Jerry Muro amshukia Tundu Lissu

Jerry Muro amshukia Tundu Lissu

Habari za weekend wakuu

Hivi ni vigezo gani vinavyotumika kuchagua wakuu wa wilaya na mikoa mbona wana poor thinking capacity kiasi hiki.

Hivi jerry kweli ni waku zungumza maneno haya ni kweli tundu lissu anamuita msaliti na dawa yake ni kunyogwa inaleta picha gani katika taifa hili.

Hivi kweli V8, mshahara na nyumba ya serikali vinaweza kukufanya ukakosa utu na huruma kwa wanadamu wenzako ....

What goes around, always comes around.

Karma haitawaacha salama

Sent using Jamii Forums mobile app

Tatizo liko wapi..? Mbona kaongea vitu halisi tu, ww amekuingizia msumari wapi umekuuma?
 
Hivi siku hizi hakuna wazee wachawi zamani wakuu was mikoa na wilaya waliheshimu wanainchi hawakuwa na mbwebwe hivi yani mkiona wanaleta mbwebwe tu mnamlaza siku mbili chooni, akijifanya mkaidi mnamlaza juu ya mti akiwa mtupu, akijifanya mjuaji asubuhi anajikuta kajinyea tupo mtupu kati kati ya barabara kuu mjini

Sasa sijui wazee mnasubilia nini ebu fanyeji jambo
Iringa wamejaribu kijana akajikuta kalala malaloni na boxer ila hakuvunjiwa yai. Nasikia siku hizi hata Msigwa anamwamkia shikamoo. Ila wajeuri kama Jerry wanafaa kuvunjiwa yai kabisa. ( ingawa naambiwa hapo itakuwa kama Mamba kumayi, maana mchezo huo sio mpya kwake)
 
Ni ujinga wa hali ya juu kumtuhumu mtu aliyejeruhiwa kwa kiwango cha Tundu Lissu na kujaribu kumnyamazisha kwa kumwambia anaharibu. Nadhani hilo ndilo exactly analotarajia kuliona Tundu Lissu.

Niliandika haya: Tundu Lissu ni fursa kwa Serikali kuonesha ubora wake - JamiiForums
You're right madame! Nilikuwazia vibaya kuwa umezeeka kumbe bado upo smart upstairs! Hongera sana kwa utu na ubinadamu unaouonyesha kwa kipindi hiki. Laiti kama kungekuwa na wawili, watatu wenye hekima na busara pamoja na utu basi huko chamani utokako basi suala hili siyo tu lingekuwa limekwisha bali kusahaulika kabisa!
Binadamu yeyote mwenye utu kwa hakika hawezi hata mara moja kushangilia suala la Lissu bali kulikemea na kuungana katika maombi kwa muujiza uliomponya unadhihirisha uwepo wa Mungu aliye hai.
Hili ni onyo kutoka kwa Mungu kuwa kilichofanyika ni ubatili ma hivyo tutubu juu ya dhambi ile na kinyume chake tutaangamia tukipuuza!
 
Dawa pekee ya kumnyamazisha Lissu huko Duniani aliko ili aachane na kuituhumu serikali yake, dawa hiyo aliyenayo ni serikali yenyewe kujishughulisha na suala la Lissu ikiwa ni pamoja na ;

1.Serikali kutoa ushahidi usio na shaka wa mtu halisi aliyehusika kumshambulia Lissu

2. Serikali kuieleza Dunia walikokuwa walinzi waliokuwa zamu kulinda nyumba za serikali wakati Lissu anashambuliwa.

3. Serikali kuieleza Dunia zilikokwenda CCTV camera baada ya Lissu kushambuliwa.

Kwa nini serikali ndo inapaswa kuwa na majibu haya? Kwa sababu ndo pekee ina mamlaka ya kutoa majibu hayo na si mwingine!!! Hayo ndiyo maswali pekee ambayo Lissu amekuwa akiyauliza kila kwenye chombo cha habari cha kimataifa anachoalikwa!!
Kamanda unazungumza mambo usiyoyajua huoni soni!!!...'
 
Kwaio unataka wajinyonge kwa kujitia kitanzi wenyewe mkuu?
 
