Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia wahamiaji haramu 14 raia wa Burundi, waliokamatwa wakiwa wameingia nchini kinyume na sheria kwa kutumia usafiri wa magari Mawili tofauti ya abiria
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana, Novemba 23 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbroad Mutafungwa, watuhumiwa hao walikamatwa kwenye kizuizi cha barabara kilichopo Kijiji cha Busisi, Tarafa ya Sengerema saa 7:30 mchana wakisafiri ndani ya Basi gari aina ya tata linalofanya safari zake za Kabanga (Ngara) kwenda Mwanza.
"Jumla ya wahamiaji haramu 13 walikamatwa tarehe Novemba 23, 2025 majira ya 7.30 mchana wakiwa wanasafiri ndani ya gari aina ya Tata yenye usajiri T. 337 DYA, mali ya Chiza Francis Lugubi, mkazi wa Dodoma, linalofanya safari zake kati ya Kabanga (Ngara, Kagera) na Mwanza,"
Hata hivyo Kamanda Mutafungwa amesema walifanikiwa kumkamata Kondakta wa Basi hilo, Pendo Matembere (36) Mkazi wa Nyegezi jijini Mwanza, huku dereva wa gari hilo Jonas Richard akifanikiwa kutoroka