Tunapendekeza kuwa labda uje na kuandika kitabu cha current Tanzania social problems za katika politics zetu na jinsi gani ya kuboresha mifumo yetu ya uongozi
Josh Michael,
Nimelifikiria jambo hilo kwa muda mrefu. Na bado liko mawazoni mwangu ingawa sijawahi kuandika kitabu hata kimoja. Pia tuwahimize ndugu zetu wengine Watanzania kuandika vitabu kuhusu siasa na matatizo ya nchi yetu.
Na nikiendelea kulifwatilia jambo hilo, ningependekeza kwa moderators kwamba labda mada hii ihamishwe na ipelekwe kwenye jukwaa la siasa kwa sababu ingawa ilianzishwa kuhusu Godfrey Mwakikagile kama mwandishi wa vitabu, tumejadili mambo mengi yanayohusu taifa letu kuliko yale yanayomhusu Mwakikagile binafsi.
Hata swali ulilouliza mwanzoni ulipoanzisha mada hii lilihusu vitabu vyake ambavyo vinahusu siasa na matatizo ya nchi yetu, na bara letu, na siyo maisha yake binafsi. Kwahiyo natumaini kwamba hata wewe, uliyeanzisha mada hii, utasaidia kufanya hivyo na kuwasiliana na moderators ili mada hii ihamishwe na iwekwe kwenye jukwaa la siasa.
Kwa sababu Godfrey Mwakikagile anaishi nje ya nchi yetu kama Watanzania wengi wengine, ambao jumla yao labda ni milioni mbili sasa, tukaanza kuzungumzia tatizo au suala la "brain drain." Pia tumejadili hapa, katika mada hii, maswala mengine yanayolihusu taifa letu ambayo yeye pia ameyajadili katika vitabu vyake; kwa mfano haja ya katiba mpya, matatizo ya muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar; vyama vya upinzani na udhaifu wao na kwa nini ni lazima viungane na kuunda chama kimoja ikiwa viongozi wa vyama hivyo wanataka kusaidia kuleta mabadiliko nchini; pia tumezungumzia ufisadi, ukabila, ubaguzi wa rangi, serikali na sera zake, mazingira ya kisiasa na uchumi nchini, na mambo mengine. Mwakikagile pia ameandika kuhusu hayo yote katika vitabu vyake. Lakini siyo matatizo yake binafsi. Ni yetu sote. Ndiyo maana nimesema mada hii ihamishwe na ipelekwe kwenye jukwaa la siasa.
Mada hii inastahili kuwa kwenye jukwaa la siasa kwa sababu nyingine badala ya kuwa hapa kwenye celebrities forum.
Godfrey Mwakikagile siyo celebrity nchini Tanzania au kama wasanii wetu walio hapa nchini au kama viongozi wetu wa taifa. Hata yeye hajioni kama ni mtu maarufu, kama alivyosema katika maandishi yake na katika majibu yake alipohojiwa kuhusu vitabu vyake (angalia profile yake katika online encyclopaedia Wikipedia kuhusu interview hiyo). Pia nakumbuka katika kitabu chake, "Nyerere and Africa: End of an Era," amesema he's just a simple African and wants to live a simple and quiet life as he always has.
Kwahiyo sidhani ni celebrity. Na hajioni kama ni celebrity ingawa labda kuna watu wanaomwona hivyo. Lakini hata kama kuna watu kama hao, ukweli ni kwamba ni watu wachache tu nchini Tanzania wanaomfahamu au waliomsikia Godfrey Mwakikagile kuwa ni mwandishi wa vitabu. Anajulikana au anafahamika kwa wanafunzi na ma professor na watu wengine katika nchi za nje kuliko hapa Tanzania. Mwandishi wa vitabu ambaye ni celebrity hapa nchini Tanzania ni Shaaban Robert. Kuna wengine, lakini Godfrey Mwakikagile siyo mmoja wao. Kwa mfano, jiulize swali hili: Anafahamika nchini Tanzania kama Faraji Katalambula au waandishi wengine wa Kitanzania?
Ni kweli ameandika vitabu, na ameandika vitabu vingi sana labda kuliko Watanzania wengine ambao pia wameandika vitabu.
Not only has Godfrey Mwakikagile written more books than any other Tanzanian; he also has more books in public and university libraries around the world than any other Tanzanian - and more than many professors, if not more than most professors, in the world have. Not all professors who write books have all their books accepted by university and public libraries the way Godfrey Mwakikagile's books have been accepted around the world. Every book Godfrey Mwakikagile has written is found in university libraries around the world. And not all professors have written as many books as Godfrey Mwakikagile has. So, in that sense, yes, he's a celebrity, of sorts, especially to some of those who have been able to find out what he has achieved as a writer of scholarly books and other titles of general interest to members of the general public.
Lakini siyo celebrity hapa nchini Tanzania kama Chinua Achebe au Wole Soyinka walivyo nchini kwao kule Nigeria na nchi za nje, au hata kama jirani yetu Ngugi wa Thiong'o alivyo nchini kwake Kenya na katika nchi zingine katika bara letu na nje ya bara hili.
Ni kwa sababu hizo ninapendekeza mada hii ihamishwe na labda iendelee kujadiliwa kwenye jukwaa la siasa. Na simaanishi tuendelee kumjadili Godfrey Mwakikagile bali maswala aliyoyajadili katika vitabu vyake na ambayo sisi pia tumeyajadili katika mada hii na ambayo yanalihusu taifa letu na matatizo yake ya siasa, uongozi, maendeleo na mambo mengine.
Pia napenda kuwajulisha wana Jamii Forum kwamba kuna update nyingine katika article ya Wikipedia online encyclopaedia iliyoandikwa kuhusu Godfrey Mwakikagile ambamo Professor Ali Mazrui amesema mengine kuhusu Mwalimu Nyerere. Pia katika Bibliography ya article hiyo, kuna vitabu vingine, nadhani viwili au vitatu, ambavyo Mwakikagile ameandika na ambavyo vimechapishwa mwaka huu wa 2009. Kutokana na Bibliography hiyo, vitabu vyake vya mwisho, kabla ya hivi vipya, vilishapishwa 2008.
Last edited: