Unachoongea MwanajamiiOne ni point.
Nyumba ndogo nyingi hazidumu kwenye uhusiano mmoja (kwa niliowahi kuwaona)
Kuna rafiki yangu wa utotoni mama yake alikuwa professional nyumba ndogo. Huyo mama amezaa watoto watatu, first born ndo rafiki yangu.
Hao watoto watatu kila mmoja ana baba yake na mababa wote ni majina makubwa.
Huyo mama alikuwa secretary lakini alijiendeleza sasa ni mwanasheria.
Mwanae alikuwa ana date kijana ambae tumekuwa nae; Ndugu za kijana walikuwa wanamchekea vizuri tu shemeji/wifi yao.
Huwezi amini siku kijana aliposema anataka kumuoa binti mama yake kijana na ndugu zake wakamwambia over our dead bodies.
Japo binti alikuwa ametulia sana na relationship moja ndugu za mwanaume walichukulia tabia ya mama yake kumdisqualify mtoto.
Binti alichanganyikiwa hakujua ni kwa nini wakwe wamegeuza kibao; ila the rest tulikuwa tunajua their reasoning.
Kwa sasa kuwa nyumba ndogo kunaweza kuwa sifa na a easy decision to make.
But in future inaweza kuwawekea nuksi watoto waliozaliwa kwenye hizo nyumba.
Kwenye jamii za kiafrika haikubaliki kwa mwanamke kuwa hana uhusiano na mwanaume mmoja. Tofauti na kuwa na baba mwenye kimada.
Nimekupata Darlingtone na hapa nachukulia kuwa unaamini kitakachokufanya usitulie ni 'shughuli' na naichukulia kuwa mapenzi hayachuji wala hamna kuwaka tamaa ya kujaribu vya nje kama inavyokuwa kwa wife. Kuwa huyo mume wa mtu anayekupenda na kukuustarehehsha wewe hatokaa achuje!! maana unavyoongelea hapa ni kama viile huyu huyu mwanaume ambaye kaona mkewe kachuja au for any reason katoka kuja kwako hatokaa atamani kwenda kwinginne na kwako akija anageuka anakuwa malaika....sweety forever? au ndo mnakwenda kimkataba!
Nisamehe mpenzi najaribu kukuelewa vizuri!