JF business ideas competition

Singidan

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
880
937
Habari wana JF.

Wakuu nimepata wazo la kuendesha shindano la mawazo ya biashara humu ndani. Wazo limekuja baada ya kuona wengi tuna mawazo ila hatuna mtaji. Hivyo mwenye wazo bora akiibuka mshindi atapata zawadi kama mtaji wa wazo lake.

Nimeleta uzi huu kwa kuomba ridhaa kutoka kwa moderators Invisible na wenzake juu ya hili wanasemaje na wadau wengine naombeni mchango wa mawazo juu ya hilo kabla sijalizindua.

UJASIR.jpg
 
Ni wazo zuri sana kwa sababu licha ya kushindana pia itakuwa ni sehemu ya kuongeza maarifa. Hongera kwa kufikiria jinsi ya kuwakomboa wana JF!
 
wazo zuri sana sasa hujatoea vigezo gani vinavyotakiwa na je mtu afuate taratibu gani
 
1. mkuu unataka mawazo yawekwe humu kwenye uzi?
2. Ni vigezo gani vitakavyotumika kupima ubora wa wazo husika na wapimaji ni akina nani?
3. Mwanzo wa shindano ni lini na mwisho ni lini?
4. Unaposema utatoa zawadi kama mtaji wa kuwezesha wazo husika, je! haitajalisha kuwa wazo litahitaji mtaji wa kiasi gani? yaani hata kama wazo litahitaji milioni 100, haina shida?

Msaada tafadhali!
 
Majibu.
1. Mawazo yatawekwa humu kwa quote uzi wa shindano pindi unapowasilisha.
2. Vigezo vya kushiriki kuweka ni kutakuwa na khngilio cha shindano, ku quote uzi wa shindano wakati wa uwasilishaji wazo. Kutuma pesa ya kiiingilio ambayo itahusika kuendesha shindano lenyewe kwa sababu shindano hili litajiendesha lenyewe. Pia ubora wazo utapimwa kulingana na ubunifu wako na wapimaji watatoka nje ya jf.
3. Shindano litanza utaratibu ukikamilika.
4. Utaratibu utatoka namna ya mawazo wapi yenye mtaji gani ndiyo yatafaa.
Ahsante mkuu
 
Nilivyoona kutoa hela tu mzuka ukaisha kabisa, ngoja nisepe.
 
Nadhani ungeweka Email ili MTU MWENYE project yake lakini hana Mtaji akufowadie, then Unashindanisha...
Nawaza tuu
 
Back
Top Bottom