Nimeona majibu na hoja za wenzangu pia ni mawazo na asanteni kwa michango yenu katika mada hii,nadhani wengi hamjaielewa vizuri mada yangu lakini pia nimelielezea tatizo na aya ya mwisho nimetoa suluhisho la mada yangu nini kifanyike na pia hii ni kwa kuongea nao moja moja wao wenyewe na asilimia kubwa wana afikiana na mawazo yangu kwamba ndoto zao zinakufa sababu kuna kubweteka na mzunguko wa 5000 hadi 10,000 na starehe ambapo ikitokea na familia ikaingia ile 10000/ inakuwa ndogo mara 2 hiyo inamaanisha tayari maisha yameanza kuwa magumu japo anaenda kazini na boda yake.
lakini pia hata mimi mwenyewe sijaajiriwa nimejiajiri hivyo nnaujua vizuri mziki wa mtaani na ugumu wake,lakini pia nnajua vitu gani vinatufelisha malengo sababu wote tumepitia hiyo hatua sema kwa njia tofauti,ishu kubwa nnayoiangalia ni baada ya miaka 15 - 20 hawa madreva boda wa leo watakuwa wapi na familia zao zitakuwa wapi,sababu asilimia kubwa ni vijana.
Tunahitaji kubadilisha mitazamo sana na kujitambua ili kuweza kuwanusuru,SA ishu ilianza hivi hivi kwa wazawa kuwa vibarua na wageni kuwa na kazi nzuri mwisho wake wote tunafahamu,vitu huanza pole pole vikiwa vinaoenakana vya kawaida ila madhara yake yanaweza kuwa ya muda mrefu,ni sawa na kupanda boda hiyo hiyo halafu ukawa unaendesha kwa kasi bila tahadhari ukifika salama unashukuru ila ukipata ajali ni kilema cha maisha.
Kujitambua ni neno kubwa na pana sana kuliko maana yake.