Ili Mradi amepitishwa na CCM, umpende usimpende, umpigie kura usimpigie kura, achangie hoja Bungeni asichangie, haisadii na wala haijalishi, chama chake cha CCM kikiamua kumpitisha ndio imetoka hiyo, hakuna wa kumzuia na ataendelea kuwa Mbunge. Kama umegundua miaka ya Hivi karibuni, wabunge wengi wameonesha waziwazi kutojali na kutowajibika kwa wananchi wa majimbo yao kwa dhana iliyo wazi kwamba SIO WAO waliowaweka hapo bali ni CCM, hivyo wengi wamekuwa si watiifu kwa wananchi bali kwa chama chao au kiongozi wa chama chao. Ni ukweli mchungu kuumeza