Jibu nililopewa na idara ya ufundi ya IPP MEDIA limenisikitisha sana!!!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jibu nililopewa na idara ya ufundi ya IPP MEDIA limenisikitisha sana!!!!!!!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KIBURUDISHO, Dec 6, 2011.

 1. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  WanaJF wenzangu mambo vp? natumai mu wazima.Kama mnakumbuka vizuri kwa siku kama tatu zilizopita niliwasilisha hapa mjengoni juu ya suala zima la upatikanaji wa chaneli zote za hapa tanzania kwa njia ya satelite zinavyosumbua.Hivyo leo nikalazimika kuwasiliana na wahusika wa IPP MEDIA idara ya ufundi moja kwa moja na ndipo wakanipatia jibu kuwa;Kwa woote wanaopokea matangazo yao kwa njia ya satelite ya INTELSAT906E kwa kutumia madish ya C-BAND ya ukubwa wa ft sita hawataweza kupokea matangazo yao hivyo wenye uwezo wa kupata matangazo yao ni wale tu wenye madish yenye ukubwa wa ft8 na inatokana na mkataba waliowekeana na hao wenye hiyo satelite kuwa mawimbi yao yanatakiwa yapatikane kwenye dish za ft8 tu wanasema hapo awali walikuwa wanafanya wizi tuu wa kupandisha signal na ndio maana sisi wenye madish ya ft6 tulikuwa tunawapata kwa hiyo kwa sasa hivi haiwezekani kwa sababu wao wenyewe wenye satelite ndio wanawacontrol.Sasa kilio changu ni kwa wale wenzangu na mimi ambao karibia woote nchi nzima tunatumia madish ya ft8,na kwa nini walifikia muafaka wa kuingia mkataba kama huo hali wakijua kipato cha watanzania walio wengi ni cha chini na hii sasa sii kwa IPP MEDIA tu ni kwa chaneli zote za bongo,Nawasilisha.
   
 2. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Naona hii kali. hivi hayo ya futi 8 ndiyo yale ya wavu yanayo-rotate yenyewe? kama mimi sasa hivi naona nashika TBC basi zingine ni chwechwe tu kama vifaranga vya kuku. huoni kitu kabisa.
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  Technology ya kuchagua dish sii technology,bora ingekua receiver!
   
 4. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,139
  Trophy Points: 280
  kumbe ukiwa na dish kubwa zaidi ndio unashika channels nyingi zaidi.
  Mi ntatengeneza dish la futi 12
   
 5. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Oneni gharama wanazotuingiza sasa dish la ft6 yanauzwa kwa sh kati ya sh,80000 hadi 100000 na dish la ft8 yanauzwa kati ya 200000 hadi 250000.Kwani kurusha matangazo kwa satelite ya C-BAND inatofautianaje na kurusha matangazo kwa satelite ya KU-BAND?
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  huu ni ushenzi mwingine.........
   
 7. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,036
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kampuni kama ipp inanunua bandwis chache kwanini ? We mengi acha ubahiri sisi wabongo hatuna uwezo wa kununua dish futi 8
   
 8. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,036
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kampuni kama ipp inanunua bandwis chache kwanini ? We mengi acha ubahiri sisi wabongo hatuna uwezo wa kununua dish futi 8
   
 9. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mkuu mitz haipendi kabisa kuona wengine nao wanaendelea..
   
 10. m

  mhondo JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Wangekuwa wastaarabu wangetangaza kwanza kwa wateja wao kabla ya kupotea hewani ghafla bin vuu.
   
 11. Didia

  Didia JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 721
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Nadhani IPP ni kampuni binafsi hivyo anaangalia faida zaidi. Idadi ya watazamaji wakipungua bilashaka wataangalia upya mkataba wao. Nionavyo mimi bmalalamiko yetu yangekuwa sahihi sana kama tungekuwa tunazungumzia TBCCM. Hatahivyo nashukuru kwa taarifa nimeelewa kwanini chanel za IPP hazipatikani. Nilitaka kumuita fundi kesho aje kurekebisha dish langu kumbe ningeharibu pesa tu.

  2014 mabepari wanabadili teknologia nasikia ndo mwisho wa madishi haya sote tunahamia Ting, Startimes N.k.
   
