Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 65
4.3 Local Government rates and taxes shall not be:
4.3.1 in excess of those generally applicable on Tanzania, or
4.3.2 based on profit, turnover, sales or output from mining operations, or
4.3.3 based on the value of land used for the mine, mining infrastructure or installations,
provided that the aggregate of such local Government rates and taxes charged shall not exceed United States Dollars Two Hundred Thousand (US$ 200,000) in any one calendar year.
Katika mkataba mzima so far hakuna mahalai nimezimia kama kwenye hiki kifungu, hebu check this out, hebu naomba wakuu mksome tena hiki kipande halafu mtoe maana zake maana ziko nyingi sana za kutufanya wananchi na serikali yetu kuwa ni majuha!
Dah!
Kwa Mujibu wa maelezo ya kichuguu kwamba Mkataba huo tunaouona Hauna seal ya serikali. hivi serikali wakija na hoja kwamba huo mkataba tuliouona ni feki, ni uzushi wa wapinzani,na kwamba yeyote anayetaka kuona mkataba halali afuate taratibu zilizowekwa ataupata.
Hivi hii si inaweza kubadirisha upepo wa siasa kwa sasa?
Nadhani ni uvivu wa kusoma na kufuatilia mambo ya nchi kwa undani na kwa uzalendo, kulisema taifa lako kwa mabaya sio jambo la kusheherekea, mbona Busha anaboronga vita ya Iraq lakini wananchi wake wako naye karibu;
Kwa mawazo yangu mimi nisiyesoma sheria kujadili taarifa ambayo taifa letu limesaini kwamba itakuwa ya siri sio jambo la kujivunia sana, ingawa sisemi kilichomo ndani ni kizuri ama la kwa kuwa sio mtaalamu wa madini wala wa sheria.
Kwa majibu ya swali lako yako hapa http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/16-2004.pdf
Nenda moja kwa moja PART IV: Section 16; Title "Establishment of the National Economic Epowerment Fund
Tujaribu kuwa wazalendo kwa kutendea taifa letu haki kwa kusema mambo kwa research zaidi, kumbuka munayoandika hapa yatakaa kwenye computer za watu wengi wa maitaifa mengi, miaka na miaka... let no think you are chating with kilitime and it will end there!
Hili jambo nalifananisha na kukata tawi ulilokalia!!! Sisi ni Watanzania na Tutaendea kuwa watanzania aidha chini ya waziri X, au Waziri Y, au Waziri Z, au etc... so let be fair to our nation,
Kilitime,
Kama jina lako, inaonyesha ni kweli wewe una "kill time" tu hapa.
Bush gani unayemzungumzia?? kama ni Dubya basi mwenzio ni "lame duck president" na hiyo is NOT a good thing.
Kila nchi iliyoendelea wananchi wanaichachafya serikali yao hadharani!! mie sioni ubaya wa hatari kwa taifa,kwa hawa mafedhuli kukomwa nyani giladi...........muheshimiwa sana kama huna la maana la kuchangia,kama si mtaalamu wa sheria na masuala ya madini na kama pia mvivu wa kusoma maelezo marefu basi usije hapa na agenda zako za uzalendo fake....uzalendo wa kizamani, uzalendo wa zidumu fikra sahihi wakati unajua si sahihi. Kuwa cheerleader kwenye sidelines pia ina ruhusiwa, ngoja nikutafutie pongpong na kibwaya ili uweze kuwa hamasisha wakina mwanamke mwafrika na wengine wakituchambulia majambozi hapa!!!!!!!!.
Matusi nimepokea kwa mikono yote, lakini soma content ya url niliyoweka! Wakati huo ukumbuke kwamba kuna part ambayo haitendewi haki, serikali yenu chachafyeni kadri mnavyotaka lakini part ya pili ya huo mkataba hamuwapi haki yao!
Matusi nimepokea kwa mikono yote, lakini soma content ya url niliyoweka! Wakati huo ukumbuke kwamba kuna part ambayo haitendewi haki, serikali yenu chachafyeni kadri mnavyotaka lakini part ya pili ya huo mkataba hamuwapi haki yao!
wakati huo tujue hatumtendei haki mwekezaji ambaye hana hatia yoyote...
Hayo ndio maoni yangu tu... mimi ninaye kili time
Dada Mwafrika wa Kike na Alles,
Sina matatizo na kukosoa serikali, na sina matatizo na wanaosema mimi kweli na kili time nadhani wana maana mimi naponda muda tu,,, pia hiyo kwangu sawa.
Wasiwasi wangu ni kwamba Serikali yetu kuu, kwa niaba ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeingia mkataba mzuri/mbaya sijui, kwa sababu terms za negotiation sizijui, lakini imeingia mkataba na Mwekezaji tena sio mwekezaji wa mfukoni hapani ni kampuni linalotambulika ulimwenguni...
Sasa sijui lakini generally mikataba hii wakisaini ni ya siri, sio kwamba serikali tu ndiyo yakupenda mikataba iwe siri lakini mwekezaji yeyote ikiwa pamoja na wale waliokuwa wanasupply mchicha kwenye mashule ya sekondari na magereza enzi zile... sasa leo hii mkataba unawekwa hadharani ati kwamba tunaikosoa serikali... wakati huo tujue hatumtendei haki mwekezaji ambaye hana hati yoyote...
Hayo ndio maoni yangu tu... mimi ninaye kili time
4.1.3 for each year of production the amount of US$ 125,000
by 31st December of each calendar year a contribution
to the Empowerement Fund
waoooo hii statement imenimaliza kabisaaaaa...
Nimeweka parts zote za article 4 maana ndiyo article inayohusu pesa na ndiyo inaonyesha Tanzania itapata nini toka kwa huu mkataba...
Articles zingine zitaendelea tena baadaye au kesho...
Thanks
Sasa sijui kesho ipi. Kwangu ndio kunakaribia kucha na ndio nimeamka.
Ni kwanini mchango wa kampuni hiyo katika uwezeshaji uwe ni Dola 125,000? Kama mkataba huu ndio umeboreshwa zaidi basi sina shaka kuwa michango ya makampuni mengine kwenye mfuko huo yatakuwa chini ya hapo.
Pili, Endapo kampuni ya madini inatengeneza faida (net profit) ya Dola milioni 20 kwa mwaka, dola 125,000 kutoka kwenye faida hiyo ni sawa na asilimia 0.0625 ya faida. Je hilo ni sawa? Kama kweli tutaweka kipengele kama hicho kwa miaka yote ijayo ya maisha mgodi huo hivi ni kweli mfuko wetu utafaidika?
Tatu, mwaka wa uzalishaji unaanza lini? Bila ya shaka ni baada ya faida kuonekana au kufikia kiwango fulani cha uzalishaji. Ina maana kwamba kama watazalisha bila kufikia kiwango cha uzalishaji kinachodefine "production year" ina maana wanaweza kujikuta wanachangia mara moja tu au mara mbili tu kabla maisha ya mgodi kuisha.
Kwanini serikali isianzishe mfuko wa tofauti kabisa ambao utachangiwa na sekta za madini na utalii na wenye lengo la kuendeleza makazi, miundo mbinu, na nguvu kazi.? na ukiongozwa na sheria tofauti kabisa?
Ningekuwa mwekezaji ambaye nataraji kuja hapa,,, ningefikiria mara mbili kama mikataba itakuwa inafanyikwa kama tunavyofanya, naombeni sana tuangalia mambo kwa mbali zaidi, tusiangalie kwa nia ya kuongoza nchi, kesho itakuwa UDP, CHADEMA etc... lakini taifa ni hili hili