Tigershark
JF-Expert Member
- Oct 9, 2018
- 7,051
- 12,560
Nimeona trend ya nyuzi za baadhi ya wadau wakisema wapinzani hawafuati sheria ndio maana wanajikuta mikononi mwa polisi na kufunguliwa kesi za uvunjaji sheria!
Katika historia ya nchi hii,kesi nyingi ambazo polisi wamewafungulia wapinzani zikienda mahakamani Jeshi linaangukia pua!Unaweza shangaa mtu kama Lissu kuwahi kushitakiwa zaidi ya mara 10 na hata mara moja mahakama haijamkuta na hatia na kumfunga!.
Sana sana tunaona mbinu zinazotumika ni kufanya figisu watuhumiwa wasote rumande na baadae DPP kuamua kutokuwa na nia kuendelea na kesi!
Mfano mzuri ni Lema ambaye alisoteshwa rumande takribani miezi 4,na kesi ilipokuwa inaelekea kuisha kwa maana ya kutolewa hukumu,DPP akasema hana nia ya kuendelea na kesi!
Hii ni wazi wanajua wanaenda hawana kesi lakini wanaamua tu kuwatesa watuhumiwa!
Kuna mambo mawili yanayoweza kuwa sababu ya Jeshi na serikali kuangukia pua mara nyingi mahakamani:
-Jeshi kutojua sheria hivyo kuwakamata wapinzani kwa mambo ambayo hayana mashiko kisheria!
-Jeshi kutumika kisiasa na wanasiasa!
Jeshi la polisi linapaswa kujitafakari,sio unashitaki kesi 50 unashinda 1 halafu unajiona uko sawa!!!