GE2025 Jeshi la Polisi latoa tamko kuelekea kampeni ya vyama vya siasa Agosti 28, 2025 " usiwe chanzo cha vurugu"

GE2025 Jeshi la Polisi latoa tamko kuelekea kampeni ya vyama vya siasa Agosti 28, 2025 " usiwe chanzo cha vurugu"

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Wakuu habari,

Tufuatilie live ya Jeshi la Polisi ikitoa tamko kuelekea kampeni za vyama vya siasa inayotarajiwa kuanza kesho Agosti 28, 2025


View: https://youtu.be/oMKspe2-o1Y?si=K58UWSQsgIJMBPg7

Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime: " Kesho Agosti 28, 2025 kama ilivyotangazwa na Tume huru ya Taifa Uchaguzi INEC Kampenin za wagombea za nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani zinaanza rasmi. Jeshi la Polisi Tanzania lingependa kuwajulisha wananchi na wadau wote kuwa liko tayari na limejipanga vizuri ipasavyo kuhakikisha tunaendelea kuimarisha usalama wakati wote wa kampeni na baada ya kampeni

Aidha Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wagombea na wafuasi wao na wananchi wote kwa ujumla kukumbuka kuwa jukumu la kudumisha amani, utulivu, usalama ni letu sote kama watanzania na kamwe asiwepo mmoja wetu akawa chanzo cha kukiuka sheria, kanuni na utaratibu wakati wote wa kampeni na baada ya kampeni ili kuepuka vurugu au uhalifu wa aina yoyote kutokea.

Pia tunatoa wito kila mmoja azingatie ratiba na muda wa kampeni aliyopangiwa ili kuepeuka mivutano, migongano, migogoro au uhalifu kutokea kwani hatutasita kuchukua hatua kama sheria za nchi zinavyoelekeza"
 
Virugu ilianza kwa mgombea wa CCM kunipa mwenyewe mbona hili wamelifumbia macho?
 
Hivi jeshi la Polisi Lina uwezo wa kutoa tamko ?

Siku jeshi la Polisi likiweza kutoa tamko na si maelekezo kutoka juu nitapoteza mda kuwasikiliza.
 
Back
Top Bottom