Wazazi na walezi kuna vyuo vya ufundi kwa watu wenye ulemavu, tuvitumie

Mzee Ngonyani

JF-Expert Member
Dec 16, 2022
821
1,876
Ndugu zangu Watanzania kwanza nianze kwa kutoa ufafanuzi kidogo juu ya VYUO hivi vya ufundi Kwa watu wenye ULEMAVU.

Hivi ni VYUO vilivyoanzishwa maalum kwaajili ya kuwasaidia walemavu kupata ujuzi na stadi za maisha Ili waweze kujitegemea na pia kujichanganya na jamii wanamo ishi.

VYUO hivi hutoa mafunzo ya ufundi stadi katika fani mbaimbali kama vile Uselemara, Uashi yaani ujenzi. Ubunifu na ushonaji wa nguo, Ufundi umeme wa majumbani, Uchomleaji vyuma, Utengnezaji wanguo za Batiki, Umpambaji n.k. Pia hutoa mafunzo ujasiriamali, stadi za maisha n.k.

Vyuo hivi vinapatikana katika mikoa ya Tanga (Tanga Mjini), Singida (Singida Mjini), Dar es salaam (Temeke) Mwanza(Milongo) Tabora na Mtwara (Masasi).

Licha ya uwepo wa vyuo hivi lakini bado WAZAZI wachache ndio wanaofahamu uwepo wa vyuo.

Pia ni muhimu kutambua kuwa bado vyuo hivi vina hitaji Watanzania kuvisaport Ili viweze kuwalea na kuwapatia elimu ya ufundi iliyo Bora vijana wetu na badae waweze kujitegemea kama walivyo watu ambao hawana ULEMAVU.

Nitoe pongezi nyingi Kwa WIZARA husika ambayo ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, hasa katibu mkuu na Mkurugenzi wa idara ya Waremavu Kwa KAZI nzuri wanaofanya.

Ukarabati unaoendelea kufanyika katika vyuo hivi umeonesha kuwa serikali inayoongozwa na Mama SAMIA inawajali watu wote pamoja na makundi ya watu walemavu.

Pamoja na pongezi hizo nina iomba serikali iwajali watumishi wanahusika kuwalea na kuwaangalia vijana wetu wenye ULEMAVU.

Sijasema kwamba serikali haiwajali, kipekee watumishi wa idara ya walemavu wanatakiwa kuangaliwa sana.

Hawa hawana tofauti na manesi hukesha na vijana, hushinda na vijana. Yatupasa tutambue kuwa vijana wanasoma katika vyuo hivi wana ULEMAVU wa aina tofauti na changamoto mbalimbali Kwahiyo wanaihitaji uangalizi wa karibu sana.

Pia wapatiwe vitendea kazi na mfunzo mbalimbaii mara kwa mara.

Pia niwaombe mashirika na taasisi mbalimbali kujitokeza na kusaidia ufadhili wa vijana wenye ULEMAVU waweze kuhudhuria katika vyuo hivi Ili
wapate elimu ya ufundi stadi na pia kwasaidia walimu wapate mafunzo ili waweze kuboresha huduma wanazotoa .

Ni wapongeze TEA ambao tayari wameanza kuonesha njia Kwa kuwasaidia vijana wenye ulemavu kupata mfunzo katika katika vyuo hivi.

Mwisho nawashauri WAZAZI na walezi kutowaacha majumbani vijana wetu wenye ULEMAVU, Bali tuwasaidie wapate ujuzi na stadi za maisha ambazo zitwasaidia kuijtegemea . Vyuo hivi ni vyetu tuvitumie na tuvisaport.

KAZI IENDELEE
 
Back
Top Bottom