Jeshi litachukua nchi Misri?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,202
Reaction score
44,238
Kwa hali ilivyosasa naamini ndani ya masaa 72 yajayo yataamua Misri inaelekea wapi. Kuna dalili zote kuwa bila ya Mubarak kuachia ngazi wananchi Misri hawatakoma. Ukishaanza kuua wananchi wako kwa ajili ya kubakia mabadarakani katika mazingira ya kisiasa unachochea wananchi wako kuzidi kukupinga. Hii ni kanuni ambayo bado haijaoneshwa kuwa ya uongo.

Hivyo, naamini kwa kuangalia hali ya kisiasa sidhani kama mabadiliko ya kiuongozi yaliyofanywa na Mubarak yatatosha kuwatuliza wananchi- Hivyo umebakia uamuzi mmoja tu nao ni jeshi kuchukua madaraka na kuandaa muda wa kurejesha utawala wa kiraia.

Kikubwa zaidi kinachofanywa nyuma ya pazia ni kuzuia Muslim Brotherhood kuingia madarakani katika mazingira haya.
 
Inaelekea hata jeshi kuingia mitaani na vifaru ni maelekezo toka DC maana hawataki kabisa kuona kuna leadership vacuum katika nchi ambayo wanaiona ina umuhimu mkubwa kwao.
 
let hosni mubarak go away, ruling for the 30 years as if no any other person within his party or country capable to rule is an insult to Eqyptians
 
there is no way he will remain on Power, watu wameshachoka na maisha, he must
step down, na ukitaka kujua Jeshi lipo lipo tu ni pale wananchi wa Misri wanapokaa
kwenye vifaru pamoja na wanajeshi na wanajeshi wanonyesha alama ya vidole
viwili, kati ya picha iliyo nitouch look this huko EgyptView attachment 21740 No one can
stop Peoples' power, lazima UCHAGUZI UFANYIKE
 
Hapa ndio watu wanaomuita Nyerere alikuwa Dikteta inabidi wajiulize kama bado wana utimamu!
 
 
haya yamefika ndugu zangu, ikitoka misri , sudan, ikitoka sudan Kenya then zimbabwe na 2013 inaweza kufika bongoland
peoples power inatisha
 
hivi kwa nini siyo tanzania? mbona na sisi tumekichoka chama kilichopo madarakani ila hatuchukui hatua? dowans epa IPTL MFUMUKO WA BEI, MIKATABA MIBOVU NA HUDUMA MBOVU ZA KIJAMII HIVI HATUJAPANDISHA HASILATU?
 
Over 100 people have been killed kwa hasira wananchi wamebreak prison.
Kuna taarifa jeshi hawataki kuua wananchi ndo maana wanawaacha raia kupanda maderaya yao.
Hakuna namna Mubarak akabaki salama.
 
However one looks at it: Mubarak is kwishehi! Jeshi linaweza kabisa kuchukua madaraka au kuwa na shinikizo kubwa katika mabadiliko yeyote ya kisiasa yatakayotokea Misri. Such has been the tradition since the 1952 army coup.

Naungana na Bubu A. K., nadhani wamarekani wanaushawishi mkubwa katika swala hili ukiangalia kwamba serikali ya marekani inatoa msaada wa $ 1.3 bilioni kwa mwaka kwa jeshi la Misri.

Hivi sasa inaonekana wamarekani wanahaha na kuogopa isije jamaa wa Muslim Brotherhood au kikundi chochote chenye siasa kali (so called 'islamic fundamentalists') kuchukua madaraka.
 
hivi kwa nini siyo tanzania? mbona na sisi tumekichoka chama kilichopo madarakani ila hatuchukui hatua? dowans epa IPTL MFUMUKO WA BEI, MIKATABA MIBOVU NA HUDUMA MBOVU ZA KIJAMII HIVI HATUJAPANDISHA HASILATU?

Tatizo la Watanzania the people reflect the leaders themselves. Tanzania wanasiasa mdomo mwingi bila action na wananchi hivyo hivyo. Tunisia kaanzisha mtu mmoja tu na wengine wakafuata. Sasa nyie wanaJF mnaoshabikia mapinduzi mbona hamna hata mmoja kati yenu ambae yupo tayari kuanza na wengine wakafuata?
 
Tunasubiri filimbi ya mwisho...


Filimbi ya mwisho imeshapulizwa na kuashiria kwamba the game is over for Mubarak. Sasa hivi nadhani anajitahidi kuomba usalama wake na familia yake yote na pia kuwaomba Marekani wamtafutie nchi ambayo itampokea kwa mikono miwili bila kumgusa au kumkamata na pia kupatiwa usafiri wa huko aendako. Sidhani kama kuna nchi ya magharibi itakayokuwa tayari kumpokea hivyo uwezekano mkubwa atakwenda katika moja ya nchi za ME hasa Saudi Arabia.

http://www.msnbc.msn.com/id/41337168/ns/world_news-mideastn_africa
 
Hivi kama kura zilipigwa na Mubarak akaibuka kuwa mshindi, then mbona idadi kubwa ya wananchi wake wanampinga?
Hizo kura nyingi zilizomweka madarakani zilipigwa na wananchi wa wapi?
Tanzania jujifunze.
 
Tunasubiri filimbi ya mwisho kwa rais Mwizi.
 
There is no such a thing as presidency for life. Mubarak is a loser as we stand now. And the most hurting issue to him is that he would not be in a position to leave the country in the hands of his son whom he started preparing for the job.
After shedding blood, you can't reverse the worse case scenarios possible
 

Hakuna mamlaka iliyowahi kushinda nguvu ya umma kama historia inavyosema. Kuanzia Shah wa Iran, Fernand Marcos n.k.
Haya ni matokeo ya hasira zilizojilimbikiza miaka nenda na sasa jipu linapasuka.
Kuwepo kwa Mubarak ni kutokana na baraka za Nchi za Magharibi zenye Maslahi Mashariki ya kati. Misri ina ushawishi mkubwa sana eneo hilo na anguko la Mubarak litaleta usumbufu sana kwa Marekani. Uwoga mkubwa ni pale maandamano hayo yatakapowapeleka Muslim Brotherhood madarakani. Hawa jamaa wana ushawishi mkubwa sana mashariki ya kati na wanauwezo wa kubadili sura ya mambo. Brotherhood wana wasomi wakubwa sana katika viwango vya PHD na ndio wanaochambua mambo ya kisiasa duniani. Ni hawa jamaa ndio walioamsha hisia za katuni za Mtume.
Lakini hofu kubwa zaidi ni hatari ya mkataba wa Camp David kati ya Misri na Israel. Kama ataingia madarkani mtu mwenye msimamo tofauti na wa sasa, eneo hilo litakuwa na vita tena kama miaka ya 60. Hii pia itawapa nguvu Hamas na Hezboullah na hatima yake ni mgogoro mzito.
Ni mtihani mgumu kwa nchi za Magharibi hasa US inayotoa Dollar Billion 1.2 kama misaada. Kuna msemo unaosema '' Better the devil you know than the Angel you don't know''
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…