JF Ladies and Gents,niko sawa au?

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,702
Sikumbuki hasa kilichotufikisha kwenye mjadala wa kujadili kuhusu mwanandoa mmoja kufariki,lakini ambacho nakijua ni kuwa kuna mgogoro mkubwa kwenye tulichokua tunakijadili.Mjadala wenyewe ni kuwa,je mume anapofariki na kuacha watoto na mjane,mali alizoacha nani anatakiwa kuzisimamia?Pia kama mjane atakuwa anahitaji kuliwazwa je akipata mtu ahame nyumbani na akakae sehemu tofauti au palepale?Vijana wote isipokuwa mimi tu walidai kuwa,mali anatakiwa asimamie ndugu wa mume na kama atahitaji mume ahame pale nyumbani,walizungumza mengi na kudai mali ni za mume na mke haruhusiwi kuzisimamia!!Nilishangaa sana!MSIMAMO WANGU ulikuwa hivi;mke ana haki sawa na mume kwenye suala la kutolea maamuzi,mume ni kiongozi mkuu,maadam hayupo mke ndie mwenye last say!Ni aibu kubwa mwanaume mzima kwenda kuleta usumbufu kwenye mali za mwanaume mwingine,atafute zake!Pia mke anaweza kutumia mali atakavyo bila kuulizwa na YOYOTE,hata akitaka kuolewa hatakiwi kuulizwa chohote ni sawa na mume angeoa na kuishi pale na mke mpya!!Je nyie wana JF mwasemaje?
 
Kwa mtazamo wangu Mali anasimamia mke.... Ila kwa kweli sioni kama ni heshima kua mtu ulikua na mumeo... Ulete mwanaume mwingine humo ndani. Naamini kama huyo mwanaume anakuheshimu hatathubutu kuja mlale woote humo ndani. Atajitahidi kwa kila namna muwe mnakutana huko nje. Hasa kama una watotot.... Wakiwa wakubwa haipendezi sababu wanajua mnafanya nini huko ndani, tofauti kama ni baba yao wamekua with the knowledge you share a room. Wakiwa wadogo ndio sumu kabisa... Inakua kama wawachanganya.... Sidhani kama huyo mwanaume unakua mmepanga kuoana... Mkiachana tena mwingine ulete humo ndani. Ki maadili kwa watoto sio nzuri na pia yakupunguzia heshima kwa huyo mwanaume, watoto, wanafamilia na Jamii nzima.
 
ngoja waje wanasheria

ila mama ana a certain %
na watoto wana % fulani
ila nyumba ya watoto, kama mama anaolewa inabidi aondoke hapo.
 
Mke ana pewa % na mama wa mme anapewa % na watoto wanapewa %.

Kutokana na dini y aki islam mtoto wa kiume anapewa zaidi ya mtoto wa kike.

Na mke wa marehemu akiamua kuolewa na mwanaume mwingine basi kwanza angojea amalize eda afu akiolewa hana kitu hapo...nyumba wanachukua ndugu za mme mpaa watoto wakuwe wa wakabaidhi..kama hajaolewa akae hapo hapo na wanae.

Wa Alahu alamu...inawezekana nimekosea sehemu lakini ndo navyo jua.
 
@fazaa
naona wee umepatia
jirani yako wakili nini??

Maana siku hizi watz
ukikaa jirani na daktari wa watu, wewe unatohoa unezi
kama jirani yako wakili, wewe unakuwa na diploma ya sheria.
 
Jamani!Nisichoelewa hapa ni kuwa,ni kwanini iwe sio heshima mwanamke kuolewa na wakakaa nyumba ileile?Tofauti ni nini?Aibu ni ipi?Plz help me to understand this!Sijajua hapa inakua nini ni nini!Nielewesheni hapa!
 
ishu ni complicated aisee

je ndoa ya miaka mingapi?
je mali za mume sio za familia ya wazazi wake?
mke ni housewife au mfanyakazi?

mume ana wazazi wanaomtegemea?
ana watoto wengine wa nje au ndoa nyingine kabla?

mke na mume walielewana hadi mwisho?

maswali mia kidogo hapo...
 
Jamani!Nisichoelewa hapa ni kuwa,ni kwanini iwe sio heshima mwanamke kuolewa na wakakaa nyumba ileile?Tofauti ni nini?Aibu ni ipi?Plz help me to understand this!Sijajua hapa inakua nini ni nini!Nielewesheni hapa!
 
ninachoelewa mke anasimamia mali zote kama watoto bado wadogo kama ni wakubwa kila mtu anapewa share yake pesa ya mirathi kisheria inagawanywa kwa mke,wazazi wa marehemu kama wako hai,watoto na inaingizwa direct kwenye akaunti ya kila mmoja kama hauna akaunti unafungua.mtoto mdogo kuliko wote ndo anapata gawio kubwa kuliko wote
 
yeah.. Ni la kisheria zaidi...

Ila nadhani kama ukiacha wasia,mara nyingi ndiyo guideline kuu..na utata mdogomdogo kama huo hupungua...
 
Unless kuna will ambayo inaonyesha mali zigawanywe vipi lakini kama hakuna kisheria mke ana haki kuwa msimamizi wa mali za mumewe na kama watoto ni wakubwa basi watajadili kama familia na maamuzi watakayofikia kati ya watoto na mama (huku kukiwepo pia wawakilishi kutoka upande wa mume maana kwani wanaweza kuzuia usimamizi huo wa mali kwenda kwa mama/watoto). hao ndugu wa mume wanaweza kuleta hoja kuwa labda mmoja wao aliahidiwa shamba etc ambapo itabidi alete ushahidi kuwa kweli alihadiwa na mama/watoto wakikubali kumpatia shamba kama ambavyo aliahidiwa mambo yanasonga. In short wanapaswa kuhusika pale mwanzoni wakati vikao vya familia vikiendelea kabla ya kwenda mbele zaidi kisheria ili kuondoa doubts zozote na mambo kama hayo. wasipohusishwa mwanzoni ndo kasheshe na wanaweza pinga.

Si heshima kuleta mtu mwingine ndani. bora mama ahamie kwa huyo rafiki mpya au watafute nyumba nyingine.
 
Mnazidi kuleta maswali zaidi,mume amefariki,mnasema mali asimamie mke lakini mnadai atafanya hivyo kama watoto ni wadogo,why??Mbona usimamizi wa mali wakati baba yupo gautegemei kama watoto ni wakubwa ama la?Halafu eti kama ameacha wosia ndo utakua mwongozo kwanini?Kwanza ni kwanini wosia atoe baba?Kwanini wosia usiachwe na mzazi atakaebaki kwa sababu wote ni sawa?Wanawake vipi nyie?Mtapewaje haki sawa kama mnakubali kuonwa hivi?
 
Jamani!Nisichoelewa hapa ni kuwa,ni kwanini iwe sio heshima mwanamke kuolewa na wakakaa nyumba ileile?Tofauti ni nini?Aibu ni ipi?Plz help me to understand this!Sijajua hapa inakua nini ni nini!Nielewesheni hapa!

eiyer!ukitaka kuelewa mambo ya mapenzi geuza scenario!sasa hapo geuza fanya kinyume chake upate hisia zake!mfano!nyie mmemsomesha kwa shida zote mdogo wenu wa kike!akaja akapata kazi akawa na mali za kutosha!akaolewa na kapuku flani!kapuku akapanda chati ya maisha,kidogo mdogo wenu kafa!kapuku kaoa mwanamke mwingine anatumia mali alizochuma mdogo wenu!now feel it!
 
Hapo kwa upande wangu mimi nahisi Mke ndio last say. Kwa akina Baba, je Mke akifa utakuwa radhi Mwanamme/Shemeji yako aje asimamie mali ulizochuma na Mke?
 
Mc Tilly,mali za mdogo wangu hazinihusu labda niambiwe na muhusika vinginevyo!Fahamu pia kumsomesha ndugu,mtu yoyote ni haki yake ya msingi siwezi kuhusisha kumsomesha mtu na mali alizopata huo ni ujinga!
 
Mi nikiRIP afu mke wangu alete njemba lilale kitandani mwangu..... wallah nawaibukia toka kaburini.

1.Mi nikiRIP.... Mke wangu atarithi kuwa kiongozi wa kusimamia mali zangu endapo tu hataolewa tena.
2.Akiolewa na aende zake kwa amani, atakuwa na gawio la mali zangu ambazo sasa zitasimamiwa na ndugu zangu.

Ila MALI ZOTE hizo ni MALI halali ya wanangu bila kujali 1 na 2 hapo juu. Watoto wakishakuwa wakubwa wataamua namna ya kumshirikisha mama yao.

Mkimwona Bibi mumwambie nimesema hivyo eti. Na ole wake akiuke.
 
Jamani!Nisichoelewa hapa ni kuwa,ni kwanini iwe sio heshima mwanamke kuolewa na wakakaa nyumba ileile?Tofauti ni nini?Aibu ni ipi?Plz help me to understand this!Sijajua hapa inakua nini ni nini!Nielewesheni hapa!
Jibu kishakujibu shemeji yangu hapo chini.

Kwa mtazamo wangu Mali anasimamia mke.... Ila kwa kweli sioni kama ni heshima kua mtu ulikua na mumeo... Ulete mwanaume mwingine humo ndani. Naamini kama huyo mwanaume anakuheshimu hatathubutu kuja mlale woote humo ndani. Atajitahidi kwa kila namna muwe mnakutana huko nje. Hasa kama una watotot.... Wakiwa wakubwa haipendezi sababu wanajua mnafanya nini huko ndani, tofauti kama ni baba yao wamekua with the knowledge you share a room. Wakiwa wadogo ndio sumu kabisa... Inakua kama wawachanganya.... Sidhani kama huyo mwanaume unakua mmepanga kuoana... Mkiachana tena mwingine ulete humo ndani. Ki maadili kwa watoto sio nzuri na pia yakupunguzia heshima kwa huyo mwanaume, watoto, wanafamilia na Jamii nzima.
 
Hii kitu inahitaji jicho la tatu kwa kweli.....as TB said maswali ni mengi sana

1. Kama ingewezekana 1st house iwe ya familia from there on kila mtu na achunge mzigo wake...will iwe ni lazima kisheria ili ukifa watu waangalie matakwa ya mwenye mali period

2. Kwa mtu anapofariki eti sehemu ya mali wapate wazazi....ilhali ameacha watoto may be wanasoma n ol that ???????

3. Suala la kuingiza partner si kwa wanawake tu hata kwa wanaume si ustaarabu asilani.....most of the times mke ndo yupo busy na mashuka na arrangement ya chumba kwa ujumla......leo afe...on the same bed and sheets you hop with another woman?????
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom