JF M & F Ambassador Of The Year 2011 Competition

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Angalizo: Mods kwa hekima mnaombwa msiiamishe thread hii wala kuichanganya na nyingine yoyote.

Wanajamii; Wana JF

Mwaka 2010 tulifanya mchakato wa kumpata JF Man & Woman of The Year 2010. Shindano kama hili pia lilifanyika Mwaka 2009.


  • Washindi wa 2009 "JF SuperLady" au "Celebrity wa JF" alikuwa WoS (Woman of Substance)
  • Washindi wa 2010 "Regia Mtema" (RIP) - Kwa JF Woman of the Year 2010
  • na Nyani Ngabu kama "JF Man of The Year 2010"

Mchakato wote mpaka mshindi kupatikana unaweza kuupitia hapa:
https://www.jamiiforums.com/complaint...ar-2010-a.html

Mwaka huu tunataka kuuboresha mchakato huu na tunapenda kupitia mchakato huu kupata washiriki wengi na kuipa taswira JF kuwa kuna watu wanafakubalika katika hii online community.

Mwaka huu 2012 tunafanya mchakato wa kuwapata Washindi wa 2011 (lakini michango yao ya sasa inakubalika iingizwe 2011).Tulichelewa kufanya kwa sababu zilizo nje ya uwezo. Mwaka huu tumeongeza na tutakuwa na Category ya:


  • JF MALE AMBASSADOR OF THE YEAR 2011 na
  • JF FEMALE AMBASSADOR OF THE YEAR 2011

Mchakato wa kuwapata washindi ndiyo unaanza sasa.Katika mchakato wa awali tutapendekeza majina mbalimbali katika category hii kulingana na unavyoona mhusika anakubalika na mwishoni tutachagua watatu kutoka katika kila category na kisha kuwapambanisha kupitia JF POLLS. Mwaka huu napendekeza tutoe zawadi yenye hadhi fulani kwa washindi ili kutoa changamoto za umakini katika mabandiko haba jamvini. Tutajulishana zawadi hizi tutakapoingia katika mchakato wa Kupiga kura.

Vigezo vifuatavyo vizingatiwe katika kutoa mapendekezo ya watakaoshindanishwa katika hizi KURA ZA MAONI:

1. Kama ni category ya FEMALE lazima uwe umemdhania kuwa unayempendekeza ni Mwanamke na una ushahidi wa Kimazingira. katika hali ya mashaka, uhakikisho wa jinsia kutoka kwa muhusika aliyependekezwa utafanya akubalike. Uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi - JEC (Superman) ya Shindano hili utakuwa ni Final. wote mnahakikishiwa hakutakuwa na Uchakachuaji.

2. Kama ni category ya MALE lazima uwe umemdhania kuwa unayempendekeza ni Mwanaume na una ushahidi wa Kimazingira. katika hali ya mashaka, uhakikisho wa jinsia kutoka kwa muhusika aliyependekezwa utafanya akubalike.

Katika 1 na 2: Uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya JF (JEC) wa Shindano hili utakuwa ni Final. wote mnahakikishiwa hakutakuwa na Uchakachuaji.

3. Anayependekezwa lazima kuwe na ushahidi unaoonyesha kuwa ni Mwana JF aliyebobea hasa kutokana na Threads alizozianzisha na pia post anazobandika. Vyote lazima viwe na impact chanya kwa wasomaji wa JF.

4. Awe ni mwenye uwezo wa kusimamia hoja zake na kuzijibu kikamilifu bila jazba na kwa umahiri wa hali ya juu pale ambapo anapata challenge toka kwa wachangiaji.

5. Awe ni mwenye ushawishi wa hali ya juu katika mabandiko anyochangia walau kwa muonekano wa wachangiaji kuunga mkono hoja zake.

6. Kwa Wanaogombea Overall tittle, asibobee kwenye Jukwaa moja tu. Walau awe mchangiaji mzuri wa majukwaa yasiyopungua mawili. Kwa wale wanaopendekezwa MMU basi akubalike katika jumuiya ya MMU

7. Asiwe mtu wa shari katika majibizano kiasi cha kupelekea Mods kumpa "BAN".

8. Aonekane wazi katika mabandiko yake anaweza akahisiwa kuwa Kiongozi Mzuri.

9. Awe Mchangiaji ambaye ni active walau mara moja kwa wiki. Ikiwa zaidi ni vizuri zaidi.

10. Awe ni mtu asiyeogopa kukemea mabandiko yenye lengo la kutukana, kudhalilisha, kubagua, kuleta mfarakano na kutokuelewana baina ya wanachama wa JF.

Sasa kila moja yuko huru kutoa mapendekezo yake ya nani wanastahili kuingia katika tatu bora katika kila category.

Angalizo: Washindi wa Miaka ya Nyuma ni Macelebrity tayari hivyo hawaruhusiwi kupendekezwa.

Nashauri kuwa mapendekezo ya majina yaambatane na maelezo mafupi.

Uwanja ni wenu. Karibuni sasa mto mapendekezo au NOMINATIONS.

Zingatia: ID za kuchakachua haziruhusiwi: i.e ID ambazo ni mpya kabisa na zimetengenezwa kwa ajili ya kupiga debe na kuongeza kura tu na ID zilizokuwa hazitumiki muda mrefu na sasa zimeibuka ghafla:

Unapofanya nomination yako andika kabisa, Unamnominate nani na kwa title gani:

Mfano: "Superman awe Male Ambassador of The Year 2011" NB: Pls msimchague Superman huu ni mfano tu.


Wasalaam
Superman-Logo.jpg

Signed & Sealed:

Superman

Mwenyekiti - Tume Ya Uchaguzi ya JF (JEC)


images
 
Nampendekeza pakajimi.
Huyu member ni mkongwe sana jamvini anasimamia hoja zake na anawakilisha.
 
Back
Top Bottom