JF Exclusive: CAG Report on IPTL/Tegeta Escrow Account

Watanzania maneno mengi vitendo zero hata litapita kama kashfa zingine zilivyozikwa kimya kimya kama hadi Raisi anahusika unafikiri nani mwingine wa kusimama kidete kama wananchi wenyewe maneno matupu
 
Wapi nimetetea naona povu linakutoka, busha ni ugonjwa wa binadamu hata wewe unaweza kupata ugonjwa mbaya kuzidi busha usijione kutembea mzima Mungu kukupa afya ukajiona mjanja kutoa kashfa kwa magonjwa, kuna uzi wangu upo kasome ujue msimamo wangu.



Msimamo wetu hayo mafisi yarudishe PESA walizokwiba ....

kuna picha nimemuona huyo Rugemarila kavaa na rozali kabisa huku kampuni yake ikiwanyonya watanzania.....

ESCROW usipite bila kuondoka na wanyang'anyi...
 
Nimeelewa sana tena sana, nisome vizuri; ikiwa hizo ndio "zilizonyofolewa" na hazina chochote cha maana itakuwa hizo zilizosambazwa?

Fikiri.

Inasemekanika kuna kurasa zaidi ya hizo na ndizo zilizo na nani kamegewa kiasi gani kutoka kwa nani...
 

Kauli kama hizi ni ishara ya kufika mwisho na kukata tamaa!

Inaonekana hakuna jinsi ila liwalo na liwe! Mungu tulinde.
 
Hivi rais anasemaje ju ya hi issue?

alitaka kuzima issue kwa mgongo wa mahakama...ref safar ya jaji mkuu kwake.

pili alimtuma makamo dodoma, kachemsha ameenda zake kukata utepe Arusha.

Sasa tusubiri j5 tu.
 

Jamaa ameandika kuwa yeye pamoja na wengineo (wapo 60 ) wana ripoti kamili...

Ripoti kamili maana yake si hiyo iliyosambaa mtaani bali ni ile iliyotoka kwa CAG na PCCB...

Hivyo hata watuhumiwa wakichakachua bado blueprint ipo na itatolewa pale tu itapohitajika...
 
Msimamo wetu hayo mafisi yarudishe PESA walizokwiba ....

kuna picha nimemuona huyo Rugemarila kavaa na rozali kabisa huku kampuni yake ikiwanyonya watanzania.....

ESCROW usipite bila kuondoka na wanyang'anyi...
Hawa jamaa watu ajabu sana ukiitaja Mkombozi Benki wanasema udini.
 
Hawa jamaa watu ajabu sana ukiitaja Mkombozi Benki wanasema udini.

Ni masharti ya Rugemarila kuwa ili upate hela yake lazima ufungue akaunti mkombozi bank ndo akuingizie....

Hili suala tukiliingia kwa undani zaidi linaweza kuzua makubwa ikaliacha nchi vipande vipande

Ngoja tusubiri mjadala.
 
Kwa sasa 'anaumwa'...

Si unajua mgonjwa huwa hatakiwi kusumbuliwa mwili na akili...

mbona meseji za pole alikua anajibu,atupe pole na hili la escrow
Nazani RWEYEMAMU anaanda andiko lako la kumuepusha boss
 

Mengine sawa, ila mfano wa kulala na mkeo umefika mbali. Hilo haliwezekani.
 
mbona meseji za pole alikua anajibu,atupe pole na hili la escrow
Nazani RWEYEMAMU anaanda andiko lako la kumuepusha boss

yuko holiday ya escrow anasubiri upepo upite ndo aje huyu ndugu ni msanii wa hatari, kimsingi si mgonjwa kama wajinga wengi wanavyo aminishwa.
 
Kwanini kurasa hizo zinyofolewe? Mbona sijaona ubaya wake kwa upande wowote?
Hata mie napata shida zinapigwa kelele nyingi sana lakini ukisoma document hizi sioni shida hata page 59 inayosemwa imeondolewa tumeiona wala haina majina ya watu nchi hii umbea umezidi.
 
Hahahaaa, umenichekesha sana. Nimeangalia hii film juzi, wife akinicheka kuwa naangalia old school.

Lizee hili au Ugly, likiona fedha, linakuwa kama Chenge kama siyo Boss wao, hahahaa, shoot ......

If you want to shoot; shoot dont talk.


Ingekuwa vizuri kama ungeweka makarabasha tujisomee wenyewe bwana Mod.
 
Miaka ya 90's EU na IMF waliupinga sana mkataba wa IPTL wakisema wazi ni mzigo usio wa lazima kwa uchumi wetu mdogo.
Canada ikajitolea gharama dola mil 200 za mradi wa Songas badala ya iptl,wakubwa bado wakang'ang'ana na iptl,yaani mtu anakataa hadi msaada na kulazimisha mkataba ghali kama iptl!
Walipobanwa sana,wakasema miradi yote miwili songas na iptl iende pamoja!
Washauri wa Tanesco wakati huo,Hunton and Williams wakaeleza wazi kuwa mkataba wa iptl haufai kwa kuwa;
-ni wa kipindi kirefu wakati tatizo lilikuwa la kipindi kifupi.
-ulikuwa na gharama kubwa zisizo na sababu.
-ulizidi mahitaji ya umeme na hivyo watumiaji na walipa kodi wangelipia gharama kubwa kuzalisha umeme wasioutumia.
-mkataba uliwapendelea mno iptl
-hakukuwa na ukomo wa muda wa kukamilisha ujenzi hivyo Tanesco kulipishwa gharama kubwa kutokana na ujenzi kuwa prolonged.Gharama zilipaswa kujadiliwa baada ya ujenzi kukamilika.

Nikipitia ushauri huu wa Hunton and Williams,na kwa kuzingatia mazingira ya kifisadi ya nchi yetu,naanza kupatwa na mashaka kama kweli matatizo ya umeme tuliyo nayo yalipaswa kuwa makubwa hivi.
Napata mashaka hata na data tunazopewa kama zina ukweli,hasa kwenye ukubwa wa tatizo,je,ni kweli mahitaji ya umeme au consuption ya umeme ya gridi nzima tunayoambiwa ni ya kweli au imezidishwa ili kuonyesha demand kubwa na hivyo kuhalalisha supply kubwa ambayo mafisadi ndimo wamewekeza?

Napata mashaka kuwa huenda tunao watu wenye ujasiri wa kufikiria kuhujumu mitambo na shirika la Tanesco ili lipate shida ambayo haikuwepo au ilikuwa ndogo na kulikuwa na alternative za kuitatua zenye gharama nafuu,lakini kwa kuwa hazikutoa maslahi kwa certain individuals,zikapigwa chini,tatizo likakuzwa na kuhakikisha linakuwa la muda mrefu ili watu wapige hela,na hivi ndivyo mashirika yetu mengi ya umma yalikufa,hata TTCL nakumbuka ilikuwa inajiendesha kwa faida kubwa,ghafla ikahujumiwa,tukaambiwa inajiendesha kwa hasara,ibinafsishwe.

Wakuu mnaukumbuka ule mgomo wa staff wa Tanesco wakipinga ubinafsishaji na kusema madai ya serikali kuwa Tanesco inajiendesha kwa hasara yalikuwa uongo mtupu?wakaishia kuzunguukwa na FFU!
Mnakumbuka net group solution ilivyokuja kuivuruga Tanesco zaidi?

1997 hazina ilikataa kutoa ushuru wa mafuta ya kuendesha mitambo ya Tanesco,lakini hazina hiyo hiyo ikatoa msamaha kwa wafanyabiashara waagizaji mafuta nje,matokeo yake mgao wa umeme ukafuatia baada ya Tanesco kushindwa gharama za ununuzi mafuta mazito kwa ajili ya mitambo ya iptl.

Hizi zote ni coicidence?
Inaogopesha sana kugundua tunao watz wenzetu wenye roho mbaya hivi,inatisha na kuondoa kuaminiana,na kutoaminiana kukikomaa,huzaa matabaka na makundi,mwishowe civil wars,kila mtu akitaka achukue chake.

Bunge hili litambue Tanzania kwanza,kabla ya vyama na maslahi binafsi.
Shughulikieni hao wezi bila huruma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…