Jeshi la wananchi (kambi ya gongo la mboto) limeasi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi la wananchi (kambi ya gongo la mboto) limeasi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lukolo, Feb 26, 2011.

 1. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Katika namna ambayo inatia mashaka, kambi ya jeshi ya gongo la mboto imeendeleza mfululizo wa mauaji, ukatili, unyama na ubabe kwa wananchi wasio na hatia. Wakati wananchi wakiendelea kuugulia maumivu ya mabomu yanayoaminika kulipuliwa kwa makusudi na wanajeshi hao wa gongo la mboto, jana wanajeshi hao walitinga mitaani na kuanza kutembeza kichapo kwa raia wasio na hatia. Kwangu mimi, hii ni ishara kwamba wanajeshi hawa wa kambi ya jeshi ya gongo la mboto hawapo kwa ajili ya ulinzi wa wananchi bali wapo kwa ajili ya kuangamiza na kuteketeza wananchi wa maeneo ya jirani. Hii inanipa shaka pia kwamba wanajeshi hawa wanye hasira na wananchi, wanaweza kuyalipua tena mabomu yaliyobakia pale ghalani ili kuwamaliza kabisa wananchi walio karibu na kambi hii au wa Dar es salaam nzima kwa kuwa tumeambiwa yaliyobakia ni makubwa zaidi ya yaliyolipuka.

  Kuna ushahidi mwingi wa kimazingira unaoonyesha kwamba mabomu ya gongo la mboto yalilipuliwa kwa makusudi ili kuwaua na kuwaangamiza watanzania wasio na hatia. Ushahidi mmojawapo ni kitendo cha wanajeshi hao kuhamisha familia zao mapema asubuhi kabla ya milipuko na kutokuwepo kwa wanajeshi wengine hapo kambini isipokuwa walinzi. Kama wanajeshi hawa walijua kungekuwa na milipuko hiyo, kwanini hawakuwatangazia wananchi ili wakae mbali na maeneo ya jeshi? Huu ni ushahidi tosha kwamba pana uasi hapa! Kwa mazingira ya ulipukaji wa mabomu, na kwa yale yaliyofanyika jana, ya wanajeshi kuwavamia raia wasio na hatia na kuwachapa, najiridhisha kwamba wanajeshi wa kambi hii wameshaasi, na hivyo siku si nyingi wanaweza kushika bunduki na kuingia mitaani kutuua kwa risasi baada ya jaribio la kutuua kwa mabomu kutokuzaa matunda yaliyotarajiwa.

  Mwisho natoa wito kwa wakaazi wa gongo la mboto na maeneo ya jirani kuandaa maandamano ya kulipinga jeshi hili lililoasi na pia kumpinga Kikwete kwa kuwa ameshindwa kusoma alama za nyakati na kuchukua hatua.
   
 2. c

  carefree JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Poleni inasikitisha sana sababu ya kutembeza kichapo ni nini?
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  kWELI cAREFREE!
  Bila kujua sababu ya wao kutembeza kichapo hicho hatuwezi kufikia conclusion yoyote!
   
 4. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Binafsi hata sijui, nilijikuta naingia tu kwenye mkumbo wa kichapo bila hata kuambiwa kwanini nachapwa. Jamaa walikuwa wanatoa kisago kile cha kuua kabisa. Ni bakola, ngumi, teke, vichwa and so on. Yaani utafikiri ndo tupo vitani kabisa. Ukionyesha kutaka kujibu wanasaidiana hata watatu kukushambulia. Hali ilikuwa ni mbaya, hawajali upo na nani, kama upo na mkeo unaweza kula kipigo wewe na mkeo au hata na babako au mamako. Kwakweli ni situation inayoudhi kwelikweli.
   
 5. c

  carefree JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Duh poleni nimekwama hata kuandika najaribu kuhisi pengine waliowapiga ni wanajeshi wa nchi nyingine si unajua huwa mavazi yanafanana au wamepata wazimu . Katika hali ya kawaida huwezi kupiga mtu sembuse watu bila sababu . Nimekumbuka inawezekana wameamua kutumia njia hiyo kuishinikiza serikali iwaboreshee maslahi huku uraiani si huwa tunaandamana
   
 6. N

  Napo Member

  #6
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii habari binafsi nimesimuliwa na mkazi wa g.mboto kwa njia ya simu "Ebwana kuna mwanajeshi kavamiwa na wananchi kapigwa kweli kisa eti wanasema wanajeshi walifanya makusudi kulipua mabomu" kiukweli nlifadhaishwa sana,gafla akapga simu tena "jamaa wamerudi wanagawa kpgo hapa nipo njian nakimbia" jamaa unapoleta hoja kama hiyo nivema utoe sababu zilizosababisha kuliko kuleta hoja ambazo zitatuwekea uadui na walinzi wa taifa letu! Kiukweli jamaa wanafany kazi ngumu mno,binafsi nimetokea mipakan 'hawalali kutulinda sisi' inaleta hasira unamlinda mtu tena kwa kujitolea then mnampga mmojawao What are we expecting?
   
 7. c

  carefree JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hapo wote wamekosa busara raia na hao wanajeshi ila wanajeshi kwa walipaswa kuwa na busara zaidi ili la kupiga watu hovyo halijatulia hata kidogo
   
 8. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,306
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  hameni.
   
 9. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,306
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  busara kivipi mkuu? mbwa umlishe then akutafune utafanyaje? ni kutafut rifle tu uachanishe roho na mwili wake. in that case walikuwa sahihi kutoa dozi ili watu wawe na heshima. jeshi siyo la kudharauliwa hata na mtu wala kiongozi wa nchi. kueni muyaone. msilete siasa na jeshi. uhuru uwe na mipaka ndugu zanguni. huwezi wadharau watu wanakulinda na wanarisk maisha kwa ajili yetu sisi. wakanyeni wadogo na watoto zenu wasipige walinzi wa jamhuri yetu. kuhamisha familia ilikuwa sikukuu watu wako outing. mwe!
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hivi hawezekani kufungua kesi....
   
 11. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Wewe unaishi dunia gani?

  Ni jeshi gani duniani liliwahi kupigana nawananchi wake likashinda??
  Jeshi hushinda vita kwa nguvu ya wananchi siyo bunduki.

  Jeshi likidharau na kuanza kupiga hata kuua wananchi Safari yakumegeka kwake na hatimaye kusambaratika huwa imezaliwa.

   
 12. c

  chetuntu R I P

  #12
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole zao wana Gongolamboto!dah full misukosuko.
   
 13. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  kujitolea???kwani kazi ya ujeshi ni wito??vp hawalipwi hawa??
   
 14. N

  Napo Member

  #14
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sizinga,unaeshmika humu janvini..! Mtu anatoa uhai wake kukulinda ww na unafurahia utulivu,unaweza kumlipa kiasi gani mtu huyo!?
   
 15. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  we mwanajeshi acha kujustify ujinga wa wanajeshi kupiga raia. kuwa mjeshi siyo ndiyo iwe sifa kupiga watu
   
 16. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kwa kweli hili ni kosa kubwa mno alifai kufanywa na wanajeshi wetu ukizingatia tunaishi nao pamoja mitaani tunakunywa wote tunagombea madem wote leo wametulipulia mabomu watu wamekufa, nyumba zimeharibiwa leo wanatufata live kwa kichapo cha mbwa mwizi?
   
 17. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #17
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  Mwanangu na uelewe kwamba,Jeshi ni samaki na sisi raia ni bahari mtoe samaki baharini hawezi kuishi
  Na sisi tunatoa uhai wetu kuwalisha ni mgawao wa kazi tu.
  Wanalinda nini! wakati mali za wananchi na nchi yenyewe inaibiwa na kubemendwa na mafisadi na matapeli wa kigeni wao wanaangalia tu na kuwapigia saluti.
  Iko siku kitaeleweka tu.
   
 18. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #18
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  Sielewi hekima ya mfano wako anaelishwa ni nani kati ya raia na mwanajeshi (mbwa anaelishwa?)
  Ni kweli hadi raisi wa nchi anawaogopa wanajeshi? maana yeye ni Amiri jeshi mkuu.
  Hivyo basi Rais na wanajeshi lazima wawaogope na kuwaheshimu raia maana wao ndio walio waajiri.
  KINYUME CHA HAPO WATAPAMBANA NA NGUVU YA UMMA.
   
 19. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wanajeshi wakapimwe akili yawezekana wameathirika kisaikologia!
  Na ninyi mliopewa kichapo mlishindwa kumkamata mmoja wao na kufa nae ka ushahidi????
   
 20. g

  gongolamboto JF-Expert Member

  #20
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 508
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Wanajeshi kupiga raia ni utovu wa nidhamu. Lakini kwa Tanzania hilo limekuwa gonjwa sugu. Raia wenapigwa sana na wanajeshi lakini mamlaka zinazohusika zinakaa kimya. Wanajeshi wanajiona wao ni untouchable katika nchi hii. Huwa wanachokoza raia kwenye mabaa, wakidundwa wanaenda kukusanya wenzao na kuleta maafa kwa raia hata wasio na hatia. Mie naomba niwakumbushe kama wamesahau. Kuna raia wengi sana wapepata mafunzo ya kijeshi na wana uwezo mkubwa sana kuliko hao wanajeshi feki waliopo sasa. Wasipojiheshimu watafundishwa adabu.

  Halafu kujidai wanatulinda, mie sioni lilote wanalifanya. Wanatulinda na adui yupi? Wao wanatekeleza majukumu yao ya kazi kama wengine. Kama walimu, madaktari, polisi nk. Na mshahara wanalipwa kwa kodi zetu.

  Wakiona kazi hiyo haiwafai waachane nayo.
   
Loading...