel, ni moja ya fani zinazoweza kukuingizia kipato. Katika kazi nyingi kama vile uandishi, usimamizi wa miradi, n.k nyingi unahitaji uwepo wa programu hizi ili zikurahisishie kufanya kazi,unaweza pia kujiajiri kama mwalimu wa kufundisha programu hizi kwani ni muhimu kwa kila mtu anayeanza kujifunza matumizi ya kompyuta.
    images (1).jpg
    picha na shardainfotech
  • Kutengeneza App za simu, Tovuti, na kuprogramu- mahitaji ya app na tovuti ni makubwa katika makampuni mbalimbali,yapo mafunzo mbalimbali kutoka mtandaoni yanayokuwezesha kuweza kutengeneza app na tovuti . pia kujifunza programing na coding itakuwezesha kuingiza kipato.
    web-app-1024x540-1024x540.jpg
    picha na AB solutions
  • Kujifunza Yoga- Yoga ni aina mpya ya mazoezi ya viungo na ubongo yaliyoshika umaarufu sana kwa sasa, mazoezi hasa yanasaidia sana afya ya akili, mwili na kiroho, ukipata mafunzo haya unaweza kuanzisha darasa hapa nchini ambapo mazoezi haya hayajashika kasi sana, na kuweza kujiingizia kipato.
    download.jpg
    picha na global circulate
  • Radio mtandao (Podcast)- Teknolojia inakwenda kasi sana, unakipaji cha kuchekesha, kutangaza , kusimulia, au kufanya mahojiano kwa njia ya kuvutia? Huhitaji tena kituo cha redio, unahitaji podcasting… hii ni njia ya kuwasilisha mazungumzo ya sauti kwa jamii kwa njia ya intaneti, wapo watu wengi wametajirika kwa kufanya podcast na kujizolea mashabiki lukuki, unaweza kuanza kujifunza kuhusu podcasting leo.
    download (1).jpg
    Picha na Google
  • Mitandao imetupa fursa ya kupata maarifa ambayo hatukuyapata shuleni, tukiitumia vizuri itatuletea mafanikio, kariibu kwa mchango na maswali.

d1131d41c2b5adcc56c48b0d8cd3d407f97615ed.png


d1131d41c2b5adcc56c48b0d8cd3d407f97615ed.png


download (1).jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom