Jeshi la Polisi linambeba DED wa Itigi kwa maagizo na manufaa ya nani?

Ulikuwepo eneo la tukio na ukamuona DED akishika Bastola? Ado Shaibu ni mkazi wa itigi?Basi itabidi jeshi la polisi likuchukue na kukuhoji juu ya tukio hilo.
Jina lako limetoa jibu tayari
Mwandishi kasema kauli zinakinzana
Waliokuwepo kwenye tukio wanasema aliefyatua risasi ni huyo DED lakini polisi ambao hawakuwepo wanasema DED alikuwa nje so hahusiki na ufyatuaji wa risasi.
Hizi ni kauli mbili kinzani kati ya watu waliokuwepo wakati wa tukio.na ambao hawakuwepo sasa hapa sijui nani anasema ukweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe kilaza wa kijani ,wewe ndio ulikuwepo ukaona aliempiga risasi sio ded Mr luhende Pius shija, halafu watu humu tunamjua kuliko unavyomjua wewe ,kwa kumsoma kwenye mtandaoni ni bonge la kilaza uliza waliosoma nae university of Arusha .
 
Kitendo cha kwenda kufuata kodi Kanisani kinanishangaza hadi leo,alishindwa means zote hadi kwenda church? Kuna maswali mengi yasiyo na.majibu
 
JESHI LA POLISI LINAWABEBA DED WA ITIGI KWA MANUFAA YA NANI?

Chama cha ACT Wazalendo kimesikitishwa na taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida iliyonukuliwa na vyombo vya habari kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Ndugu Pius Luhende "alikuwa nje ya kanisa wakati mauaji yakifanyika hivyo basi yeye si mtu aliyemfyatulia risasi Ndugu Isaka Petro".
Maelezo haya ya Jeshi la Polisi yanakwenda kinyume na maelezo ya Ndugu wa marehemu na waumini wote waliokuwepo ndani ya kanisa siku ya Jumamosi ya tarehe 2 Februari mwaka huu, wakati mauaji hayo yakifanyika.
Kwa mujibu wa Baba wa Marehemu na waumini wa kanisa hilo, aliyemfyatulia risasi marehemu ni Mkurugenzi wa Itigi Ndugu Luhende. Maelezo kuwa Mkurugenzi wa Itigi siye aliyefyatua risasi, polisi wameyatoa wapi?!
Ni jambo linalofadhaisha kwamba jeshi la polisi linajaribu kufanya hila ili kupindisha haki kwenye tukio hili la mauaji ya kinyama yaliyofanyika kwenye nyumba ya Mungu.
Tunachojiuliza ni kwamba Jeshi la Polisi linayafanya yote haya ili kumnufaisha nani na kwa maelekezo ya nani?
KAULI YETU:
1. Tunaendelea kulaani tukio hili la kinyama lililofanyika kwenye nyumba ya ibada. Bila shaka haya ni matunda ya vitendo vya kibabe vilivyoshamiri katika serikali ya awamu ya tano miongoni mwa watendaji wa serikali na kufumbiwa macho na serikali kuu.
2. Tunataka haki itendeke bila kuangalia nani ana cheo gani au ana mahusiano na mkubwa gani serikalini. Kila mtendaji wa serikali na askari aliyeshiriki kwenye kitendo hicho cha kinyama achukuliwe hatua za kisheria.
3. Tunawakumbusha Watendaji wa Serikali hasa Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa kuzingatia sheria katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ado Shaibu,
Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi,
ACT Wazalendo.
08 Februari, 2019.View attachment 1019076

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoto wa dada Ado
Acha kelele..
Halafu Polisi kauli zao siku hizi ni za mwisho. Alie toa haya maelezo apandishwe cheo... Full stop

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulikuwepo eneo la tukio na ukamuona DED akishika Bastola? Ado Shaibu ni mkazi wa itigi?Basi itabidi jeshi la polisi likuchukue na kukuhoji juu ya tukio hilo.

Kama cctv kwa lisu mliziondoa,hata huyo jamaa angekuwepo eneo la tukio mngebisha tu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
mtasingizia watu tuhuma za mauaji hadi lini?
Jingalao, acha ubishi! Ushahidi wa mazingira unatosha kabisa kumtia dc hatiani. Hata kama alikuwa nje ya kanisa alikuwa akifanya nini wakati yeye siyo muumini wa kanisa hilo?
Kama kiongozi ilitosha tu kuwaelekeza polisi kumkamata mtuhumiwa na kufikishwa polisi kisha yeye akaandika statement yake polisi pia na mtuhumiwa akapelekwa mahakamani na kama alihitaji mjadala angeomba ruhusa polisi na akaufanyia polisi.
Kwa maana hiyo yeye anabaki kuwa key suspect! Isitoshe, ni kwanini aende na askari wa wanyapori ilihali siyo kazi yao kuarrest na kushtaki?
Hebu jitunzie sehemu ya heshima uliyobaki nayo basi hapa jf na usiutete uuaji wa namna yoyote wa binadamu mwenzako bali sheria na taratibu zifuatwe! Yaweza kutokea kwako au ndugu yako je, utatetea hivihivi? Nakuheshimu japo tunasigana kwa hoja!
 
Back
Top Bottom