Jeshi la Polisi Dar kuandamana Leo...

Jeshi la Polisi Dar kuandamana Leo...

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
16,202
Reaction score
8,781
Askari wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar Es salaam leo hii watafanya maandamano makubwa na ya kihistoria kupinga Unyanyasaji wa Kijinsia kwa watoto nchini

Source: Magazeti RFA.

My take.
Walitakiwa waanze kwa kuandamana kupinga mauaji ya raia wasio na hatia.
 
Nilistuka nikasema nani atawamwagia maji ya pilipili? Haya maandamano mema, ile shopping mall ya oysterbay polisi ingekuwa imeshakamilika wangejisuuza na lunch baada ya maandamano kwa kutumia rushwa wanazopewa na wanaume waliowekwa ndani kwa ubakaji na kupiga wake zao.
 
Huu utamaduni wa kila mtu kulalamika nchini mwetu umeshika kasi.
Kama jeshi la polisi nao wanaandamanj wanaleta picha gani?
Wao ni watendaji na wangeonyesha hilo kwa kushughulikia kwa uharaka uchunguzi wa kesi lukuki zilizojaa vituoni mwao!

Tafsiri yangu ni kwamba kuandamana ni kukiri udhaifu.
 
nilipata mawazo kama yako, nani atarusha vitu vyenye ncha kali? Kumbe maandamano ya amani sorre kumbe maandamano ya kwao loh, posho ipo lakini?
 
Hii ya leo kali, siku si nyingi tutaskia wameandamana mawaziri kupinga ugumu wa maisha kwa watanzania, yaani kweli hii ndo Tanzania sarakasi kila kona
 
nilipata mawazo kama yako, nani atarusha vitu vyenye ncha kali? Kumbe maandamano ya amani sorre kumbe maandamano ya kwao loh, posho ipo lakini?

Na je sheria ya vyombo vya ulinzi inaruhusu maandamano?
 
Hii ya leo kali, siku si nyingi tutaskia wameandamana mawaziri kupinga ugumu wa maisha kwa watanzania, yaani kweli hii ndo Tanzania sarakasi kila kona
Pata picha JWTz watakapoamua kuandamana!
Patakalika nchini kweli?
 
Wakiingia tu barabarani tunawapiga mawe shwaini wale!
 
Na je sheria ya vyombo vya ulinzi inaruhusu maandamano?

Kuna sheria bongo mkuu, nimeanza kuamini ile kauli ya jamaa mmoja kuwa wabongo wengi wanaingia maofisini wakiwa wamekunywa viroba. Haziwezi kuwa akili timamu hizi
 
Polisi wana nguvu na mamlaka ya kuwasaka, kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria wote wanaoshiriki kwenye vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto, kuingia barabarani kuandamana ni kupoteza tu muda ambao ungetumika kutekeleza hayo majukumu yao.
 
jamani hebu changieni point za msingi, kwani huo unyanyasaji wanafanyiwa watoto wao? police ni kwa manufaa ya umma kumbukeni hao mnaowatusi na kuwakejeli kama sio baba zenu ni mama zenu au ndugu zenu wa karibu. changieni kwa manufaa ya umma.
 
natamani siku askari wa JWTZ wajewaandamane wapinge kutumika kisiasa kuwanufaisha wakina pinda na kikwete!!
 
Kuna sheria bongo mkuu, nimeanza kuamini ile kauli ya jamaa mmoja kuwa wabongo wengi wanaingia maofisini wakiwa wamekunywa viroba. Haziwezi kuwa akili timamu hizi
Mkuu,
Hiyo kauli mimi sikuipata, ninachokumbuka ni kwamba Naibu spika Job Ndugai alisema kuwa wabunge wengi wanaingia bungeni session ya mchana wakiwa wamelewa pombe kali na sgara.
 
midhali siwapendi basi ntawapinga kila wanalolifanya, wala siulizi nikifika tu nauliza nani? kafanya hili nikijibiwa ni polisi basi ntampinga hapohapo, polisi wanafanya maandamano ya kupinga unyanyasaji wa watoto kijinsia, unapinga nini? nini wao ndiyo wenye data za kila aina ya uhalifu , kupungua au kuongezeka . na aina hii ya uhalifu unatokea zaidi ndani ya jamii .haizuiliki kwa askari kufanya doria ni sisi wenyewe raia ,tuone na tujitolee kutoa taarifa polisi/ ustawi wa jamii. unyanyasaji huu ukiachwa ,unazaa aina nyingine ya uhalifu ambao utafanywa na hao watoto walionyanyaswa pindi wanapokuwa wakubwa.vitendo vya ukabaji, ukahaba, ujambazi, madawa ya kulevya na nk. hivyo ni jukumu la polisi kuelimisha umma na umma unatakiwa kupokea kwa dhati sio kejeli na kutoa mawazo ya kufurahisha genge, jamii ni yetu sote tu ,waathirika.
 
Wanaandamana kwani wameshahakikishiwa ulinzi? Au Jeiwii itahusika?
 
Kibali cha kuandamana wamepata kwa nani?Hakuna taarifa za kiintelijensia za kuyazuia hayo maandamano?
 
Back
Top Bottom