midhali siwapendi basi ntawapinga kila wanalolifanya, wala siulizi nikifika tu nauliza nani? kafanya hili nikijibiwa ni polisi basi ntampinga hapohapo, polisi wanafanya maandamano ya kupinga unyanyasaji wa watoto kijinsia, unapinga nini? nini wao ndiyo wenye data za kila aina ya uhalifu , kupungua au kuongezeka . na aina hii ya uhalifu unatokea zaidi ndani ya jamii .haizuiliki kwa askari kufanya doria ni sisi wenyewe raia ,tuone na tujitolee kutoa taarifa polisi/ ustawi wa jamii. unyanyasaji huu ukiachwa ,unazaa aina nyingine ya uhalifu ambao utafanywa na hao watoto walionyanyaswa pindi wanapokuwa wakubwa.vitendo vya ukabaji, ukahaba, ujambazi, madawa ya kulevya na nk. hivyo ni jukumu la polisi kuelimisha umma na umma unatakiwa kupokea kwa dhati sio kejeli na kutoa mawazo ya kufurahisha genge, jamii ni yetu sote tu ,waathirika.