Jeshi la China lachangia amani na usalama barani Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111285191162.jpg


Tarehe 1 Agosti ni Siku ya Kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China. Katika miaka mingi iliyopita, jeshi hilo limeshiriki katika masuala ya usalama ya Afrika kwa hatua madhubuti, na kuchangia amani na usalama barani humo.

China ni nchi ya pili duniani kwa mchango wa fedha kwa ajili ya operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, na pia inapeleka walinzi wenzi zaidi wa amani kati ya wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja huo. Tangu ianze kushiriki katika operesheni za ulinzi wa amani, China imetuma zaidi ya askari 40,000 katika operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa, ambapo zaidi ya asilimia 80 wametumwa katika nchi za Afrika, zikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Liberia, Sudan, Sudan Kusini, Mali, Libya na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kwa sasa, zaidi ya wanajeshi 2,000 wa China wanalinda amani barani Afrika, ambao wanachukua zaidi ya asilimia 75 ya walinda amani wote wa Umoja wa Mataifa barani humo. Wametoa mchango mkubwa katika utatuzi wa mizozo, kudumisha usalama na utulivu na kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi za Afrika.

Mbali na operesheni za ulinzi wa amani, tangu mwezi Desemba mwaka 2008, China imekuwa ikituma mara kwa mara manowari ili kulinda meli zinazopita katika Ghuba ya Aden barani Afrika. Katika miaka 14 iliyopita, jeshi la wanamaji la China limetuma vikundi 41 vya manowari, na kutoa ulinzi kwa zaidi ya meli 7,000 zilizopita ghuba hiyo.

Tangu kutokea kwa janga la COVID-19, jeshi la China limechukua hatua madhubuti kushirikiana na majeshi ya Afrika kukabiliana na janga hilo. Jeshi hilo limetoa dozi za chanjo ya COVID-19 kwa wanajeshi wa zaidi ya nchi 10 za Afrika, zikiwemo Sudan, Ethiopia, Tunisia, Guinea, Msumbiji na Mauritania. Aidha, jeshi la China pia limetoa msaada wa nyenzo nyingine mbalimbali za kukabiliana na janga hilo, kutuma vikundi vya madaktari wa kijeshi, na kufanya mikutano ya video wa kubadilishana uzoefu katika kuzuia na kudhibiti janga hilo kwa nchi za Afrika.

Hivi karibuni, kongamano la 2 la amani na usalama kati ya China na Afrika lilifanyika kwa njia ya video. Katika barua yake ya pongezi kwa kongamano hilo, Rais Xi Jinping wa China alieleza kwamba anatilia maanani sana ushirikiano wa amani na usalama kati ya China na Afrika, na kupendekeza kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye hatma ya pamoja katika shughuli za amani na usalama. Kama ndugu wa watu wa Afrika, Jeshi la Ukombozi la Watu wa China litachangia zaidi usalama na amani barani Afrika.
 
Mkishiba mnasema Marekan anachafua Amani afrika kwa kuitumia Umoja wa Afrika wakati huo huo mnasema 75% ya jeshi la umoja wa mataifa ni wachina
 
mkishiba mnasema Marekan anachafua Amani afrika kwa kuitumia Umoja wa Afrika wakati huo huo mnasema 75% ya jeshi la umoja wa mataifa ni wachina
Ya kwamba asilimia 75 ni wachina, watu wakishiba makande.....! Ni hatari.
 
China hana lolote ni wachumia tumbo tu hao. Hakuna watu wa hovyo kama wachina tena nchi yoyote yenye kushirikiana nao lazima tu iwe maskini. Bure kabisa.
 
Back
Top Bottom