Jicho lililopotea

Jicho lililopotea

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,208
Reaction score
829,198
Nikiwa mdogo, Mama yangu alikuwa anawasiliana nami kwa macho..., bila kutamka na nilikuwa namuelewa vizuri!!

Jicho hilo silioni siku hizi miongoni mwa akina mama.

Ilikuwa wageni wakija nyumbani, mimi kama narukaruka na kucheza mbele ya wageni bila staha, kulikuwa na namna fulani ya mama kuniangalia ilimaanisha "toka hapa". Nilielewa mara moja na kutii!!

Ilikuwa wageni wakila chakula nami kutaka kudowea, basi kulikuwa na uangaliaji wa mama ambao ulimaanisha " ukijaribu tu nitakuchuna ngozi ukiwa hai!" lakini wakati huohuo kwa wageni uso wake ulimaanisha "endeleeni tu, huyu dogo ameshakula...."

Ilikuwa mkiwatembelea ndugu na ukataka kulilia kitu cha watu, kulikuwa na jicho fulani hivi toka kwa mama lililoonyesha kuwa "Ukifanya ng'ee tu tukifika nyumbani nitakukaba shingo, sitaki ujinga.."

Lakini wanawake wa leo, namaanisha akina mama wa leo ehhh..., vioja. Macho yao yamepofushwa na nini sijui..! Labda ni hizi kope za bandia wanazozivaa au hizi rangi wanazopaka kwenye nyusi!!

Kusema ukweli macho yao hayana mawasiliano na watoto wao

Wazazi wetu wa zamani, Mungu awajaalie maisha marefu. Ninyi ndo mlitutengeneza tukawa hivi tulivyo leo. Hatuna tamaa ya vitu vya watu..........

Nakala:
- Wanaume wote
- Akina mama vijacho wote
 
mzee umenikumbusha mbali mno

mmeenda ugenini wakatenga msosi alafu mkakaribishwa mle,unamuangalia kwanza bi mdashi,kuna namna akikuangalia apo kula,na kuna namna akikuangalia usiguse yani hata kama unanjaa utasema umeshiba afu na yeye anakwambia kulaaa huku anakukata jicho

hatukuwa tunapractice au akinambia ila we had deep connections,tatizo watoto wa sasa hivi wanakua kwa maziwa ya ng'ombe,wanajisaidia kwenye mapoti hawatengwi miguuni,hawabebwi na mama zao na kwenda umbali mrefu na vitu kama hivyo!!
 
Mwenyewe mother nilikuwa nikipewa Chakula ugenini nasema nimeshiba, au pesa na sema ahsante Nashukuru nikimcheki mama naona kabisa kuna jicho linaniambia "Pokea uone ila jua tukifika nyumbani nitakung'ata ng'ata nikuteme"

hapo najichekesha tu ila moyoni najua hapa nikipokea nyumbani itakuwa kipigo chambwa Koko
 
demu wangu hua ananichek kwa jicho la mahaba ad nashusha wakorea hapo hapo.
 
Baba yupo Jf muda wote anashughulika na makundi ya whatsap,mama yupo insta anapambana kulike picha za Wema na yiule Madam wa Uganda,hizo mbinu za macho watazipata saa ngapi wakati wote wapo busy wanatafuta hela na watoto wanalelewa na dada wa kazi.
 
Enzi za utoto wetu mama zetu walikuwa wakiwasiliana nasi kwa usiri pasipo upande wa pili kuelewa nini kinaendelea baina ya mama na mtoto. Unaonywa pasipo mtu wa pembeni kuelewa kama umeonywa au kukatazwa kufanya kitu. Siku hizi hakuna ufundi kabisa katika kulitumia jicho kuwasiliana na mwana na akaelewa wamaanisha nini. Nafikiri ufundi huo umehamia kwenye kuperuzi katika mitandao ya kijamii.
 
Mshana Jr, Hata hivyo mzee mganga ule utamaduni wa kutembeleana na kuonyeshana album za picha, sikukuu kutoka nyumba moja kwenda nyingine hakuna kila mtu kwaoooo. Watoto na ma gemu ya simu, computer nk
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom