Watanzania wapasha habari Bwana tabu tupu wakilindwa shida!!! wasipolindwa serikali gani hii??? mambo ni ilimradi tu wamelaumu hivi au vileHabari wakuu.
Kuna hali ambayo siyo ya kawaida hapa Songea kwani asubuhi ya leo kila kona hapa Mjini na nje ya Mji Wanajeshi wametapakaa mitaani na hakuna taarifa yoyote ya uhakika iliyopatikana, watu wameingiwa hofu hata vyombo vya usafiri ikiwemo bodaboda kama ilivyozoeleka hakuna.
Mji umepoa sana.
Kwa mwenye taarifa zaidi tujuzane waungwana.
Wese? Aya!
Kama umesafir leo basi umepekuliwa na jwtz
Ni kweli mkuu nipo na gari ndogo tinted imenilazimu nizitoe zote imebaki clear! wanaweza wakakushuku wakakupasua ubongo ndan ya gari
Weee.. Unazungumzia JWTZ Hawa wanaopigaga wananchi mtaani au..? Hao wapo kama form two wa enzi zile mashuleniHahahahaha...mkuu umenifurahisha sana..ila JWTZ hawako hivyo..
Tena pale karibu kabisaa na kambi ya jeshi ya RuhuwikoBasi la superfeo la Dar mbinga lilizuiliwa eneo la national milling Usiku huu Kwa Muda wa saa nzima. wananchi hawaelewi kinachoendelea wanaogopa yasije yakawa ya 2005
hayo ni mazoezi ya kawaida kwa tuliopita jeshi inaitwa route march
Acha unanga route match ya kuzagaa mtaani ni ya jeshi gani?
Vijana wa JKT mujibu wa sheria wanajiona wameiva sana Mkuu, mimi nadhani huo mkusanyiko wao utakuwa ni sehemu ya mafunzo yao, mara nyingi huwa wanajigawa makundi mawili, kundi la Adui na kundi la mapambano. Wanweza anzia porini na kuja mpaka mjini kulingana na mwelekeo wa Adui.
Nafikiri ndicho walichokuwa wanafanya hao Walinzi wetu, Watu wa Songea toeni hofu.