 12. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #12
  Dec 6, 2011
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  TV za TZ ni wezi tu, yaani wote hawapatikani kuanzia ITV/EATV/Capital/Chanel TEN hadi Star TV halafu wote wapo kimya hamna neno lolote kwa wateja wao...ni TBC1 pekee na chanel za nje ndio zinapatiakana. Inabidi tuwashtaki kwa mamlaka ya mawasiliano au kule huduma kwa walaji labda watapata adabu kdg
   
 13. MGAWARIZIKI

  MGAWARIZIKI JF-Expert Member

  #13
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 306
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli madish sasa imekuwa kero signal hazieleweki unaweza kupata picha safi lakini baada wiki zikaanza kukatakata mbona wenzetu Kenya channel zinapatikana ktk K-U BAND safi bila zengwe au ndio wanataka tuanze kutumia ving'amuzi? mpaka sasa ni kama mikoa 7 tu wanapata signal, pole sana watz maana walio wengi madish yao ni ft 6 hii ni aina nyingine ya ufisadi kuna mtu kashaingia kwenye biashara ya madish ft 8
   
 14. Suip

  Suip JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,039
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  TCRA Kazi yao ni nini, hivi nchi inaelekea wapi, au ni mbinu ya sisi tunaoishi mbali vijijini tusipate mawasiliano ya TV ili tusione midahalo ya katiba mpya ? Mikataba ya dish na satelite inakuwaje?
   
 15. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  kuna fundi mmoja mitaa ya sinza na kimara huwa wanayaunda madishi wenyewe futi 12 ulizeni watu wa sinza na kimara sina hakika watawaambia ni wapi mkachukue kwa bei nzuri.,bahati mbaya sipo dar ngwapata ramani halisi
   
 16. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  TCRA yeye ni kama NATIONAL REGULATORY hawana mamlaka na hao wamiliki wa satellite
  kilichopo sasa ni kuruhusu SERVICE PROVIDER wengi kurusha matangazo ya tv za hapa nyumbani ndio digital system ilivo
  msiwalaumu TV channels kwani kuwa content provider na service provider ni garama sana kwa kuwa hawana uwezo wa kumiliki essential facilities bila kutegemea wamiliki wa satelite ambao wana rules zao
   
 17. Ondio Osio

  Ondio Osio Member

  #17
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 11, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunashukuru mkuu kwaktujulisha.
   
 18. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #18
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Kwa nini wasihamie band ya KU-BAND halafu woote wakatumia Transponder moja kama zilivyo zile chanels za nigeria?????.Halafu kama wangelikuwa waungwana wangelitutangazia kwanza ndipo wachukue uamuzi wa kuhama na hii ni kwa chaneli zote. TBC1 na STAR TV zenyewe zinajitahidi kuonekana kwa sababu signal zao ziko juu sana ndio maana tunawapata kwa shidashida.Jamani hebu angalieni mikataba kama hii mnayoingia harakaharaka sasa sisi watu wa kipato cha chini tutafanyaje.
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,328
  Trophy Points: 280
  Nashauri tuachane na hizi sattelite dish zinazotumia signal za bure kama Intelsat au Nothern Atlantic kwa sababu zote ni analog mwisho wake ni mwaka 2014.

  Its high time tuanze kuhamia digital na sio kusubiri mpaka 2014. Tanzania tayari tunao multiplex oparators watatu, Star Media, Agape Associets na muungano wa Mengi na Dialo.

  Star Media wameshaanza, local channels za TBC-1, TBC-2, Clouds TV na Channel Ten wanaitumia kingamuzi cha Star Media.

  Agape Associets wao wanarusha ATN na channel kibao nzuri ikiwemo HBO.

  ITV na Star Tv nao wataingiza kingamuzi chao wakati wowote kuanzia sasa, hivyo kununua dish kubwa ili kuipata ITV na Star kwa kipindi kifupi might be wastage!.

  Cha kuwauliza hao ITV na Star TV ni lini wataanza kuitumia hiyo leseni yao ya multiplex oparator?.

  Kwa wasio fahamu kuhusu Multiplex Oparators. Kwanye kuhama toka matangazo ya analpjia kwenda digital, Transmiter moja inaweza kurusha mpaka chaneli 100 kama DSTV. Kwa mfumo wa analogia kila kituo cha TV kinarusha matangazo yake kwa transmiter zao kwenye digital hii haihitajiki tena. TCRA imetoa vibali kwa makampuni matatu ambayo ndio pekee watarusha matangazo ya TV. Makampuni haya ndio yanaitwa multiplex oparators.
   
 20. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #20
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Ni sawa kabisa ndugu yangu Pasco walivyofanya kwa kuchagua makampuni matatu maana wakiachia kampuni moja tuu itakuwa kama inavyofanya Tanesco.Ila kingine wanachotakiwa kukifanya inatakiwa chaneli zetu zote za hapa bongo zipatikane kwa kila kingamuzi cha kila kampuni ili chaneli zao binafsi ndizo ziwe zinamvutia mteja kuchagua kingamuzi kipi anunue ili ushindani uwepo mkubwa,na Watumie mfumo kama wa Dstv wa kutumia satelite ndio watawafikiwa wananchi walio wengi kwa nchi nzima na kwa muda mfupi saana tofauti na kutumia terestial ambayo inasumbua na kuwa na chengachenga.
   
Loading...