samirnasri
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 1,388
- 213
Jennister mhagama alifanya vizuri katika nafasi ya uenyekiti ndani ya bunge lililopita na aliendesha vikao vya bunge kwa mafanikio kuliko hata job ndugai na pengine kuliko hata anne makinda. Mhagama alikua mtu wa kwanza kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya unaibu spika nami niliamini angepata nafasi hiyo bila wasiwasi. Ghafla nikasikia zengwe la jina lake kutaka kuondolewa, mara nikasikia ameondoa jina lake kwa kile kilichosikika kua ni kuleta uwiano wa kijinsia ambao hata hivyo umekuwa ukitafsiriwa ndivyo sivyo. Baada ya kuondoa jina lake nilitegemea angepewa uwaziri au unaibu waziri lakini cha ajabu nimeshuhudia sophia simba akipewa uwaziri wakati jennister mhagama akiambulia patupu. Swali ninalojiuliza ni kwamba JE JENNISTER MHAGAMA SIO MWANAMTANDAO!!!. I SUBMIT...