JF-get together party Disemba 2018

Habari wana Jf kwa ujumla, nadhani mko salama na mnaendelea vizuri na majukumu yenu.
Kama ilivyokawaida ya wanajumuiya iishiyo pamoja kunakuwa na mambo ya kukutana, kufahamiana na kufanya ki-tafrija kidogo.
Hivyo basi kama ilivyo kawaida ya wana Jf, tumeamua kukutana, kupiga story mbili tatu, kula, kunywa na kucheza pamoja kama wadau walivyotaka. Maana wameona kimya na party hakuna tena kama ilivyo desturi ya hapa Jf.

Hivyo basi, kutakuwa na JAMII FORUMS GET TOGETHER PARTY hapo mwezi wa kumi na mbili (December).
Na vile vile tumependekeza mambo yafuatayo katika kuelekea siku hiyo ya party yetu.
Mambo yenyewe ni kama ifuatavyo:

1. Eneo la kukutania kwa ajili ya party ni pale AFRICAN HOUSE LOUNGE iliyopo pale block 41 Kinondoni karibu na Best Bite Namanga.
Hapa tutachagua kama tutakaa sehemu ya garden au ndani ya kiukumbi amazing.

2. Mchango ambao tumependekeza ni Tsh 30,000/= ambao utajumuisha vinywaji, ukumbi, chakula na picha 1 kwenye red carpet.

3. Michango kwa ajili ya party hiyo itumwe kwenye namba zifuatazo;
Tigo-pesa.
0716-394882 jina May
NA
M-Pesa

0756-986874 jina Mwanahawa Hassan
Ukishatuma mchango wako, njoo pm kwa Mzigua90 au kwa Madame B ukiwa na screenshot ya message ya pesa uliyotuma ili upate namba ya uthibitisho wa kuingilia ukumbini siku hiyo.

●Pili, Pia unaweza kututext kwa message ya kawaida kwenda kwenye namba hizo hapo juu ili uweze kutuambia jina lako ulilotuma pesa na ID yako unayotumia.

●Tatu, pia unaweza kutumia njia ya tatu ya kutuma pesa kwa ambao hawatapenda wajulikane ID zao.
Fanya hivi:
Tuma pesa kwa namba hizo hapo juu, ukishamaliza kutuma, njoo kwa text ya kawaida useme kuwa umetuma pesa na limetokea jina flani halisi au la wakala uliyetumia kutuma pesa na wala haina haja ya kutaja ID
Tukihakikisha ni kweli unawekwa kwa list.
Maana si wote watapenda tufahamu ID zao halisi hapa Jf.


4. Dress code ya siku hiyo ni:
WANAUME/WANAWAKE
●Tshirt/shati nyeupe au nyeusi.
●Jeans suruali ya bluu/nyeusi
●Jeans kaptura ya bluu/nyeusi

Pia kwa wadada wasioweza kuvaa suruali au kaptura wavae black dress (dress to impress)

Tupendeze jamani....
Party ya kwetu hii....

5. Tarehe ya party ni tarehe 15/12/2018 siku ya Jumamosi kuanzia saa kumi kamili jioni mpaka usiku sana.

6. Unaweza kuanza kutuma mchango wako kuanzia sasa hivi.
Na mwisho wa kupokea mchango wako ni tarehe 08/12/2018 saa kumi na mbili jioni.

7. Majina ya waliochangia party yatawekwa hapa jukwaani katika updates zetu.
Kwa ambao hamtapenda kuwekwa majina yenu hadharani,hatutayaweka.

Natumaini wote tutakuwa tumeelewana kuhusu ujio wa hii party yetu ya JF.
Tunaomba tuhudhurie kwa wingi ili tuweze kufahamiana na kupiga story mbili tatu.

NB:
Ukumbi unachukua watu 50 tu.
Hivo kuwahi kwako kutoa... ndipo urahisi wako wa kupata nafasi ya kuhudhuria party hii kabambeeeee!!!!

KARIBUNI.....KARIBUNI!!!!View attachment 866458View attachment 866453View attachment 866454
View attachment 867245View attachment 867247
View attachment 867246

UPDATES YA WALIOTOA:
Mzigua90
Madame B
RRONDO
Wakala
Wakala
UPDATES:
●Kutakuwa na
RED CARPET matata sana toka kwa wadhamini wa Party yetu ambao ni JAMII FORUMS MEDIA

●Pia kutakuwa na picha mnato kutoka kwa wadhamini na waandaaji.
Na vingine vingi vinakuja....

SI YA KUKOSA KABISA
Ha ha ha ha ha mm hata ukinilipa na posho siji kabisa
 
Akirudi lazima umpe tena kitumbua. Ukikaa vibaya unashangaa kashakukonki
😂😂ila jina halijawah nitoka..alinitafuta sana miaka ya 80 mwanzoni nikawa nashindwa coz nilikua bado chini ya homaya ya wazaz... siku nitamfata fb😁😁 .. kanitoa miaka ya 72 hv
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom