Jerry Silaa: Magufuli acha ubabe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jerry Silaa: Magufuli acha ubabe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, Mar 7, 2012.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,514
  Trophy Points: 280
  SIKU moja baada ya Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli kuamuru mabango yaondolewe barabarani, Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa amemtaka waziri huyo kuacha ubabe katika utekelezaji wa majukumu yake badala yake atumie vikao rasmi kutoa matamko yake.

  Juzi wakati akizindua kituo cha daladala Mbezi, Dk Magufuli alitoa siku tano kwa wakala wa barabara (Tanroads) Mkoa wa Dar es Salaam kuondoa wafanyabiashara na mabango yote yaliyojengwa pembezoni mwa barabara ili kukabiliana na msongamano.

  Akizungumza ofisini kwake jana, Silaa alisema viko vikao vya bodi ya barabara na vya kamati ya ushauri ya mkoa ambavyo vyote vinaongozwa na mkuu wa mkoa na kwamba waziri huyo anaweza kuvitumia kupeleka hoja zake na kujadiliwa.

  "Nchi hii siyo ya kwake na lazima atambue kuwa halmashauri zote ziko kisheria hivyo atumie vikao rasmi kutoa maagizo yake,"alisema Silaa. Alisema waziri huyo anatumia sheria ya barabara ya mwaka 2007 na kwamba kabla ya kutungwa kwa sheria hiyo kulikuwapo na sheria nyingine ambazo hadi leo bado zinatumika hivyo anatakiwa aziheshimu.

  Alisema miongoni mwa walipa kodi wakubwa nchini ni wenye mabango hivyo kutaka kuyaondoa ni sawa na kuhujumu maendeleo.Kwa mujibu wa meya huyo fedha za mabango zimekuwa zikitumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo kama shule, barabara na hospitali.

  Alisema watu wenye mabango wana mikataba halali na halmashauri na wanaotangaza kwenye mabango hayo wana mikataba halali na wenye mabango hayo na kwamba kuyaondoa ni kusababisha usumbufu usiokuwa wa lazima katika mikataba hiyo.

  Kuhusu suala la kutochaji ushuru katika kituo cha Mbezi, Meya huyo alisema suala hilo siyo sahihi kwani kuna gharama mbalimbali za uendeshaji ambazo zitatakiwa kulipwa.

  Kwa mujibu wa meya huyo gharama hizo ni walinzi na uendeshaji wa choo ambao alisema zinaweza kulipwa na ushuru utakaokuwa unatozwa.

  Katika hatua nyingine, halmashauri hiyo imesema itawashtaki wamiliki wa mabango ya biashara walioshindwa kulipa ushuru ambao unafikia Sh984 milioni. Silaa alisema karibu kampuni 20 zinadaiwa ushuru wa mabango na halmashauri hiyo zikiwamo kampuni ya simu za mkononi, kampuni ya vinywaji na kampuni zinazohusika kuweka mabango.

  Alisema wameamua kuwashtaki baada ya kuzungushwa kwa muda mrefu na wamiliki hao ambao kila wanapofuatwa wamekuwa wakidai kuwa hawana fedha.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,514
  Trophy Points: 280
  Huyu Meya najua yuko hapa JF ila ana akili fupi na Magufuli ana hoja ya msingi..

  Watu wenyewe walioweka mabango hawalipi kwa sababu serikali na wanaohusika ni legelege ,, Sasa kwa nini barabara isiongezwe ili kupunguza foleni.. Huyu jamaa hajui kuwa serikali inapoteza mapato kiasi gani na nguvu kazi kwa sababu ya watu kuishi barabarani kwenye foleni kubwa..eti mabango yanaiingizia serikali pesa kwa hiyo barabara zisipanuliwe...
  BIG JOKER....
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,514
  Trophy Points: 280
  hapo je?
   
 4. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,840
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Huyu Meya ni Hamnazo Kabisa!! Ustaarabu wa jiji la Dar Umepotea!!

  Jiji Limekuwa kama DANGULO! Haoni Hilo? Hata mtu ambaye anamsemea Yeye aliyeshindwa majukumu yake kama meya bado anafungua mdomo Kumkosoa!! What the Hell of this so called Meya!!! Kwa jiji la Dar Hali imekuwa Mbaya!! Unafika Manzese Unakuta Foleni inaanzia Maeneo ya Kagera Kisa Watu wamepanga Biashara Katikati ya barabara MANZESE!! Je Hakuna Mamlaka inayoweza kuwapangia hawa watu maeneo na ustaarabu ukawepo?

