Jerry Silaa usijisahau Kuna maisha baada ya 2025

Waziri wa madini

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
379
465
Mbunge wa Jimbo la ukonga Jerry silaa kumbuka ahadi zako ulizozitoa wakati wa kampeni,kumbuka jinsi ulivyopigana na kupiganiwa ili kupata ubunge wa ukonga. Kumbuka wananchi wa ukonga wanakutazama na wanasubiria utekelezaji wa ahadi zako.

Tangia uapishwe kuwa mbunge hujawahi kuitisha mkutano wowote katika Jimbo lako kujadili changamoto zinazowakabili na jinsi ya kuzitatua,hujawahi kuonekana hata siku moja bungeni ukichangia hoja zinazo husiana na kero pamoja na changamoto za wakazi wa Jimbo lako la ukonga.

Ushauri wangu kwako bado mapema sana ila tunakukumbusha kuwa Jimbo unaloliongoza ndio linaongoza kwa changamoto ya miundombinu kuliko sehemu yoyote ya mkoa wa Dar Es Salam,Jimbo unaloliongoza ndio linaongoza kwa shida ya maji japokuwa mradi wa maji umezinduliwa lakini kunaurasimu mkubwa kwenye usambazaji wa maji hayo,kumbuka Kuna ahadi nyingi ulizitoa wakati wa kampeni.

Kuwakimbia wapiga kura wako mapema hivi unajiweka hatarini Sana kuja kutetea nafasi yako ya ubunge.

Mheshimiwa Silaa tumekuona unachangia hoja za kutetea ndege za Magufuli umefanya jambo zuri kumtetea mpendwa wetu na kuchambua ukweli kuhusu ATCL lakini kumbuka Kuna kazi uliyotumwa na wakazi wa ukonga mbona huifanyi kwanini huwasemei?

Nakuomba hebu siku moja jaribu upite barabara ya majohe ,viwege hadi mbondole uone maisha ya wakazi wa ukonga yalivyo hatarini barabara haipitiki kabisaa mbaya mbovuu ,mbunge upo na barabara ipo katika ilani ya uchaguzi 2020-2025 lakini mbunge umekaa kimya tu barabara inamashimo haipitiki .

Mwisho kumbuka Kura za wanaukonga ulizopewa kuwa na utu na ukumbuke ulipotoka.
 
Achani kumtsha, Kwani lazma 2025 ashinde??
Mzee ashinde asishinde Jerry bado kijana mdogo Sana na fursa hii ya ubunge ukonga naamini ni katika ndoto zake za muda mrefu kwakuwa ameipata fursa hii ajitahidi kufanya kweli ili azidi kuaminiwa na kujijenga kisiasa.
 
Hata huyu wa sasa siyo mbunge? Je Waitara?
Waitara hamna kitu yule ndio maana alikimbilia kwao.Dunian Kuna watu ni opturnist na Wana bahati hatari mmoja wapo ni Waitara alishinda kipindi Kile sababu kubwa ilikuwa nguvu ya ukawa ndani ya dar mzee akaangalia ukonga Kuna idad kubwa ya watu wa Kanda ya kwao na kweli kabila likambeba.Baada ya kuharibu ukonga akakimbilia kwao na kwa bahati hiyohiyo akakutana na Ile operation Magufuli naona Ccm wakaona yeye ndio karata pekee ya kumshinda Heche.
 
Lakini Jerry Slaa han hata miezi 6 tangu awe mbunge. Pia hili ndiyo bunge la kwanza la bajeti anashiriki hauoni mnamuonea kumhukumu mapema hivi?
 
Hayo mkuu ndio majungu yenyewe kiukweli sio haki na busara kumhukumu mtu kwa kipindi kifupi hivi ts lyk chuki binafsi
 
Hakuna mbunge wa CCM
anaye tegemea kura yako kuingia bungeni bro,,
Fanya kazi acha majungu
 
Mbunge wa Jimbo la ukonga Jerry silaa kumbuka ahadi zako ulizozitoa wakati wa kampeni,kumbuka jinsi ulivyopigana na kupiganiwa ili kupata ubunge wa ukonga.kumbuka wananchi wa ukonga wanakutazama na wanasubiria utekelezaji wa ahadi zako.
Tangia uapishwe kuwa mbunge hujawahi kuitisha mkutano wowote katika Jimbo lako kujadili changamoto zinazowakabili na jinsi ya kuzitatua,hujawahi kuonekana hata siku moja bungeni ukichangia hoja zinazo husiana na kero pamoja na changamoto za wakazi wa Jimbo lako la ukonga.
Ushauri wangu kwako bado mapema Sana ila tunakukumbusha kuwa Jimbo unaloliongoza ndio linaongoza kwa changamoto ya miundombinu kuliko sehemu yoyote ya mkoa wa daressalam,Jimbo unaloliongoza ndio linaongoza kwa shida ya maji japokuwa mradi wa maji umezinduliwa lakini kunaurasimu mkubwa kwenye usambazaji wa maji hayo,kumbuka Kuna ahadi nyingi ulizitoa wakati wa kampeni.
Kuwakimbia wapiga kura wako mapema hivi unajiweka hatarini Sana kuja kutetea nafasi yako ya ubunge.
Mheshimiwa Silaa tumekuona unachangia hoja za kutetea ndege za Magufuli umefanya jambo zuri kumtetea mpendwa wetu na kuchambua ukweli kuhusu Atcl lakini kumbuka Kuna kazi uliyotumwa na wakazi wa ukonga mbona huifanyi kwanini huwasemei?
Nakuomba hebu siku moja jaribu upite barabara ya majohe ,viwege hadi mbondole uone maisha ya wakazi wa ukonga yalivyo hatarini barabara haipitiki kabisaa mbaya mbovuu ,mbunge upo na barabara ipo katika ilani ya uchaguzi 2020-2025 lakini mbunge umekaa kimya tu barabara inamashimo haipitiki .
Mwisho kumbuka Kura za wanaukonga ulizopewa kuwa na utu na ukumbuke ulipotoka.

Kulikua na maisha pia kabla ya 2020
Msimpangie Jerry awaze mnachotaka nyie
 
Atakuja na hela. Atawagawia.
Kisha mtampIgania kama kawaida.
 
Back
Top Bottom