Tatizo liko wapi..? Mbona kaongea vitu halisi tu, ww amekuingizia msumari wapi umekuuma?
Punguza ujinga basi! Wewe ulifindishwa kuhukumu? Anayehukumu ni yule aliyekuumba na si yeyote awaye!
Huyaoni makosa ya muro? Anasisitiza Lissu kutubu huku yeye akimuhukumu kifo tena cha kunyongwa! Anasoma biblia ipi? Na kanisani ( kisomioni) anafuataga nini? Sunday school na fellowship ipi ilimfunda hivyo? Jerry katubu kwa matamshi yako haya yaliyomkarahisha Mungu na kama ulidhani unamkebehi na kumdhihaki Mungu ili umpendezeshe mtu basi, tegemea mapigo yasiyokoma kama yale aliyopigwa farao na jeshi lake kwani Mungu hadhihakiwi bali hutukuzwa!
 
Tatizo upande fulani haunaga hoja za msingi zaidi ya kuongea maneno ya kwenye kanga
 
Inahusianaje na hoja hii? By the way, ndiyo maana mlimzawadia makofi hadharani? Hamna aibu hata kidogo ninyi watoto wa kichupa! Na karma itawatafuna kwa kelele kama ukoma na sijui mtavifichaje mabutu ya madole yenu yaliyokatika! Hata maandiko juu ya wazazi na wazee hamyasomi?

Unajua Kashfa Za Ufisadi Za Huyu Babu?

Rejea Kashfa Za Madini Za Kampuni ya Mwananchi!

Kwa ufupi tu Huyu Mzee aliwahi kutapeliwa dili kubwa Sana akaogopa kumpeleka Mahakamani aliemtapeli kwa Kuwa lilikuwa dili
 
Usidanganye watu alikuwa John Malecela siyo Jaji Warioba danganya ambao hawana kumbukumbu. Wengine tunakumbuka sana na ni heshima ya Jaji Warioba ndiyo iliyosababisha Mh. Mkapa amchaguwe Jaji Warioba kuwa Mwenyekiti wa tume ya kufanya uchunguzi namna ya kupambana na rushwa hadi leo inaitwa tume ya Warioba na report yake ipo hadi kesho. Unatia hadi aibu kuandika uwongo kama huo.

Wewe Ni Mtoto Mdogo Sana
Wazee tukiwa tunaandika wajibu wako ni kuchukua Penseli, ufutio Na Daftari kuandika sio kubishana

Mzee Ally Hassan Mwinyi akiwa Rais kawahi kuvunja Cabinet yake Mara mbili

Mara ya kwanza ilikuwa 1990 Na Waziri Mkuu akiwa Joseph Sinde Warioba kwa Tuhuma Za kukithiri kwa Rushwa Kwenye Cabinet

Mara ya pili ilikuwa 1994 Na PM akiwa John Samweli Malecela Na sababu ikiwa Ni Mgogoro wa Serikal tatu Na Malecela kushindwa kumshauri ipasavyo Mzee Mwinyi Kwenye Sekeseke lile

Rudi Tena nikupe Darsa zaid
 
Zamani zile alikua msemaji wa klabu kongwe hapa nchini, kwa sasa ni mkuu wa wilaya, Ghagla kaibuka kua msemaji wa ziara ya TAL nchi za nnje! ngoja tuendelee kuangalia nani wengine wataibuka kuongelea ziara hiyo kwasababu inawagusa wengi.

Ila jamaa alivyomuongeaji ngoja tuone mpambano, Japo sidhani TAL atamjibu mana level zinatofautiana sana.

Yajayo yanafurahisha.

Sina mengi, Tafuta hiyo Youtube uangalie
Screenshot_20190211-065616_YouTube.jpeg
Screenshot_20190211-065607_YouTube.jpeg
Screenshot_20190211-065606_YouTube.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku hizi ma standard seven na division zeros ya form 4 yanadhani yamefiiika! Nchi kwa vituko haijambo kabisa.. vilaza ndo wanaongoza eti.. khaa!
 
Habari za weekend wakuu

Hivi ni vigezo gani vinavyotumika kuchagua wakuu wa wilaya na mikoa mbona wana poor thinking capacity kiasi hiki.

Hivi jerry kweli ni waku zungumza maneno haya ni kweli tundu lissu anamuita msaliti na dawa yake ni kunyogwa inaleta picha gani katika taifa hili.

Hivi kweli V8, mshahara na nyumba ya serikali vinaweza kukufanya ukakosa utu na huruma kwa wanadamu wenzako ....

What goes around, always comes around.

Karma haitawaacha salama

Sent using Jamii Forums mobile app

Achana nae huyo ni mwehu
 
Back
Top Bottom