Jeshi la Polisi linambeba DED wa Itigi kwa maagizo na manufaa ya nani?

Niliumia sana ndugu yangu Kwa jina la Mkumbo aliondolewa kwenye ukurugenzi katika wilaya moja huko tanga Kwa kuendesha gari na kubishana na polisi ila muuaji/mshiriki wa mauaji anarembwa rembwa eti hakuwepo. Nchi hii Kuna watu wameigawa Sana Kwa tabia zao za kibaguzi
 
JESHI LA POLISI LINAWABEBA DED WA ITIGI KWA MANUFAA YA NANI?

Chama cha ACT Wazalendo kimesikitishwa na taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida iliyonukuliwa na vyombo vya habari kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Ndugu Pius Luhende "alikuwa nje ya kanisa wakati mauaji yakifanyika hivyo basi yeye si mtu aliyemfyatulia risasi Ndugu Isaka Petro".
Maelezo haya ya Jeshi la Polisi yanakwenda kinyume na maelezo ya Ndugu wa marehemu na waumini wote waliokuwepo ndani ya kanisa siku ya Jumamosi ya tarehe 2 Februari mwaka huu, wakati mauaji hayo yakifanyika.
Kwa mujibu wa Baba wa Marehemu na waumini wa kanisa hilo, aliyemfyatulia risasi marehemu ni Mkurugenzi wa Itigi Ndugu Luhende. Maelezo kuwa Mkurugenzi wa Itigi siye aliyefyatua risasi, polisi wameyatoa wapi?!
Ni jambo linalofadhaisha kwamba jeshi la polisi linajaribu kufanya hila ili kupindisha haki kwenye tukio hili la mauaji ya kinyama yaliyofanyika kwenye nyumba ya Mungu.
Tunachojiuliza ni kwamba Jeshi la Polisi linayafanya yote haya ili kumnufaisha nani na kwa maelekezo ya nani?
KAULI YETU:
1. Tunaendelea kulaani tukio hili la kinyama lililofanyika kwenye nyumba ya ibada. Bila shaka haya ni matunda ya vitendo vya kibabe vilivyoshamiri katika serikali ya awamu ya tano miongoni mwa watendaji wa serikali na kufumbiwa macho na serikali kuu.
2. Tunataka haki itendeke bila kuangalia nani ana cheo gani au ana mahusiano na mkubwa gani serikalini. Kila mtendaji wa serikali na askari aliyeshiriki kwenye kitendo hicho cha kinyama achukuliwe hatua za kisheria.
3. Tunawakumbusha Watendaji wa Serikali hasa Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa kuzingatia sheria katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ado Shaibu,
Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi,
ACT Wazalendo.
08 Februari, 2019.View attachment 1019076

Sent using Jamii Forums mobile app
Ado, Kama itatokea hiyo, na kama mzazi wa marehemu atakubali kutoa ushahidi wa uongo au mchungaji au waumini watatoa ushahidi wa uongo, itathibitisha pesa ilivyo na nguvu kuliko chochote. DED ni cheo kidogo sana ktk nchi kiasi cha kuruhusu uhai wa mtu upotee bila adhabu, eti tu ni DED.

Lakini Tusishangae maana nchi hii au Afrika ni matukio ya kawaida kutetewa na serikali kama inaona una uhusiano wa karibu na wansiasa. Tuliona ya Ditopile akitetewa na hata rais wa nchi kujidai kutoa ubani kwa familia ya marehemu bila kujali ubora wa akili yake na hatimaye nature ikachukuwa nafasi. Leo hii hatumsikii Ulimboka na hata familia yake haijawahi kusema baya juu ya yaliyompata kijan wao. NI aibu, utu unapokuwa chini kabisa kiasi hiki.
 
Ulikuwepo eneo la tukio na ukamuona DED akishika Bastola? Ado Shaibu ni mkazi wa itigi?Basi itabidi jeshi la polisi likuchukue na kukuhoji juu ya tukio hilo.



jingalao, tafadhali sana jaribu kuficha ujinga wako, kwa sasa umebaki wewe tu humu JF
 
Hapo kanisani hawakuwepo "RAIA wenye hasira Kali"?

Wangefanya kama yule Mwenyekiti wa kule Mwanza wangetoa funzo.

Hapa " Kidevu" kashatoa maagizo mpwa anakingiwa kifua tu.

Yule DED wa Bukoba alikosea takwimu tu akaomba DT aje afafanue akatumbuliwa ila huyu anatuhumiwa mauaji kabisa lakini hadi Leo hii uteuzi wake Bado haujatenguliwa.

Alafu kila uchwao utamsikia "mniombee" Mimi kamwe sitamuombea nikiomba daima dua yangu ni "eeeh Mungu ikikupendeza utuepushe na kikombe hiki".
Kama mnafikiri kuua,kuteka,kutesa ni makosa kwa JPM mtasubiri Sana...
 
Back
Top Bottom