Jerry Muro kortini tena

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
47,286
Points
2,000

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
47,286 2,000
Jerry Muro kortini tena *Kesi aliyoshinda kusikilizwa upya Mahakama Kuu


Na Rehema Mohamed

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo inatarajiwa
kuanza kusikiliza rufaa ya Serikali dhidi ya aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC1), Bw. Jerry Muro na wenzake.

Kwa mujibu wa wakili wa utetezi, Bw. Richard Rweyongeza, alisema rufaa hiyo inatarajiwa kusikilizwa mbele ya Jaji Dkt.
Fauz Twaib wa Mahakama hiyo.

Katika rufaa hiyo, upande wa Serikali unapinga hukumu iliyotolewa na Hakimu Frank Moshi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, ambayo iliwaachia huru Bw. Muro na wenzake
kwa madai kuwa, upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.

Hakimu Moshi alidai vidhibiti vilivyofikishwa mbele ya Mahakama hiyo na upande wa mashtaka vilikuwa haviendani na kesi hiyo.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo walikuwa Bw. Edmund Kapama na Bw. Deogratius Mugasa, ambao kwa mara ya kwanza
walifikishwa Mahakamani Februari 5,2011.

Mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili ni kula njama na kuomba rushwa ya sh. milioni 10 kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, Bw.
Michael Wage.

Wakati shauri hilo likisikilizwa upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi saba pamoja na vielelezo, ambapo inadaiwa kuwa, Januari 28,2011 jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao walikula
njama ya kutenda kosa la kuomba rushwa.

Katika shtaka la pili ilidaiwa Januari 29,2011, kwenye Hoteli ya
Sea Cliff, Dar es Salaam, washtakiwa hao waliomba rushwa ya sh. milioni 10 kutoka kwa Bw. Wage.

Ilidaiwa kuwa, washitakiwa hao waliomba rushwa ili kuzuia habari inayoelezea tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma inayomuhusu Bw. Wage akiwa Mhasibu wa halmashauri hiyo isirushwe katika televisheni ya TBC1.

Bw. Muro alikamatwa Januari 31,2011 baada kwa tuhuma hizo na kushikiliwa kwa saa saba kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Kati, Dar es salaam na baadaye kuachiwa.

Washtakiwa hao walifikishwa mahamani na kusomewa mashitaka yao na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali, Bw. Boniface Stanslaus, akisaidiana na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Bw.
Ben Lincolin, mbele ya Hakimu Mkazi, Bw. Gabriel Mirumbe.

Baadaye washtakiwa wote waliachiwa kwa dhamana baada ya kusaini hati ya dhamana ya sh. milioni tano kila mmoja na kuwa
na wadhamini wawili wa kuaminika hivyo kuendelea kufika mahakamani wakati kesi ikiendelea.

Juni 2011, upelelezi wa kesi hiyo ulikamilika ambapo upande wa mashitaka ulidai utakuwa na mashahidi 11, wakati Bw. Wage akiwa mmoja wa mashahidi hao.
 

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2011
Messages
5,106
Points
2,000

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Joined Jan 8, 2011
5,106 2,000
Watu wanaacha kushughulikia mambo ya msingi wanapambana na mtu kisha kawanyima kula isiyo halali. Hapa sijui wanataka nini tena
 

Rosena

Member
Joined
Sep 11, 2012
Messages
51
Points
0

Rosena

Member
Joined Sep 11, 2012
51 0
Aibu kubwa sana kwa Taifa lenye shida za wananchi lukuki kushindana na kijana mdogo kisa kawaanika uozo wa polisi na rushwa. Serikali ya mahawala na mashemeji ina taabu kwelikweli.
 

Mjanga

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2011
Messages
1,244
Points
1,225

Mjanga

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2011
1,244 1,225
Hivi ni wakati gani (katika mazingira gani) mtu anaweza kuomba kwenda Uhamishoni kwa sababu za usalama wa maisha yake??
 

Osia

Member
Joined
Sep 1, 2012
Messages
57
Points
0

Osia

Member
Joined Sep 1, 2012
57 0
Aibu kubwa sana kwa Taifa lenye shida za wananchi lukuki kushindana na kijana mdogo kisa kawaanika uozo wa polisi na rushwa. Serikali ya mahawala na mashemeji ina taabu kwelikweli.
Ni kweli kbs Rosena, ni aibu. Tuna matatizo mengi na changamoto nyingi mno hapa kwetu; Elimi, Kilimo, Miundombinu, Afya, na mengine mengi tu. Kwa upuuzi huu waufanyao wanatupotezea fedha nyingi ambazo kimsingi tungeweza zielekeza kwenye haya kiliko visasi tena baina ya watu na watu tena kwa mtu anayekosoa pale tulipokosea?!!!
Nchi ya aibu sana hii
 

katalina

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2012
Messages
264
Points
0

katalina

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2012
264 0
Mimi nadhani suala si kaonewa, au hili si la muhimu kama mdau mmoja alivyosema. Hili ni suala la RUSHWA tatizo kubwa hapa nchini. Kama anaonewa hata na mimi nampa pole lakini kama ni kweli acheni sheria ichukue mkondo wake. Kitendo cha kusema kwamba kawaumbua watu na hivyo na yeye akifanya kosa asishitakiwe huo sio utawala wa sheria. Sheria ni msumeno unakata pande zote. Kuwa mwandishi wa habari sio kigezo cha kutokushitakiwa!
 

Forum statistics

Threads 1,389,283
Members 527,879
Posts 34,022,069
Top