Fascinating
Senior Member
- May 14, 2025
- 149
- 357
Jensen Huang amejiuzulu kama rais na Mtendaji Mkuu (CEO), na mjumbe wa bodi wa Nvidia, kuanzia sasa, na kuhitimisha miaka 33 iliyobadilisha kampuni changa ya kutengeneza 'graphics-cards' kuwa kampuni kuu katika enzi za Akili Mnemba (AI). CFO wa Nvidia, Colette Kress anakuwa CEO wa muda wakati bodi ikiendelea kutafuta mrithi wa kudumu.
Kujiuzulu kwa kushtukiza
Nvidia ilisema kujiuzulu kwa Huang kulifuatia uchunguzi huru kuthibitisha kama alikuwa amelengwa na operesheni ya ujasusi wa kigeni (Foreign espionage), hii ni baada ya kuibuka kwa ripoti za mahusiano ya nje ya ndoa yaliyomhusisha Alice Huang na kigogo wa afya wa Nvidia, Kimberly Powell. Kampuni hiyo ilisema haijapata sababu yoyote ya kuamini kuwa siri za kampuni au usalama wa taifa uliingiliwa, lakini tuhuma hizo zilisababisha uchunguzi mkali na shinikizo kubwa kwa bodi.
Mwenyekiti wa bodi Harvey Jones alimshukuru Huang kwa mchango wake na kusema shughuli za Nvidia na mipango ya bidhaa zitaendelea bila usumbufu wowote.
Urithi wa Huang ndani ya Nvidia
Huang alishiriki kuanzisha Nvidia mwaka 1993 pamoja na Chris Malachowsky na Curtis Priem. Chini ya uongozi wake, Nvidia iligundua na kufanya biashara ya Chip za kuchakata picha na graphics (GPU), ikiwezesha upatikanaji GPU kwa watumiaji wa kompyuta za kawaida kupitia CUDA, na kujenga msingi wa 'hardware' na 'software' kwa ajili ya mandeleo ya AI yanayotokea sasa.
Kukua kwa thamani ya Nvidia chini ya Huang ni wa kipekee sana: mapato ya mwaka wa fedha 2026 yalifikia dola bilioni 215.9, likiwa ni ongezeko la asilimia 65 mwaka hadi mwaka, huku mapato ya 'data-center' yakifikia dola bilioni 89.0, ambalo ni ongezeko la asilimia 117. Kampuni iliripoti faida halisi (net income) ya takriban dola bilioni 120 kwa mwaka huo wa fedha, ikisisitiza jinsi uamuzi wa Huang kuwekeza kwenye 'accelerated computing' ulivyobadilisha kabisa biashara ya Nvidia.
Musk anampango wa kumuajiri Huang?
Wakati ripoti zikiibuka kuwa bodi ya Nvidia inaweza kumwondoa Huang, chapisho la Zerohedge kule 'X' lilimsihi Elon Musk: "Elon, tafadhali muajiri Jensen." Musk alijibu, "Hiyo itakuwa ni heshima kubwa."
Jibu hilo lilisambaa kwa kasi mtandaoni kwa sababu liliwakutanisha kiongozi mashuhuri zaidi wa chipsi za AI wa Silicon Valley, na mjasiriamali maarufu zaidi wa AI na masuala ya anga za juu.
Musk hakutangaza cheo maalum, kampuni, au mpango wowote wa kumuajiri, lakini kauli hiyo ilionyesha heshima ya wazi kwa Huang hata wakati mzozo wa uongozi ndani ya Nvidia ukiendelea.

| Mafanikio | Kwa nini ilikuwa muhimu |
|---|---|
| Kushiriki kuanzisha Nvidia mwaka 1993 | Aliijenga kampuni kutoka kuwa kampuni changa (startup) ya 'graphics-chip' hadi kuwa jukwaa la kimataifa la kompyuta. |
| Kuzindua GPU mwaka 1999 | GeForce 256 ya Nvidia ilitangazwa kama GPU ya kwanza duniani, na kubadilisha kabisa 'graphics' za kompyuta na uchakataji wa pamoja (parallel computing). |
| Kutengeneza CUDA | Ilifanya chipsi za Nvidia kuweza kupangiwa programu (programmable) kwa ajili ya utafiti wa kisayansi na AI, na kutengeneza mfumo thabiti wa 'developers' ulioleta utawala wao kwenye ulimwengu wa AI. |
| Kuchochea mapinduzi ya AI | Chipsi za Nvidia kwa ajili ya 'data-centers' zikawa miundombinu mikuu kwa ajili ya kufundisha na kuendesha mifumo mikubwa ya AI (large AI models). |
| Kujenga kampuni ya dola trilioni 4 | Huang aliongoza Nvidia hadi ikawa moja ya kampuni zenye thamani kubwa zaidi duniani na nguvu inayoongoza kwenye uchumi wa AI. |