  Sasa huyu meya anaongea kama hayupo Dar es Salaam? Nenda ubungo Mataa masoko hadi kwenye all road reserve hali hii inahatarisha zaidi maisha ya wauzaji na wanunuzi!! Huyu meya hana hata mshipa wa kuona hii ni Hatari na Kero? Kwa nini asijipange na kuandaa mazingira ya ustaarabu ili tukamuona angalau kuna ambacho anakifanya!! City center ambako ndio Ilala Kwenda kariakoo na usafiri Binafsi ni kero Kuliko Kuingia Lango la Jehanamu!!

  Ni nini huyu Meya amefanya kuboresha? Meya Kijana Lakini Hamnazo!! Muheshimiwa Magufulu Mpuuze Huyu Mp*****zi Na Chapa mwendo labda Hata utatutoa kwenye Hii Kero Kuu ya jiji la Dar!! Kariakoo Kila mahali watu wamepaki Magari Hovyo Hakuna official Parking Hakuna maeneo ya Biashara!! Haya Mheshimiwa raisi amejitahidi Hadi Limejengwa MACHINGA COMPLEX!! Haya meya jitahidi vijana wa kariakoo wahamie kwenye hili soko!! Umeshindwa umekaa kubadilisha suti tuu!! so what?? To Hell!!
   
 5. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kweli siasa mchezo mchafu ccm hao hao wanawakandamiza wananchi nani hao hao wanajifanya kuwatetea, sidhani hapa kama kuna jipya kwani lao ni moja
   
 6. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Huyu Meya nadhani inafaa aanze kusoma alama za nyakati,kumbe watu wengine ukiwaona unaona wana maana kumbe kichwani hamna kitu,anadhani Magufuli alikuwa anafanya siasa kumbe mwenzake anafanya utekelezaji wa majukumu yake kama waziri,yeye kakazania mabango tu bila kuangalia kwa upana wa tatizo lenyewe,sitoshangaa kuona kuwa huyu Meya ana maslahi binafsi katika biashara ya mabango.
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,328
  Trophy Points: 280
  Wajameni huyu meya huyu namfahamu, kiukweli ni kati ya hazina kubwa chache za vichwa vya ukweli CCM ilivyonavyo japo nakiri kwenye suala hili ameshindwa kujieleza vyema.

  Sehemu yuko right na sehemu yuko wrong na Magufuli yuko right kwa asilimia 100%.

  Ni kweli Halmashauri zina mamlaka yake ambayo hayapaswi kuingiliwa na serikali kuu ikiwemo mabunge yake (mabaraza ya madiwani) ambayo yanamamlaka ya kisheria kujitungia bylaws zake. Hivyo mabango yapo kisheria na yana mikataba halali na halmashauri husika, hivyo meya yuko right, mabango hayo hayawezi kungolewa kwa agizo la siku 7 kama Magufuli alivyogiza!.

  Alichofanya Magufuli ni kusisitiza matakwa ya kisheria ya utekelezaji wa sheria mpya ya road reserve ya mwaka 2007 ambayo inakwenda kinyume cha by laws za halmashauri, hivyo licha ya sheria hiyo kupitishwa, halmashauri zilipaswa kutengua bylaws zake na kuzioanisha na sheria hiyo mpya, kitu ambacho hakikufanyika na badala yake Halmashauri zimeendelea kurenew mikataba ya mabango kwa sheria za zamani ili kuendelea kuvuna pesa nene!.

  Hata hivyo ukweli wa mambo, uinguliaji mkubwa wa road reserve sio mabango, ni vibanda vya biashara na wafanya biashara ndogondogo ambao hawako covered kwenye by laws za halmashauri.

  Alichotakiwa kusema huyu meya ni kuamuru utekelezaji wa kuwaondoa hao wafanya biashara kwanza na kusema mchakato wa kuyaondoa mabango ufuate matwakwa ya kisheria ili halmashauri zisiingie kwenye migogoro ya kisheria na kesi za madai kufidia hasara ya kuvunja mabango ya watu yaliyokuwepo kabla ya sheria hiyo kupitishwa!.
   
 8. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Mkuu kweli intention yako ilikuwa ni kusema huyu ni kichwa??
  Mbona sasa tena kama vile wewe unaelekea kum-devalue??
   
 9. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,840
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Pasco Huwa Nakwaminia na Nitaendelea Kufanya Hivyo!! Ila kwani Hizi By laws zinasema kusiwe na Utaratibu wa kufanya biashara? Kusiwe na ustaarabu kwenye Jiji pekee Kubwa Tanzania!! Bila shaka By laws Nyingi zinataka jiji liwe katika ustaarabu Fulani!! sasa Huyu Meya Anasimamia nini? Mapato ya Mabango bila Ustaarabu?
   
