90
Ukifuata trick ya upande wa kushoto:
Ameanza na 4+4=20, ina maana hapa 4 imebeba thamani ya 10
Ikafuatia 5+5=30, hapa 5 imebeba thamani ya 15; Kutoka 10 hadi 15 kuna ongezeko la 5
Ikafuatia 6+6=42, hapa 6 ina thamani ya 21, ambayo ni sawa na 15 jumlisha 6
Kwa maana hiyo kwa kila hatua, inaongezeka thamani ya 1 zaidi ya lile ongezeko husika
Hivyo 7+7, ni sawa na (21+7) + (21+7), 28+28=56
Iliyorukwa 8+8 ni sawa na (28+8)+(28+8) yaani 36+36=72
SASA 9+9 ni sawa na (36+9)+(36+9), yaani 45+45=90
Kwa upande wa kulia (wa majibu)
Tunaanza na 20
Inafuata 30, yaani 20+10
Kisha inafuata 42, yaani 30+12
Kisha inafuata 56 yaani 42+14
Kisha itafuata 72 iliyorukwa yaani 56+16
Mwisho kabisa kwa kufuata trend ya 10, 12, 14, na 16...inayofuata itapata ongezeko la 18, hivyo itakuwa 72+18=90
Hizo ni njia mbili za kufikia jibu la 90, najua zipo nyingi ila mimi nimeonyesha hizo mbili tu.
Mwenye jibu tofauti atuelezee naye kalipataje.