Kwa hali ilivyosasa naamini ndani ya masaa 72 yajayo yataamua Misri inaelekea wapi. Kuna dalili zote kuwa bila ya Mubarak kuachia ngazi wananchi Misri hawatakoma. Ukishaanza kuua wananchi wako kwa ajili ya kubakia mabadarakani katika mazingira ya kisiasa unachochea wananchi wako kuzidi kukupinga. Hii ni kanuni ambayo bado haijaoneshwa kuwa ya uongo.
Hivyo, naamini kwa kuangalia hali ya kisiasa sidhani kama mabadiliko ya kiuongozi yaliyofanywa na Mubarak yatatosha kuwatuliza wananchi- Hivyo umebakia uamuzi mmoja tu nao ni jeshi kuchukua madaraka na kuandaa muda wa kurejesha utawala wa kiraia.
Kikubwa zaidi kinachofanywa nyuma ya pazia ni kuzuia Muslim Brotherhood kuingia madarakani katika mazingira haya.