 10. g

  greenstar JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  bwana mdogo zuzu sana,anaharibu sifa ya vijana kushika hatamu kwa kuendekeza ujinga badala ya kufanya kazi.Watu tunakaa kwenye foleni zaidi ya masaa 3 lakini hilo halioni? .....natamani avuliwe gamba mapema kabla halijakomaa
   
 11. Gwandalized

  Gwandalized JF-Expert Member

  #11
  Mar 7, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  IN magufuli we trust,hichi kichwa sijui huko kinafanya nini
   
 12. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mji wa Dar es Salaam ni kama mji wa Mbuzi; kila mahali ni choo, kila mahali ni hotel, kila mahari ni sehemu ya biashara, kila mahari ni parking, kila mahari kuna gereji, n.k. Bahati mbaya huu ndo mji mkuu wa kibiashara wa nchi hii. Gharama tunayoliingiza taifa hili, kutokana na uzembe huu wa kupanga mji mkuu, ni kubwa mno kuliko hivyo vifedha mbuzi vya matangazo wanavyopata Manispaa. Meya hajaangalia msitu anaangalia mti.

  Kuhusu by-laws za manispaa. Mimi si mwanasheria, ila najua kuwa katika nchi kuna Katiba, Sheria, na vi-sheria (ndo hizi by laws). Kwa kawaida ikiwepo sheria ambayo inapingana na katiba inatakiwa ibadirishwe ili iendane na matakwa ya katiba vinginevyo sheria hiyo inakuwa si halali. Vile vile hizi by-laws inatakiwa ziwe zinabadirishwa ili kuendana na sheria mama za nchi. Zisipobadirishwa zinakuwa sheria mfu na kuendelea kuzitumia ni uzumbukuku.

  Kama sheria ya bara bara imetungwa mwaka 2007, kwa nini hadi leo manispaa hawajarekebisha by-laws zao kuendana na sheria mama? Au ndo tunaanza kutengeneza vi-falme ndani ya nchi? Na kwa nini meya anapuliza vuvuzela kwa nguvu hivyo wakati yaliyozungumzwa ni maamuzi ya serikali kuu? Naamini hapa kuna tatizo.

  Hali ni mbaya sana kwa huu mji wa Dar na kadri siku zinavyoenda hali inazidi kuwa mbaya. Upangaji wa mji haupo na mambo yanafanyika kiholela. Na wanaosababisha upangaji holela ni hawa wanaojiita serikali za mitaa sababu ya ubabaishaji mkubwa uliojaa huko. Hatuwezi kuendelea hivi hivi hadi milele.
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Pasco, hapo kwenye red natofautiana na wewe kabisa. Huyo dogo ni mzigo kwa nchi hii. Hana la maana zaidi ya kutetea mabango kwa sababu mabango ni ATM yake binafsi. Tumekuwa tunasikia kelele za kutaka vijana wapewe nafasi za uongozi then tunapata aina ya hii ya Jerry Silaa! Kafanya nini tangu awe meya wa Ilala zaidi ya kuuza sura kule michuzi blog? kasafisha mitaro? kaweka taa barabarani? kasaidia usafiri kwa wanafunzi ndani ya manispaa yake? Kaondoa foleni ya magari Ilala? Amefanya nini mpaka tuseme meya ni hazina?

  Na kwa nini anawashwa sana kila issue ya mabango inapotajwa? Ukitaka kusikia sauti (ya juu kabisa) ya huyu Jerry Silaa basi sema mabango yaondolewe! Jiji limekuwa kama x'mas tree kwa utitiri wa mabango, ni uchafu kabisa. Lakini meya yuko radhi watu waendelee kusota barabarani kwa msongamano wa magari ili mradi mabango ya wafadhili wake yapo! Dar es Salaam ni moja ya miji inayokuwa kwa kasi sana barani Africa, yeye kama meya anafanya nini ili kuweka miundo mbinu itakayoendana na ukuaji huo? Kwa kuweka mabango?

  Katiba mpya inakuja, hivi vyeo vya kupeana mezani kama meya vifutwe.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe mkuu. Jerry Silaa anajibu gani, kwa nini hajabadilisha sheria ndogo ili iendane na sheria kuu? Anaicha hiyo sheria kwa manufaa ya nini? Halafu alivyo kichwa maji mabango yakitajwa anakuwa wa kwanza kurukia hiyo sheria mbuzi. Hakuna kitu kinachoniudhi kama mtu kupuuza juhudi za kuondoa foleni Dar. Ni mateso matupu barabarani.
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,460
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Sahihisho......huyu anaitwa Silaa na sio SLAA....:lol::eyebrows::embarassed2:
   
 16. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,840
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Pia Kuna hii Miradi Mbuzi (Uchwara) Inayoendeshwa na Manispaa!! Mfano Huu Mradi unaoendelea wa uwekaji wa Vitofali Vya waenda kwa miguu Katikati ya Jiji, Say Ilala Maeneo ya posta!! Huu ni Ubadhirifu wa Hali ya Juu!! Kazi inafanyika bila Mpangilio wowote!!

  Jana nimepita maeneo ya British Library Nikamuuliza Msimizi wa kazi Pale, Ndugu yangu hii kazi Unayofanya unamichoro yoyote ambayo inazingatiwa!! Aliloniambia Karibu Nizimie!! Alinieleza Ndugu Yangu Tunafanya ili Mkono Uende Kinywani Kwani Michoro ina umuhimu gani?

  Hapo hapo nikagundua huu ni Ufujaji wa hali ya juu wa Kodi Zetu!

  Mimi ninachopendekeza katika Halmashauri Zetu ni Bora kila kitu wanachotegemea Kufanya Kizingatie Tafiti za Kitaalamu ili Malengo yanayotegemewa yafikiwe badala ya kuharibu Hela za Kodi Zetu Bure Kabisa!

  Katikati ya jiji kwa sasa kunahitaji Mpangilio Mpya ikiwa ni pamoja na kuondoa miti iliyozeeka na kupanda mingine ili kuondoa athari za watu Kuangukiwa na miti na kusababisha madhara makubwa.

  Then Mipangilio Mipya ifanywe na Vile Vitofali Vijengwe kwa Mpangilio Maalumu!! Vinginevyo kinachofanyika ni Ubadhirifu Mkubwa Wa hela za walipakodi.

  Meya kama pasco alivyokufagilia Fanya chochote hapo tukuone upo Makini!! Sio Kukaa na kulumbana na Wenzio wanaojaribu Kwenye Haya Mazingira Magumu!!
   
 17. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #17
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Pasco,

  Naona umemvalue sana jamaa na then mwishoni mwa thread yako ukadevalue jamaa yako Slaa

  Nikirudi kwenye mada inawezekana Magufuli yuko right na meya naue ana sehem yake yuko right; Sheria ya barabara ilitungwa na inagovern barabara zote ambazo zinasimamiwa na mamlaka inayohusika na barabara Sheria imeweka na kupanga aina mbalimbali za barabara na ukubwa wake na nini umbali kutoka makzi au biashara yoyote magufuli yuko sawa kusimamia sheria mama inayotamka ni kitu gani kinapaswa au hakipaswi kuwepo kwenye barabara husika.

  Meya kwa upande wake anasimamia na ana halmashauri yake ya Minispaa ya Ilala ambayo nayo kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa ina mamlaka yake ya kutunga bylaws ambazo zinatawala masuala yote ya uendeshaji wa manispaa yake na masuala ya biashara na utendaji wa kila siku wa Manispaa.

  Kwa mujibu wa sheria inapotungwa sheria mama kwa mfano hiyo sheria ya barabara mamlaka za miji au manispaa au jiji zinatakiwa zihakikishe kuwa by laws zao haziendi kinyume na sheria mama na kama kuna kipengele chochote ambacho kinapingana na sheria mama jiji au manispaa au mamlaka za miji zinatakiwa kuziorekebisha sheria zao hatraka sana.

  Kinachofanyika hapa inaonekana toka sheria hii inayohusiana na barabara itungwe bado mamlaka za majiji au manispaa kama ya Jerry hawajarekebisha bylaws zao hapo ni kwamba zinaenda kinyume na sheria mama na hapo kisheria ni kwamba by laws yoyote inayopingana na sheria mama ni void
   
 18. bht

  bht JF-Expert Member

  #18
  Mar 7, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Pasco sheria ya road reserve inaenda kinyume na by-laws za Halmashauri?

  By-laws za halmaishauri ndizo zinazotakiwa kubadilishwa kuendana na sheria husika na kwa hivyo hizo ndo zibadilishwe ziendane na sheria.
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,514
  Trophy Points: 280
  big joke again ..mkuu ni kweli inasikitisha yaani tunaenda enda tu hatujui tunaenda wapi ..nchi haina mwenyewe ..hili linaonyesha wazi kabisa kuwa hakuna mwenye maamuzi wala vision. watu wanaangalia hio calling mkono kwenda kimyani sijui kinywani
   
 20. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #20
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,840
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Tutatunga Hata sheria Mia Tano na Ushee Ila kama Hamna Msimamiaji Hakuna chochote Tutakachoambulia!! Suala sio Kutunga sheria!! Hapa suala ni nani anayeweza Kusimamia hata Hiyo Sheria mbovu Iliyopo? Jibu Ni hakuna!! Sasa kwa nini tupoteze Muda kutunga hizo sheria?
   
Loading...