Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,179
- 133,280
Coach Parcells, kwa kifupi,May someone please explain what this is all about?
S.M.P2503, naomba tofautisha kesi za jina na madai, kesi ya madai huishia pale mdaiwa anapokuwa mufilisi, hata Tanesco ikitangaza kufilisika, assets za Tanesco zitawekwa kwenye attachment ili kulipa registered madeni. Sasa ukilinganisha tozo ya dowans na assets za Tanesco, hiyo tozo ni peanut!.Nilikwisha sema kitambo humu humu JF siku za mwanzo kabisa wakati kesi imefunguliwa huko Paris kwamba njia pekee ya Tanesco kuokoka na mikataba hiyo na madudu yake (Malipo) ni kujitangaza imefilisika...(bankruptsy). Hao wanaotaka kufungua kesi ZAO dhidi ya Tanesco waendelee tu kizifungua na watakuwa wanapoteza resources zao bure kwa kuifungulia kampuni muflisi mashtaka...
Hebu niembieni jamani hivi ni kwa nini Tanesco wanang'ang'ania sana kuendelea kuwepo ili hali kila siku utasikia wanadhaminiwa na kodi zetu kupitia serikalini kuchukua mikopo ya kujiendesha...na kila siku utasikia habari za megawati hewa !!!
Kazi ya umeme imewashinda.. inafaa wakubali kwamba kazi hii ya uzalishaji hawaiwezi na kuachia manyanga na labda watanzania wataunda Tanesco nyingine itakayokuwa free na hizi legal issues na madudu mengine...
Yangu macho na hongera invisible kwa kutuhabarisha haya madudu mengine... lakini ukweli utabaki pale pale kwamba kila siku ukifungua JF na kuona habari za Tanesco hata kabla ya kuzisoma roho inaanza kudunda kwa kujua kwamba wanaongezewa mzigo mwingine wa malipo...
You should have at least laid out your understanding or what you think is the implied meaning of the quoted statements, because you could have taken them out of their legal context, msee.
Not necessarily, especially given the kind of legal language aka legalese applied here. The statements provided appear to be open to interpretation. That being said, you'll need to clarify as to the particular context(s) these statements allude to (according to you), and your own understanding of their legal meanings and/or consequences.
May someone please explain what this is all about?
ni kweli mkuu hapa CCM sijui itatokajetokaje..kuna gemu wanachezeana wao kwa wao humo ndani.. kuhusu Chadema kwenye jambo kama hili kuwa wangefanya nini .. nina uhakika chama makini kama chadema kisingefanya uzembe wa kuingia kwenye janga kama hili .. na kama wangeingia katika hali kama hii basi ingebidi wafanye maamuzi magumu . ccm hawawezi kufanya maamuzi magumu sio kwamba hawataki au hawapendi .. ni kwamba hawawezi na yapo nje ya uwezo wao
Mkuu, CCM hapa itafanya nini kweli? Hawawezi kufanya lolote, pendekezo letu la awali la TANESCO kujitangaza mufilisi lilikuwa na maana japo lilipuuzwa!
Kama CHADEMA au hata CUF wanaweza kuwalaumu CCM kwa hili (la leo) basi watwambie the way forward (wangefanya nini wao katika hali kama hii)
Kakalende, Matapeli wakati wote huwa wanaangalia upepo unavyoenda nakuhakikisha wamejiweka usawa wa kutopoteza walicho ki target , hii ni pamoja na kutumia vifungu vya sheria kuweka sawa mambo ili yawe kisheria zaidi kuliko kitapeli.Hivi ruling ya High Court Tanzania ilishatolewa? Kama bado, halafu hawa matapeli wanaanzisha shauri jingine huko nje nadhani itakuwa ni sarakasi za kisheria!
Hawa Dowans wanafanya haya kwa kushirikiana na watanzania wenzetu, hapa dawa ni kuchapana bakora baadhi ya watu wakatafute hifadhi ya ukimbizi huko wanakoficha vijisenti vyao. Natamani ile sheria ya uhujumu uchumi ingefufuliwa kutoka makabrasha ya Hayati Sokoine, tusingeona upuuzi kama huu.
Hawa Dowans wanafanya haya kwa kushirikiana na watanzania wenzetu, hapa dawa ni kuchapana bakora baadhi ya watu wakatafute hifadhi ya ukimbizi huko wanakoficha vijisenti vyao.
Coach Parcells, kwa kifupi,
Nyerere angekuwa ni rais wa nchi hii, tungevunja uhusiano na ICC, tusingelipa chochote!, mitambo tungetaifisha!, hao wawekezaji wa ulaya wangefungasha virago vyao na kwenda makwao wakatengeneze dhahabu na gesi zao huko viwandani kwao. Wachina wangetuletea teknolojia ya kuichimba dhahabu yetu, gesi yetu na mafuta yetu huku faida asilimia 100%, ikibaki ni mali yetu, kuliko sasa wanavyochimba hawa maharamia kwa jina la waweklezaji, wakikomba asilimia 98% huku wakituachia asilimia 2% eti ndio royality!.
Lakini kwa vile siye yeye, waliopo wanaheshimu utawala wa sheria, wawekezaji ndio tunawanyenyekea na kuwalamba miguu, amini nawaambieni, Tozo tutalipa, tena sio Tanesco, bali serikali kwa kodi zetu!.
dawa ni ubabe,kisheria hatuwezi,kama mkuu wetu wa nchi yupo tayari tuitaifishe kibabe na kuvunja mahusiano na hiyo mahakama full stop!