Lusungo
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 27,139
- 39,375
CCM wangekuwa against hii issue wangeivumbua mapema kwa sababu wana full access na mambo yanayofanyika, lakini walikaa kimya hadi pale issue ilipofunuliwa na mbunge wa upinzani sasa CCM nao wanajifanya kuamka! Hivi lusungo unataka kutuaminisha CCM hasa waandamizi wakuu hawakujua uwepo wa huu uharamia kabla ya mhe. Kafulila?
Unafikiri Kama wanaCCM na wazito wasingekuwa na ridhaa juu ya hili Kafulila angefika wapi??
Jiulize swali jepesi tu ... Unakumbuka majibu ya watawala juu ya sakata hili kwenye hatua za mwanzo kabisa lilipoibuliwa na Kafulila?
Je unadhani bila msukumo Wa hao CCM kwenye hili Kafulila angefurukuta? kuna mangapi yanaibuka na kuzimwa bila lolote kutokea?
Je hujiulizi jeuri na kujiamini kwa watawala juu ya majibu waliyotoa awali imepotelea wapi? ni kafulila tu ameweza kuzima jeuri hii? Kama ndiyo mbona mwanzo hakuweza??
Unaamini ni Kafulila pekee anaehangaisha watawala wasilale??
Kama ndivyo fikra zako zilivyo Una safari ndefu Sana kuutambua ulimwengu huu Wa tabu...
Last edited by a moderator: