Jenista Mhagama: Rais amedhamiria kila mlengwa wa TASAF aishi maisha Bora

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kila mlengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini anaishi maisha bora kama ambavyo Serikali imekusudia.

Mhe. Jenista amesema hayo akiwa katika Kijiji cha Wiri na Ngumbaru Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro wakati akikagua utekelezaji wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini katika halmashauri hiyo.

Mhe. Jenista amesema, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani aliamua kuendelea kutekeleza Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini ili kuboresha maisha ya wananchi walio katika kaya maskini.

“Nimeenda kujionea mwenyewe namna walengwa wa TASAF walivyoanzisha miradi ya kufuga kuku, mbuzi na ng’ombe na wengine wamejenga nyumba za kuishi,” Mhe. Jenista amesisitiza.

Mhe. Jenista ameongeza kuwa, uamuzi huo wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan umewawezesha watoto wa walengwa wa TASAF kupata elimu bora na huduma bora za matibabu kupitia utekelezaji wa miradi ya elimu na afya ya TASAF na kuongeza kuwa, katika maeneo mengine walengwa wa TASAF wamefanikiwa kujiunga na bima ya afya inayowasaidia kupata huduma ya matibabu kwa urahisi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema, amejionea mafanikio ya walengwa wa TASAF wilayani Siha na kuongeza kuwa pamoja na mafaniko hayo lakini bado Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea na jitihada zake za kutafuta fedha ili zitumike kuboresha maisha ya Watanzania wengi zaidi.

Mhe. Kikwete amewataka Watanzania kuendelea kuwa na imani na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameonesha nia ya dhati ya kuboresha maisha ya wananchi anaowaongoza, hivyo walengwa wa TASAF hawana budi kumuunga mkono kwa kutumia vizuri ruzuku wanayoipata kuboresha maisha yao.

Naye, mmoja wa walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Ngumbaru wilayani Siha Bi. Kilei Kessy amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
WhatsApp Image 2023-03-05 at 16.36.37(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-05 at 16.36.39.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-05 at 16.36.39(2).jpeg
 
Back
Top Bottom