Jeshi la wananchi Egypt lampindua Rais Morsi

Jeshi la wananchi Egypt lampindua Rais Morsi

Kikao kimemalizika kati ya wakuu wa SCAF, viongozi wa vyama vyote na MB na tamko linafutia muda si mrefu.
 
egypt1680FB680.jpg
 
Mohamed Mursi amekwishaambiwa kwamba yeye si rais wa Misri tangu masaa matatu yaliyopita, kinachosubiriwa ni serikali ya mpito itayoongoza hadi utakapofanyika uchaguzi mwingine.
 
Linatamkwa jina la Mohamed El-Baradei ambae aliwahi kuongoza taasisi ya ukaguzi wa silaha za kinyuklia.
 
Kamanda mkuu wa jeshi anaongea sasa.
 
Wananchi wanamsikiliza mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ya Misri au SCAF generali Abdul Fatah Khalil Al-Sisi akizungumza kwenye luninga.

Al- Sisi pia ndie waziri wa Ulinzi wa Misri.
 
live kiongozi wa kijeshi anatangaza mda huu
 
Anatangaza political road map kutatua mgogoro.

  • Katiba imekuwa suspended kwa muda.
  • Jaji Mkuu wa Mahakama ya Katiba atakuwa kiongozi wa muda mpaka Rais mpya achaguliwe.
  • Jaji Mkuu atatangaza uchaguzi wa Rais mapema iwezekanavyo.
  • Chief justice wa Mahakama ya Katiba atachukuwa madaraka kama interim leader mpaka uchaguzi mkuu utakapofanyika
  • Mahakama ya katiba itaandaa uchaguzi wa bunge jipya.
  • Freedom of expression na free media vitaendelea kuwepo.
  • Hatua zote zitachukuliwa kuhakikisha kuwa vijana wanahusishwa kwenye maamuzi.
  • Wamisri wameombwa wameobwa kuwa watulivu.
 
Jambo muhimu ambalo Generali Al-Sisi amesema ni kwamba Mohamed Mursi alionywa kwa miezi mingi tu kwamba hali ya kutokukubaliana na wapinzani wake kwenye mambo kadhaa (ya msingi) kungempeleka mahali pabaya..
 
Jeshi la Misri limechukua nchi.

Source: Al jaazera
 
It is official now: MORSI HAS BEEN OVERTHROWN
 
Back
Top Bottom