Jeshi la Polisi kuangukia pua mara kwa mara kesi dhidi ya Wapinzani!!!

Tigershark

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
7,051
12,560
Nimeona trend ya nyuzi za baadhi ya wadau wakisema wapinzani hawafuati sheria ndio maana wanajikuta mikononi mwa polisi na kufunguliwa kesi za uvunjaji sheria!

Katika historia ya nchi hii,kesi nyingi ambazo polisi wamewafungulia wapinzani zikienda mahakamani Jeshi linaangukia pua!Unaweza shangaa mtu kama Lissu kuwahi kushitakiwa zaidi ya mara 10 na hata mara moja mahakama haijamkuta na hatia na kumfunga!.

Sana sana tunaona mbinu zinazotumika ni kufanya figisu watuhumiwa wasote rumande na baadae DPP kuamua kutokuwa na nia kuendelea na kesi!

Mfano mzuri ni Lema ambaye alisoteshwa rumande takribani miezi 4,na kesi ilipokuwa inaelekea kuisha kwa maana ya kutolewa hukumu,DPP akasema hana nia ya kuendelea na kesi!

Hii ni wazi wanajua wanaenda hawana kesi lakini wanaamua tu kuwatesa watuhumiwa!

Kuna mambo mawili yanayoweza kuwa sababu ya Jeshi na serikali kuangukia pua mara nyingi mahakamani:
-Jeshi kutojua sheria hivyo kuwakamata wapinzani kwa mambo ambayo hayana mashiko kisheria!
-Jeshi kutumika kisiasa na wanasiasa!

Jeshi la polisi linapaswa kujitafakari,sio unashitaki kesi 50 unashinda 1 halafu unajiona uko sawa!!!
 
Kwani aliyekwambia lengo huwa ni kuwafunga ni nani??

Lengo huwa ni kupotezeana muda na timing tu.bahati mbaya wapinzani huwa hawajui huu mtego nao wanajaa kizembe.
 
Kwani aliyekwambia lengo huwa ni kuwafunga ni nani??

Lengo huwa ni kupotezeana muda na timing tu.bahati mbaya wapinzani huwa hawajui huu mtego nao wanajaa kizembe.
Wakati mwingine wanakuwa wanatimiza majukumu yao,hasa hawa wabunge!
 
True sovereignty is reflected not in the power of making laws – as a legal definition would have it – but in the ability to control outcomes and respond to the fundamental needs of the people: what we term as peace, safety, and public good
 
Kufanya kazi kwa maelekezo hakumtii mtu hatiani,kutampeleka mahabusu vyombo vya sheria vikiweka maelekezo kando vikatenda kwa kufuata sheria lazima polisi washindwe kesi.
 
Kufanya kazi kwa maelekezo hakumtii mtu hatiani,kutampeleka mahabusu vyombo vya sheria vikiweka maelekezo kando vikatenda kwa kufuata sheria lazima polisi washindwe kesi.
Hapo ndipo tulipofikia!Unakuta hata jeshi lenyewe wanajua hawana kesi ila ili wasionekane hawafanyi kitu kwa wakubwa zao inabidi watambae na beat tu!
 
True sovereignty is reflected not in the power of making laws – as a legal definition would have it – but in the ability to control outcomes and respond to the fundamental needs of the people: what we term as peace, safety, and public good
I couldn't agree more!
 
Ukweli ni kwamba polisi hawajui sheria hivyo kuwakamata wapinzani kwa makosa ambayo hayana mashiko kisheria na pia kuendekeza maswala ya kuendeshwa na hisia za kisiasa huku wakinyemelea teuzi
 
Back
Top Bottom