Auz
JF-Expert Member
- Apr 6, 2016
- 13,843
- 11,782
Kama wanakula wote je?Nimewapa kazi mchunguze
Kama wanakula wote je?Nimewapa kazi mchunguze
Loh! Umenikumbusha Waziri fulani wa MADINI (RIP) ambaye alivyokua anaingia kwenye lift lazima wote muondoke apande peke yake. Na pia akihama Wizara anahama na meza, viti na dereva wake!Hivi bado ana ile tabia yake ya kutaka kupanda pekee yake kwenye lift za majengo ya taasisi yake? Akiingia kwenye lift wengine wote mtazuiwa kuingia.
Nikweli kabisa maana pamoja na walikuwa wapigaji lakini walifanya mamboDau,Mafuru,Msechu hakuna mbadala wao!Taasisi walizokua wanaziongoza zimekufa kifo cha mende muda sii mrefu zitakua omba omba.
Erio chaguo la Mkapa yupo hapokwa nguvu ya mkapa
Kimsingi hujawai kumuona lakini tatizo lako ni kupanda lift peke yake?Bora kumwona akiwa pekee yake kwenye lift. Mara kadhaa nilikuwa nashuhudia asubuhi walinzi wakiwazuia wengine wote wasiingie kwenye lift hadi imepeleke kwanza yeye akiwa pekee yake. Labda kama siku hizi kaacha huo utaratibu wake.
Nakubali mzee ni hasara kubwa sana sijui watafanyaje..Miradi ya haya mashirika ingeachwa imalizike. Haya mashirika yaliwekeza sana Dae kuhamia Dom kumesababisha hasara ambayo hawataisahau maisha
Andika kwa waziri, alafu nakilisha Magufuli: aione kwenye kablashaMheshimiwa Mhagama, hili dude NSSF litakufia na wewe utakwenda na maji.
Baada ya Dau kuweka miradi ya kifisadi alipoondoka miradi mingi imesimama na ni kwa sababu hajapatikana a right person kuongoza hili shirika.
Fitina Erio aliomfanyia Prof Kahyarara ili yeye achukue nafasi yake tunaijua, ila huyu dogo alikuwa keshaharibu huko PPF akishirikiana na idara ya HR.
Alifika wakati wakawa wanajilipa mamilioni ya pesa kila baada ya miaka miwili, mhasibu mkuu alipotaka kuhoji walimfukuza kazi. Taarifa zipo. Ni huyo Erio aliyumbisha PPF hadi kutaka kufa kabla Rais hujachukua hatua za kuunganisha.
Sasa yaliyoko NSSF kwa Erio yanaanza kutishia uhai wa shirika.
Waziri chip in ujue A&B za NSSF ya sasa.
Mshauri Rais amuondoe. Shauri lako.
naenda mimi sasa, nikapande nae hao walinzi uchwara nataka nikaonane naoBora kumwona akiwa pekee yake kwenye lift. Mara kadhaa nilikuwa nashuhudia asubuhi walinzi wakiwazuia wengine wote wasiingie kwenye lift hadi imepeleke kwanza yeye akiwa pekee yake. Labda kama siku hizi kaacha huo utaratibu wake.
Nimekuelewa mkuu.Erio hajawahi na wala kutaka kupanda lift peke ake huo ulikua utaratibu wa security company kumpandisha mkuu wa taasisi lift akiwa peke ake pamoja na walinzi hii hata taasisi nyingine wanafanya sana hasa SUMA JKT
Vibaraka wa Dau mnahaha sana tulieni dozi iwaingie hakuna kiongozi mwenye weledi na maarifa katika mifuko ya hifadhi kama Mzee Erio toka amekanyaga NSSF ametengeneza mifumo madhubuti ya ukusanyaji mapato na ulipaji wa mafao ambayo haukuwahi kuwepo nssf na pia amekomesha mambo ya unyanyasaji wa kidini na amefanya wafanyakazi wote kujiona ni sawa.
mwisho acheni kelele muacheni mteuzi wa Raisi Mr Erio afanye kazi period
Mkuu sijui ni kipi hapo ambacho haujaelewa? Ninachomaanisha ni kwamba bora kuonekana akiwa pekee yake kwenye lift maana kuna uwezekano wakati anaingia hakukuwa na watu wengine waliohitaji kuingia. Tatizo linakuja pale anapokuwa anataka kuingia na wengine wanaotaka kuingia wanakuwepo lakini walinzi wanawazuia wote ili bwana mkubwa aingie pekee yake hadi lift itakaporudi tena. Hayo maelekezo ya kuwazuia wengine yanakuwa aidha yametoka kwake au yameridhiwa na yeye.Kimsingi hujawai kumuona lakini tatizo lako ni kupanda lift peke yake?
Mkuu nakueleewa lakini haiwezekani tukawa tunajadili LIFT badala ya impact ya utendajiwake kazi. Unanilazimisha nijadili hili la lift ikiwa halina uzito wowote katika utendaji wake kazi.Mkuu sijui ni kipi hapo ambacho haujaelewa? Ninachomaanisha ni kwamba bora kuonekana akiwa pekee yake kwenye lift maana kuna uwezekano wakati anaingia hakukuwa na watu wengine waliohitaji kuingia. Tatizo linakuja pale anapokuwa anataka kuingia na wengine wanaotaka kuingia wanakuwepo lakini walinzi wanawazuia wote ili bwana mkubwa aingie pekee yake hadi lift itakaporudi tena. Hayo maelekezo ya kuwazuia wengine yanakuwa aidha yametoka kwake au yameridhiwa na yeye.
Huyu Erio ni mchapa kazi nzuri, anasikiliza sana wateja, mie ni shuhuda alitukuta UBUNGO Plaza NSSF Kinondoni tukifuatilia MADAI yetu, kwa kweli alitupa ushirikiano mkubwa kiasi ambacho SIKU hizi kuna mabadiliko chanya kwenye utoaji wa MAFAO. Kikwazo kikubwa FAO LA kujitoa, halitoki kwa professional, hii inatokana hali mbaya ya uchumi katika NSSF ambayo kwa namna moja ama nyingine zama za Dau zilizalisha hall mbaya mfuko kifedha. Erio jukumu lake kubwa ni kufufua hali ya mfuko kimapato. Mwacheni achape kaziMheshimiwa Mhagama, hili dude NSSF litakufia na wewe utakwenda na maji.
Baada ya Dau kuweka miradi ya kifisadi alipoondoka miradi mingi imesimama na ni kwa sababu hajapatikana a right person kuongoza hili shirika.
Fitina Erio aliomfanyia Prof Kahyarara ili yeye achukue nafasi yake tunaijua, ila huyu dogo alikuwa keshaharibu huko PPF akishirikiana na idara ya HR.
Alifika wakati wakawa wanajilipa mamilioni ya pesa kila baada ya miaka miwili, mhasibu mkuu alipotaka kuhoji walimfukuza kazi. Taarifa zipo. Ni huyo Erio aliyumbisha PPF hadi kutaka kufa kabla Rais hujachukua hatua za kuunganisha.
Sasa yaliyoko NSSF kwa Erio yanaanza kutishia uhai wa shirika.
Waziri chip in ujue A&B za NSSF ya sasa.
Mshauri Rais amuondoe. Shauri lako.
Urio baba yake mchaga tena Prof , mama huyo Urio ndo ndo dada yake na mzee mkapa...Dah bahati mbaya siyo mchagga. Tungepata story jf
Haitwi Urio anaitwa Erio acha fix. Angelikuwa mchagga huyo ungekuta huu uzi upo page ya 666Urio baba yake mchaga tena Prof , mama huyo Urio ndo ndo dada yake na mzee mkapa...
Hivi bado ana ile tabia yake ya kutaka kupanda pekee yake kwenye lift za majengo ya taasisi yake? Akiingia kwenye lift wengine wote mtazuiwa kuingia.
Siyo kuvizia vizia ni kwamba pesa hakuna.... Mimi nadhani serikali imechukua pesa za hili shirika na imegoma kuirudishaUlitakiwa uandike matatizo yanayoikabili NSSF ambayo unadhani mkurugenzi huyo ameshindwa kuyatatua. Tatizo mkubwa lililopo sasa ni shirika kushindwa kuwalipa wastaafu malipo yao ya mwezi kwa tarehe inayoeleweka. NSSF inatakiwa iwe wazi kuhusu mafao itoayo na taratibu zilizowazi kwa wachangiaji wa mfuko huo badala ya kuviziavizia.
