Ikiwezekana naomba muweke threads maalumu kwa watu ambao ni public figures ambapo zitakuwa hazina option ya reply. Hii ni pamoja na wabunge, viongozi wakuu wa vyama na serikali ambao wamejisajili au watajisajili humu.
Kama mtu akijisajili kwa jina la kiongozi, then muwasiliane naye on private kwanza ili ku-confirm ni yeye kiongozi au ni majina kufanana.
Natoa pendekezo hili kwa sababu baadhi ya viongozi wanapotoa kauli, unakuta zinachangiwa na mamia ya wanaJF, kiasi kwamba ili mtu uweze kuipata hiyo stori, ni lazima uwe na mda wa kutosha (sometimes haupo), wa kusoma posts zote kwenye hiyo thread.
Hata hivyo ikiwa wanapewa special place ya kutoa taarifa zao, bado wapewe option ya jutuma na kushiriki hizi threads za kawaida.
Thanks.