JF vs FACEBOOK

fb stil iko juu ka ni kutngozana ata umu wapo weng 2... kule unawez kumpata ata m2 uliepotezana nae long tym af kuna detailz za ukwel co umu watu wanaogpa ktoa id zao za ukwel... al in al zote zko poa bt 4 da new genrtn fb iko pwh
 
Unajua kitu kinaweza kikawa kizuri ila watu wakakipasive vibaya, fb ni nzuri ila kiukweli jamii yetu ndo inaitumia vibaya hasa dada zetu ambao wanaitumia kama uwanja wa matangazo, kila dakika wanabadili photos.

Lakini lazima tukubali watu wana interest tofauti, hasa dada zetu wengi hawapo interested na kujadili mambo ya msingi kama siasa,na afya, ndomana si rahisi kujiunga JF kwani watu wengi wanazan JF ni mambo ya siasa tu, ila wakijulishwa kuwa ata mambo ya mapenzi yapo watakuja 2, ndomana ata kwenye makongamano ya katiba unawaona ni wachache sana wanauzulia.

Binafsi nipo FB lakini nilikua kila nikiweka mada zinazousu siasa hamna aliyekua ana comment, ila nikicheck kwa wale walibadili picha na walioweka mada za mapenzi kuna comments zakutosha, bt thanx kwa ndg yangu mmoja ambaye baada ya kunisikiliza nilipokuwa natoa comments zangu 2lipokuwa tunajadili kuhusu uchaguzi uliopita, akaniuliza kama uwa napitia JF, bt that was my 1st day kuisikia, baada ya kuifuatilia nikasikitika sana kuchelewa kujiunga JF.

WITO WANGU:
Bado kuna watu wengi sana makini kwenye jamii yetu ambao maoni yao tunayahitaji ila kujenga taifa letu lakini bado hawaifahamu vizuri JF, hivyo sisi tunaojua mazuri ya JF tuwajuze na kuwahamasisha kwani kwa pamoja tutaifikia Tanzania tunayoitaka.

ol ze best.
 
Jamani labda mi ndio mshamba kabisa. Nilijiunga na facebook tangu mwaka juzi, huko naona kumejaa ujingaujinga na usharabaro, kila mtu anakutaka. Hapa Jf sina muda mrefu lakini nina furaha na amani, napata changamoto mbalimbali, najifunza mambo mengi na yenye manufaa.

Wadada wenzangu wao wako busy na facebook, ukiwauliza wanaenjoy nini wanasema kuchat, ukiwaambia habari za JF wanasema we Ambilikile kweli (mshamba).

Sasa mshamba sijui ni mimi au wao ambao hawabenefit kitu. Jf is a place to be, thats why niko online kanzia asubuhi hadi usiku mzito.

I am the luckiest one kuwa miongoni mwa wana wa hii familia kubwa ya JAMII FORUMS

Facebook na Jamii forums ni vitu viwili tofauti, kimoja ni social network(facebook) na kingine ni forum(jamii) hivyo sioni kama kuna umuhimu wa wewe kutoka kule facebook labda kama na wewe hujui matumizi yake. Naomba kuwasilisha..
 
Facebook na Jamii forums ni vitu viwili tofauti, kimoja ni social network(facebook) na kingine ni forum(jamii) hivyo sioni kama kuna umuhimu wa wewe kutoka kule facebook labda kama na wewe hujui matumizi yake. Naomba kuwasilisha..
1.binafsi sioni kama kuna tofauti kati ya social network na jamii
2.unaweza ukawa unajua matumizi lakini lafiki zako wakawa hawajui matumizi(misuse)
hivyo kupoteza flavor kabisa, kwa maelezo ya dada ndo alichokua anamanisha
soma vizuri nazan utamuelewa, so kwa maelezo yake hasa tukizingatia kuwa watu tuna interest tofauti naona yupo sahihi kutoka.
 
Jf makes my day,nimewashawish ndugu zangu na staffmate wangu wajiunge,napata hbr fast,nilipata hbr za kifo cha prof kamuzora early than mwanae,mimi ndo nilimjuza,
zaid ya yote nikiwa alon inaniliwaza sana

Ndio nasikia sasa kuwa Prof. Kamuzora amekufa/fariki. Please naomba unijuze ni lini na alikufa kwa kitu gani, ugonjwa, ajali au.
 
JF ni kidume cha mbegu...ni cheche za fikra,ni ulingo wa hoja na uwanja wa kujenga watu kiakili....FB is jus chombo cha kupukutisha maadili (yasiyokuwepo) ya wanetu vipenzi! Hakuna ulinganisho katika haya!
 
face book ni nini mbele ya JF............. JF ni kila kitu...... raha zaid ni pale unapokuwa umevaa tshet yenye nembo ya JF halafu watu wanakukodolea mijicho wakitaka kujua ni nini hcho..... naipenda JF saaaaaaaaanaaaaaaaaaaaaaaaa
 
kwa kweli JF ni kisima cha mambo mengi ambayo kiukweli huwezi kuyapata FB
 
Mkipata nafasi tembeleeni wall ya Violet Mzindakaya ya FB siku mojamoja mwone waungwana wanavyomchana, mtasema ile wall ni JF Academia
 
Lets always make jf the thinking tank of this nation

Lets love sense, reason and meaning of the issues

Lets be honourable, noble and show the Tanzanian diginity

lets find what unity all of us togather as Tanzanians ...lets be it... let the forum work for it!!

AND

Iam serously taking this favorable opportunity to welcome Mr president JK and all of the member of cabinet !! Be here, feel at home ... xpress and discuss with open mind ..educate and make all clear!!

Let jf be jf and Fb be what it is!!
 
Kulinganisha JF na Facebook ni sawa na kufananisha mlima Kilimanjaro na kichuguu.Huko facebook hakuna la zaidi ila ni kuambiana tu mmependeza jamani,lakini ukija humu sidhani kama kuna kitu utakosa katika nyanja zote za maisha na hata ukitaka Breaking News hapa ndio penyewe,Mfano mimi nipo nje ya nchi lakini mabomu ya Gongo la Mboto yalipolipuka taarifa ya kwanza niliipata kwa sms toka kwa JF member nikakimbilia kwenye Pc yangu lakini katika mitandao yote ni JF pekee iliyotoa live coverage wengine wote walitoa report kesho yake,na huo ni mfano tu sasa utalinganisha JF na hiyo takataka?
 
Back
Top Bottom