Ni mtoto wa dada yake wa damu Mh. Benjamin Mkapa na hakika yuko hapo NSSF kwa nguvu yake. Mtaimba nyimbo zote na hapo hatatolewa kabisa. Ila nimefurahi eti kuwa alikuwa akiingia list PPF House alikuwa ni yeye tu mfalme hakuna kibaraka wa kupanda nao. Ni Mungu watu huyu. PPF alikuwa na skendo nyingi mno na ninakumbuka mpaka mitandaoni alipitishwa sana ila sema alikuwa kwa namna zote ni kuhakikisha anaweka sawa mambo ili mambo yake yasipate media attention. Mimi simo muulizeni aliyekuwa Mwanahabari!!!!
Halafu unamwaga upupu mwiingiii humo ndani akome...Dawa yake unakata fyuzi za umeme na jenereta abaki humo peke yake
Hakuna cha privilege ni tabia mbaya na misuse of power ya miafrika, huku ikishindwa ku deliver.....Mkurugenzi wa idara ya Misitu na nyuki, FBD, miaka hiyo, marehemu Prof Said Idd, pale Makao makuu tulikuwa tunapanga naye lift moja. Pia wakati ni mkurugenzi alikuwa anaitwa SUA kufundisha, sasa shangingi badala ya kupiga mafuta mpaka Morogoro yeye anaenda zake Ubungo anapanda Abood Bus, yaani hana makuu wala huu upuuzi wenu wa sijui privilege.Mkuu nakueleewa lakini haiwezekani tukawa tunajadili LIFT badala ya impact ya utendajiwake kazi. Unanilazimisha nijadili hili la lift ikiwa halina uzito wowote katika utendaji wake kazi.
Yyeye kama kiongozi ni ana privilege zake hili halina ubinshi, hata wewe Nyumbani kwako una privilege ambazo hakuna anayebishia, sabau nikiongozi wa familia yako. kwa maana hii sioni kosa yeye kupanda peke yake maana huenda ni makubaliano yao au sera ya utawala inasema hivyo.
Maana kama tutabishania lift, basi tubishabie sera za posho ambazo yeye kama kiongozi anapata posho kubwa kulio Afisa mwingine sasa mpaka hapa naona hoja ya lift ni mufilisi haina maana.
Mfano, sijajua iyo Ghorofa yao ilikua na floor ngapi lakini jee, kama yeye anaharaka ya kufika ofisini akiwa na call ya mamlaka ya uteuzi, wewe kwa hoja yako unataka apande lift moja na raia ambao watashuka kila ghorofa mpaka afike ofisini kwake? Mpaka hapo atakua amechelewa call ya mamlaka ya uteuzi.
Naomba tuajdili impactya utendaji wake tuache chuki za kijinga zisizo na mantiki.
FYI.. Mpaka Mifuko inakua Disolved yeye na PPF yake ndio walikua Mfuko ulio Stable kuliko yote. Sasa utasemaje hana jambo?
Apande mwenyewe kama nani? Kwani lifti ni jeneza useme utaingia mwenyewe!Hivi bado ana ile tabia yake ya kutaka kupanda pekee yake kwenye lift za majengo ya taasisi yake? Akiingia kwenye lift wengine wote mtazuiwa kuingia.
Kwaiyo unakataa Privilege sio? [emoji3][emoji3][emoji3] wewe changamsha genge hapa na mihemko yako ya mifano ya "miaka ile"Hakuna cha privilege ni tabia mbaya na misuse of power ya miafrika, huku ikishindwa ku deliver.....Mkurugenzi wa idara ya Misitu na nyuki, FBD, miaka hiyo, marehemu Prof Said Idd, pale Makao makuu tulikuwa tunapanga naye lift moja. Pia wakati ni mkurugenzi alikuwa anaitwa SUA kufundisha, sasa shangingi badala ya kupiga mafuta mpaka Morogoro yeye anaenda zake Ubungo anapanda Abood Bus, yaani hana makuu wala huu upuuzi wenu wa sijui privilege.