Jeshi la Polisi linambeba DED wa Itigi kwa maagizo na manufaa ya nani?

Ado Shaibu

Verified Member
Jul 3, 2010
99
225
JESHI LA POLISI LINAWABEBA DED WA ITIGI KWA MANUFAA YA NANI?

Chama cha ACT Wazalendo kimesikitishwa na taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida iliyonukuliwa na vyombo vya habari kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Ndugu Pius Luhende "alikuwa nje ya kanisa wakati mauaji yakifanyika hivyo basi yeye si mtu aliyemfyatulia risasi Ndugu Isaka Petro".
Maelezo haya ya Jeshi la Polisi yanakwenda kinyume na maelezo ya Ndugu wa marehemu na waumini wote waliokuwepo ndani ya kanisa siku ya Jumamosi ya tarehe 2 Februari mwaka huu, wakati mauaji hayo yakifanyika.
Kwa mujibu wa Baba wa Marehemu na waumini wa kanisa hilo, aliyemfyatulia risasi marehemu ni Mkurugenzi wa Itigi Ndugu Luhende. Maelezo kuwa Mkurugenzi wa Itigi siye aliyefyatua risasi, polisi wameyatoa wapi?!
Ni jambo linalofadhaisha kwamba jeshi la polisi linajaribu kufanya hila ili kupindisha haki kwenye tukio hili la mauaji ya kinyama yaliyofanyika kwenye nyumba ya Mungu.
Tunachojiuliza ni kwamba Jeshi la Polisi linayafanya yote haya ili kumnufaisha nani na kwa maelekezo ya nani?
KAULI YETU:
1. Tunaendelea kulaani tukio hili la kinyama lililofanyika kwenye nyumba ya ibada. Bila shaka haya ni matunda ya vitendo vya kibabe vilivyoshamiri katika serikali ya awamu ya tano miongoni mwa watendaji wa serikali na kufumbiwa macho na serikali kuu.
2. Tunataka haki itendeke bila kuangalia nani ana cheo gani au ana mahusiano na mkubwa gani serikalini. Kila mtendaji wa serikali na askari aliyeshiriki kwenye kitendo hicho cha kinyama achukuliwe hatua za kisheria.
3. Tunawakumbusha Watendaji wa Serikali hasa Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa kuzingatia sheria katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ado Shaibu,
Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi,
ACT Wazalendo.
08 Februari, 2019.
20190209_224543.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,080
2,000
Ulikuwepo eneo la tukio na ukamuona DED akishika Bastola? Ado Shaibu ni mkazi wa itigi?Basi itabidi jeshi la polisi likuchukue na kukuhoji juu ya tukio hilo.
 

Kiduman

Member
Nov 12, 2018
43
125
Ulikuwepo eneo la tukio na ukamuona DED akishika Bastola? Ado Shaibu ni mkazi wa itigi?Basi itabidi jeshi la polisi likuchukue na kukuhoji juu ya tukio hilo.
Mimi nilifutalia huu mkasa ni kwel waliondan ya kanisa kwa maaana ndio mashuhuda akiwemo mzazi wa marehem wanadai kwamba DED ndio alikua shooter.
Sasa cjui viongoz wapo juu ya sheria!! Ushahid upo kanisani pale pale
 

Zumbe Mtana

JF-Expert Member
Sep 15, 2011
2,595
2,000
Hapo kanisani hawakuwepo "RAIA wenye hasira Kali"?

Wangefanya kama yule Mwenyekiti wa kule Mwanza wangetoa funzo.

Hapa " Kidevu" kashatoa maagizo mpwa anakingiwa kifua tu.

Yule DED wa Bukoba alikosea takwimu tu akaomba DT aje afafanue akatumbuliwa ila huyu anatuhumiwa mauaji kabisa lakini hadi Leo hii uteuzi wake Bado haujatenguliwa.

Alafu kila uchwao utamsikia "mniombee" Mimi kamwe sitamuombea nikiomba daima dua yangu ni "eeeh Mungu ikikupendeza utuepushe na kikombe hiki".
 

tzkwanza

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
1,369
2,000
Ulikuwepo eneo la tukio na ukamuona DED akishika Bastola? Ado Shaibu ni mkazi wa itigi?Basi itabidi jeshi la polisi likuchukue na kukuhoji juu ya tukio hilo.
Ni kazi sana kutete uovu, wenzako tulikuwa huo upande tulitetea tukaona ni kama vile tunatwanga maji kwenye kinu. Kwa kifupi kupitia MAGUFULI watanzania wataanza kuionja jehanamu hata kabla ya hukumu, huyu mtu ni laana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,080
2,000
Mimi nilifutalia huu mkasa ni kwel waliondan ya kanisa kwa maaana ndio mashuhuda akiwemo mzazi wa marehem wanadai kwamba DED ndio alikua shooter.
Sasa cjui viongoz wapo juu ya sheria!! Ushahid upo kanisani pale pale
Ulikuwepo kanisani wakati mauaji yanatokea?Je uliwahoji waliokuwa nje?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom